Je, Wajua? Wamarekani ni Wabaguzi wa Kichinichini. Wanaendekeza Mfumo Dume, Ubaguzi wa Jinsia, Racism na Kuwabagua Wahamiaji

Je, Wajua? Wamarekani ni Wabaguzi wa Kichinichini. Wanaendekeza Mfumo Dume, Ubaguzi wa Jinsia, Racism na Kuwabagua Wahamiaji

Heshima yako uliyojijengea kwa kipindi kirefu unataka kuipoteza kirahisi Sana. Acha kuwapangia wamarekani nini cha kufanya na badala yake Njoo hapa Bongoland ukemee uovu unaofanywa na chama tawala kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kosa la Paschal ni kuishi kwa kutegemea hisani ya mtu, anatakiwa ajiulize nchi yetu bunge na serikali vinaongozwa na wanawake nini cha maana wamefanya zaidi ya kuruhusu ufisadi wa kutisha? kwanini na sisi tusitumie rasilimali zetu kuwa matajiri kama Marekani?
 
Mzee wangu umeputanga, ukiwa unaandika kitu cha hovyo hata points za maana unakua huna unarudia kile kile post nzima.

Sasa mkuu hiyo si ndio demokrasia yenyewe, wewe mwenyewe umeelezea maana ya demokrasia halafu tena unawapangia wamchague nani kwa sababu zako binafsi.

Kwahiyo hata hapa Tz 2025 wasiomchagua mama ni mazuzu?
(Na hili ndo lengo la uzi wako).
 
The are not racist, they are just being nationalistic,
Hawana tofauti na
Sisi wenyewe wa bongo, ni wabaguzi sana,
Ukiwa na asili ya kagera, unaonekana kama mnyarwanda, waha wakigoma, huchukuliwa kama warundi!
Kwa hili nakukatalia sisi Watanzania sio wabaguzi kivile ndio maana japo sheria inasema kwa baadhi ya nafasi, mgombea lazima awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa kwa wazazi wote Watanzania, lakini tumekuwa na viongozi hawakuzaliwa Tanzania, baba zao halisi , the biology fathers sio Watanzania, walizaliwa huko waliko zaliwa na kuja Tanzania wakiwa wadogo, mama zao wakaolewa na Watanzania, watoto hao wakaandikishwa shule kwa majina ya baba zao wa kufikia, na tukawapa uongozi wa juu, huku tunajua sio Watanzania na tukawaacha! Naomba nisiwataje majina maana hawawezi kujitetea!.

Japo Tanzania tuna mipaka mingi lakini Kagera ndio the most notorious, mtafute Mkuu britanicca kuhusu kitoto fulani cha Banyamulenge kikapewa jina la kihaya la Katto!.

Sasa hivi kuna hawa banyamulenge wengine wawili, wanakwenda vizuri, kuna watu tunawajua ni Banyamulenge lakini hatuwataji wala kuwasema kwasababu they are so good, bright and brilliant, hivyo waache wawe nchi yetu ipate maendeleo, kwasababu kuna vitu sisi wenyewe, hatuviwezi, tunahitaji kusaidiwa na watu wa jirani zetu ambao kiukweli they are so good!. Thread 'Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu?' Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu?

P
 
Mzee wangu umeputanga, ukiwa unaandika kitu cha hovyo hata points za maana unakua huna unarudia kile kile post nzima.

Sasa mkuu hiyo si ndio demokrasia yenyewe, wewe mwenyewe umeelezea maana ya demokrasia halafu tena unawapangia wamchague nani kwa sababu zako binafsi.

Kwahiyo hata hapa Tz 2025 wasiomchagua mama ni mazuzu?
(Na hili ndo lengo la uzi wako).
Aya yako ya mwisho ndilo hasa lengo la bwana huyu...
 
images (5).jpeg


Pascal Mayalla kwanini usupport ushoga ? Na kwanini uamini gender balance na useme wamarekani hawakumchagua halis kwasabu ya jinsia, je wanaume nao wakisema trump hajachaguliwa kwasabu ni mwanaume kama halisi angeshinda ?

Siasa za kutapatapa ni mbaya sana, nnchi zetu zilikuwa zinashindwa kupinga direct ushoga kwasabu ya Democratic, now watatoa sauti, na misaada ya janja janja tutaiskia tu.

Mkuu wamerakani sio kama sisiem mnaoangalia matumbo yenu, kila kitu ndiomana hamuendi mbele mpaka mgongwe kama patasi kwamujibu wa bwege,
Tizama Marekani ilipoteza hata hofu ya mungu, ni very bad deepstate inatumia gender na rangi ili wapenetrate.
images (6).jpeg

Unachagua vipi chama kinachonyima watoto haki ya kuishi ?
Unasapoti vipi chama kinachopromote LGBTQ ?

Shule za watoto zinazosupport LGBTQ zilikuwa zinafadhiliwa na hao hao Democratic,

images (7).jpeg


But-Johnny-Cant-Spell-G-A-Y-1.jpg
 
Wanabodi,

Niko hapa jijini Washington DC, mji mkuu wa Marekani, pamoja na mambo mengine, nimepata fursa ya kuushuhudia uchaguzi wa Marekani, ambapo nchi ya Marekani inaitwa The Biggest Democracy kumaanisha ni demokrasia kubwa kwasababu ilipata uhuru wake Julai 4, mwaka 1776 lakini Wamarekani ni wabaguzi wa kichini chini, wanaendekeza mfumo dume, hawataki kutawaliwa na rais mwanamke!. Huu ni ubaguzi!. Pia wana ubaguzi wa rangi wa racism, ni ma racist fulani hivi, na wanawabagua fulani wahamiaji!.

Wagombea wakuu wa uchanguzi huu wa Marekani ni Kamala Harris wa chama cha Democrat ambaye ni makamo wa rais wa sasa, na Donald Trump wa chama cha Republican, ambaye aliwahi kuwa rais wa Marekani na akafanya vituko vingi.

Matokeo ni, pamoja na vituko vyake vyote, Wamarekani wamemchagua tena Donald Trump na kumtosa Kamala Harris.

Moja ya sababu za Wamarekani kumchagua tena Trump, licha ya vituko vyake, lakini pamoja na mambo mengine, Wamarekani wameamua kumchagua tena Trump, kwasababu ni mgombea mwanaume, kuliko kumchagua mgombea mwanamke!. Huu ni ubaguzi m-baya wa gender discrimination!.

Hivyo pamoja ni jina kubwa la nchi ya Marekani kuitwa demokrasia kubwa, lakini bado inakabiliwa na udhaifu mkubwa wa ubaguzi wa mfumo dume.

Mara ya kwanza kwa Donald Trimp kushinda urais, ni alishindana na mgombea mwanamke, Hilary Clinton, mke wa aliyekuwa rais wa Marekani, Bill Clinton.

Kwa vile hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke kugombea urais, Marekani, Trump alisema maneno fulani ya udhalilishaji jinsia ya kike, hivyo aliposhinda urais, Wamarekani walionyesha bado hawajawa tayari kutawaliwa na rais mwanamke.

Chama cha Democrat kilipoamua kumsimamisha tena mgombea mwanamke kwenye uchaguzi wa mwaka huu, na Donald Trump akaamua kugombea tena!, ikitegemewa safari hii, Wamarekani watamchagua rais wa kwanza mwanamke kwasababu Trump vituko vyake wanavijua.

Matokeo yalipotangazwa kwa Trimp kushinda kiukweli mimi ni miongoni mwa tuliopigwa butwaa, na kupata bumbuwazi na matokeo haya ya uchaguzi wa Marekani.

Nikajiuliza kuwa kunawezekana hawa Wamarekani nimewaona kama ni majitu majinga ya ajabu kwa kwa kumchagua tena rais mwanaume yule yule mwenye vituko vya ajabu na vituko vyake wanavijua na bado wakamchagua!.

Wamarekani wameamua, kuliko kumchagua rais mwanamke, wakaamua kumtosa mwanamke na kumchagua rais mwanaume kwasababu tuu ya kugubikwa na ubaguzi wa mfumo dume.

Japo ni demokrasia kumchagua mgombea yoyote kwa sababu yoyote au hata bila sababu yoyote, bali ni kumpenda tuu, lakini sio demokrasia ya kweli kutokumchagua mgombea fulani mwenye sifa zote, lakini hachaguliwi kutokana na jinsia yake!, huu ni ubaguzi!.

Matokeo haya ya uchaguzi wa Marekani, yanauhusiano na uchaguzi mkuu wetu wa mwaka 2025, hivyo natoa wito kwa sisi wa Tanzania, tuyapokee matokeo haya na kuyachukulia kama ni fursa kwa Tanzania kuifundisha dunia demokrasia ya kweli.

Kwa vile mwakani, 2025, Tanzania tunafanya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, na tayari kuna chama kimoja kimeisha tangaza nia kwa kauli na matendo ya utaratibu wake wa ndani wa mserereko, kitamsimamisha mgombea mwanamke.

Kwa vile Tanzania imepata rais mwanamke kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, kufuatia lile tukio la Machi 17, 2021, lakini Watanzania walikuwa bado hawajawa tayari kuchagua rais mwanamke, hivyo uchaguzi wa 2025, macho ya dunia yatakuwa Tanzania.

Mnaonaje kama hiyo 2025, tuta ionyeshea Marekani na dunia kwa ujumla kuwa Tanzania ni wakomavu zaidi wa demokrasia, na tunaweza kufanya demokrasia ya kweli bila ya ubaguzi m-baya wa jinsia na kuutaa mfumo dume kwa Watanzania kuonyesha wanaweza kuchagua kiongozi wao bila kugubikwa na mfumo dume, na ubaguzi wa jinsia?

Hivyo Tanzania tuchangamkie fursa ya kuwa mwalimu wa demokrasia ya kweli kwa Wamarekani na dunia kwa kufanya maandalizi kamambe ya kuwaandaa Watanzania kuchagua rais mwanamke, na sababu za kuchaguliwa rais mwanamke, sio kuchaguliwa kwasababu ya gender yake, ya uanamke, bali awe amechaguliwa kwasababu ya uwezo wake wa urais na uongozi.

Sio vema kumchagua mtu hana uwezo, lakini tumchague tuu kwa kumhurumia kwa sababu ni mwanamke, lakini pia sio vema, kutokumchagua mtu ana sifa zote, na uwezo lakini kumbe ni mwanamke!

Tuyatumie matokeo ya uchaguzi wa Marekani kama shamba darasa la demokrasia ya kweli 2025

Paskali
Washington DC
Marekani.
Mbona simpo sana mkuu, usiumie kihivyo, waonyeshe kwamba wewe siyo mbaguzi, kwa kuanza kuongozwa na mkeo
 
US itabakia US - kamwe hawatakupa kazi ya kuliongoza Taifa lao kwa majaribio ya Gender bali ni kwa uwezo wako na kwa sera za chama chako kuhusu mambo muhimu yanayowapa challenges kwa wakati huo - na hicho ndiyo wamekifanya.
 
Mkuu Richard ,kwanza asante kwa kuchangia uzi wangu huu, pili asante kwa objectivity yako kwenye hili la kushindwa kwa Kamala, natamani chama cha the Democrat 2028 kije kimsimamishe Michelle Obama ndipo mtanielewa, naendelea kusisitiza hawa Warekani ni majitu majinga ajabu kutomchagua mwanamke, kitendo cha the biggest democracy kuwa wabaguzi kwa kumtosa mwanamke, Tanzania yukitumie kama fursa ya kujionyesha jinsi tulivyo na akili kuliko Wamarekani kwa kuchagua rais mwanamke come 2025

P
Advocate acha kuficha white kwa mgongo wa wamarekani. Waliopita Havana wameshakuelewa
 
Fedheha
 

Attachments

  • b3a34e7e631270a9e73fdd13db687369.mp4
    3.6 MB
  • watermark-51a3cc01acd06eefe8d1d23a20c76918_0.jpeg
    watermark-51a3cc01acd06eefe8d1d23a20c76918_0.jpeg
    516.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom