Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Niko hapa jijini Washington DC, mji mkuu wa Marekani, pamoja na mambo mengine, nimepata fursa ya kuushuhudia uchaguzi wa Marekani, ambapo nchi ya Marekani inaitwa The Biggest Democracy kumaanisha ni demokrasia kubwa kwasababu ilipata uhuru wake Julai 4, mwaka 1776 lakini Wamarekani ni wabaguzi wa kichini chini, wanaendekeza mfumo dume, hawataki kutawaliwa na rais mwanamke!. Huu ni ubaguzi!. Pia wana ubaguzi wa rangi wa racism, ni ma racist fulani hivi, na wanawabagua fulani wahamiaji!.
Wagombea wakuu wa uchanguzi huu wa Marekani ni Kamala Harris wa chama cha Democrat ambaye ni makamo wa rais wa sasa, na Donald Trump wa chama cha Republican, ambaye aliwahi kuwa rais wa Marekani na akafanya vituko vingi.
Matokeo ni, pamoja na vituko vyake vyote, Wamarekani wamemchagua tena Donald Trump na kumtosa Kamala Harris.
Moja ya sababu za Wamarekani kumchagua tena Trump, licha ya vituko vyake, lakini pamoja na mambo mengine, Wamarekani wameamua kumchagua tena Trump, kwasababu ni mgombea mwanaume, kuliko kumchagua mgombea mwanamke!. Huu ni ubaguzi m-baya wa gender discrimination!.
Hivyo pamoja ni jina kubwa la nchi ya Marekani kuitwa demokrasia kubwa, lakini bado inakabiliwa na udhaifu mkubwa wa ubaguzi wa mfumo dume.
Mara ya kwanza kwa Donald Trimp kushinda urais, ni alishindana na mgombea mwanamke, Hilary Clinton, mke wa aliyekuwa rais wa Marekani, Bill Clinton.
Kwa vile hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke kugombea urais, Marekani, Trump alisema maneno fulani ya udhalilishaji jinsia ya kike, hivyo aliposhinda urais, Wamarekani walionyesha bado hawajawa tayari kutawaliwa na rais mwanamke.
Chama cha Democrat kilipoamua kumsimamisha tena mgombea mwanamke kwenye uchaguzi wa mwaka huu, na Donald Trump akaamua kugombea tena!, ikitegemewa safari hii, Wamarekani watamchagua rais wa kwanza mwanamke kwasababu Trump vituko vyake wanavijua.
Matokeo yalipotangazwa kwa Trimp kushinda kiukweli mimi ni miongoni mwa tuliopigwa butwaa, na kupata bumbuwazi na matokeo haya ya uchaguzi wa Marekani.
Nikajiuliza kuwa kunawezekana hawa Wamarekani nimewaona kama ni majitu majinga ya ajabu kwa kwa kumchagua tena rais mwanaume yule yule mwenye vituko vya ajabu na vituko vyake wanavijua na bado wakamchagua!.
Wamarekani wameamua, kuliko kumchagua rais mwanamke, wakaamua kumtosa mwanamke na kumchagua rais mwanaume kwasababu tuu ya kugubikwa na ubaguzi wa mfumo dume.
Japo ni demokrasia kumchagua mgombea yoyote kwa sababu yoyote au hata bila sababu yoyote, bali ni kumpenda tuu, lakini sio demokrasia ya kweli kutokumchagua mgombea fulani mwenye sifa zote, lakini hachaguliwi kutokana na jinsia yake!, huu ni ubaguzi!.
Matokeo haya ya uchaguzi wa Marekani, yanauhusiano na uchaguzi mkuu wetu wa mwaka 2025, hivyo natoa wito kwa sisi wa Tanzania, tuyapokee matokeo haya na kuyachukulia kama ni fursa kwa Tanzania kuifundisha dunia demokrasia ya kweli.
Kwa vile mwakani, 2025, Tanzania tunafanya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, na tayari kuna chama kimoja kimeisha tangaza nia kwa kauli na matendo ya utaratibu wake wa ndani wa mserereko, kitamsimamisha mgombea mwanamke.
Kwa vile Tanzania imepata rais mwanamke kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, kufuatia lile tukio la Machi 17, 2021, lakini Watanzania walikuwa bado hawajawa tayari kuchagua rais mwanamke, hivyo uchaguzi wa 2025, macho ya dunia yatakuwa Tanzania.
Mnaonaje kama hiyo 2025, tuta ionyeshea Marekani na dunia kwa ujumla kuwa Tanzania ni wakomavu zaidi wa demokrasia, na tunaweza kufanya demokrasia ya kweli bila ya ubaguzi m-baya wa jinsia na kuutaa mfumo dume kwa Watanzania kuonyesha wanaweza kuchagua kiongozi wao bila kugubikwa na mfumo dume, na ubaguzi wa jinsia?
Hivyo Tanzania tuchangamkie fursa ya kuwa mwalimu wa demokrasia ya kweli kwa Wamarekani na dunia kwa kufanya maandalizi kamambe ya kuwaandaa Watanzania kuchagua rais mwanamke, na sababu za kuchaguliwa rais mwanamke, sio kuchaguliwa kwasababu ya gender yake, ya uanamke, bali awe amechaguliwa kwasababu ya uwezo wake wa urais na uongozi.
Sio vema kumchagua mtu hana uwezo, lakini tumchague tuu kwa kumhurumia kwa sababu ni mwanamke, lakini pia sio vema, kutokumchagua mtu ana sifa zote, na uwezo lakini kumbe ni mwanamke!
Tuyatumie matokeo ya uchaguzi wa Marekani kama shamba darasa la demokrasia ya kweli 2025
Paskali
Washington DC
Marekani.