Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

Siasa au Dini πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mwanzo 1:26
[Kisha Mungu akasema, β€œTumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.”]

kama ni mfano wake kwa nini maneno yao yasiwe mfano wakeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sauti ya wengi ni sauti ya mungu kwakuwa na tec ni jopo la watu wengi hivyo ni sauti ya mungu
Sio kweli.Kwa MUNGU huyu ninayemjua mimi (YAHWEH) hana wengi wape.Cha kwake huwa kinapendwa na wachache.Mfano:gharika la enzi ya Nuhu waliokolewa watu 8 tu,Sodoma na Gomola ilipoangamizwa kwa moto waliokolewa watu 3 tu,Enzi za Danieli kule Babeli walipoambiwa wasujudu mbele ya sanamu ya Nebuchadneza,watu wengi walisujudu isipokuwa vijana watatu tu,Meshaki,Shadraki na Abednego.Sasa Vipi wewe utuambie sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU!Ni MUNGU yupi unayemzungumzia! MUNGU (YAHWEH) yeye anatutaka watu tunaojinasibu kumfuata tutii mamlaka(Warumi 13:1-5).Labda ikitokea mamlaka ikatoa amri inayopingana na amri mojawapo ya MUNGU kama kutulazimisha kufanya kazi za kiserikali siku ya sabato,ndipo tunaposema;"imetupasa kumtii MUNGU kuliko wanadamu(matendo 5:29).Lkn suala la bandari linapingana Vipi na sheria ya MUNGU iliyoko kwenye kutoka 20:1-17!
 
Unazani haelewi? Anaelewa sana hata hivyo umemjibu kiungwana sana fala huyu. NISAMEHE KAMA NITAKUWA NIMEKUCHAFULIA COMMENT YAKO
 
Kama siasa zote asili yake ni BIBLIA, according to the book of Genesis, 1&2Samwel, 1&2 Kings , Exodus, Daniel, Isaiah,Waamuzi nk nk,

Unawezaje kuutenga waraka wa TEC na Neno la Mungu?

Sikio lisizidi KICHWA Paskali.
Sijawahi kusikia Mkatoliki Mpumbavu wa kiwango hiki. Siasa na Uongozi vyote asili yake ni dini kulingana na Biblia ambayo Leo amethibitisha alikuwa anaiamini Ila Kwa maslahi binafsi haiamini tena.
 
Altare? sijuia kama uliwahi kuingia kanisani na unazijua sehemu za kanisa vizuri. Bado kidogo uatatwambia

ni kasiki la kuwekea sadaka
 

Attachments

  • 1693233942779.png
    9.9 KB · Views: 1
Kwa hiyo kwa sababu bandari haipo kwenye Biblia, basi mnajiona mna haki ya kuzichezea raslimali zetu kwa kuwauzia wageni siyo!!

Hakika umepotoka pakubwa sana! Tambua tu jukumu la viongozi wa dini kukemea maovu, halikuanzishwa na TEC! Soma Biblia kwa umakini halafu ujionee mwenyewe ni mara ngapi viongozi wa imani kwa nyakati tofauti waliwakemea watawala waliokiuka maadili ya utawala wao.
 
Siliza rais ndiye mwenye dhamana -heshimu mamlaka
 
Kama siasa zote asili yake ni BIBLIA, according to the book of Genesis, 1&2Samwel, 1&2 Kings , Exodus, Daniel, Isaiah,Waamuzi nk nk,

Unawezaje kuutenga waraka wa TEC na Neno la Mungu?

Sikio lisizidi KICHWA Paskali.
Enzi za viongozi wa dini kuwa viongozi wa jamii yote, zimekwishapita karne nyingi nyuma. Katika karne hizo dini ilikuwa nyenzo ya biashara.

Kwa karne yetu, Dini ni moja kati ya nyenzo za dola.

Utake ndio hivyo, usitake ndio. Huu ndio ukweli mchungu. comte
 
Siliza rais ndiye mwenye dhamana -heshimu mamlaka
Kwani huyo Rais anatokana na nini? Hayo mamlaka uliyotaja hapa, ameshushiwa kutoka mbinguni! Au yametokana na sisi wananchi?

Na kama yametokana na sisi wananchi, je kuna kosa tunapolalamikia mikataba isiyo na manufaa kwa nchi?
 
Nimesoma lakini sijaona hoja yako ni ipi?

The claim which you assert, and which I deny, is that, there is separable etiological connection between a creator and its creature.

You have not defended your case yet!
We are not talking about creationβ€”the creator and the creatures. We are talking about politics and religion; do they have a soil and blood relationship? My answer is no; the two do not mix; they are social constructs, and God does not even know them.
 

Sorry!
A polity and religion are natural societies (Refer to: Thomas Aquinas' Political Philosophy).
They are not conventional societies
God knows them.
Start again.
 
Mimi nadhani Maaskofu hawana kosa, kawaida duniani ni kumwamini mtendaji aliye chini yako kwa vile atakuwa na data zaidi na muda mwingi zaidi kutafakari. Fr Kitima kawasaliti, katumia imani yao kupenyeza mambo ya CUADEMA. Ulimsikia akisema Mkataba huu unawapa Waarabu haki ya kibomoa Kanisa la St Joseph? Hili haliongezi afya wala shibe, ni chuki tupu kama tulizosikia kwa Wahutu. Baadaye akasema Watanzania "walio wengi" hawataki Mkataba, kajuaje? Ni maneno ya CHADEMA, kada wa CHADEMA aliona nafasi nzuri kutangaza pipozpawa. Kumbuka pia alikuwa ni msemaji kule Temeke kumtukana Rais, hakuna Askofu aliyejua hilo. Ni mtu mmoja asiwakwaze Watanzania.

Mie ni whitefather tuna watakatifu 22 wafiadini: Papri Mapera hakuwahi kumtukana Kabaka. Hili la bandari si la Imani Katoliki bali ni la sensa ya Padri Kitima kudai ni Watanzania walio wengi.
 
Historia inakukatalia
Toka zamani dini ilikuwa sehemu ya watu- Wayahudi kwa mfano, kama ilivyo kwa wasukuma. Yesu alikpokuja ukaibuka Ukristo ( Mtendo ya Yesu+ Uyahudi). Alipoondoka wakristo (Wafuasi wa YESU) wakaanza habari ya kueneza ukristo nje ya Uyahudi, wakapata upinzani kutoka kwenye mamlaka. Kumbuka wakati huo kila mahala ni utawala wa Kirumi. Walipoweza kumnasa mrumi -ukapatikana muungano tena wa dola na dini ( wakristo wa Roma- RC). Kulipokuja vuguvugu la jamii mbalimbali kujitawala,dola mpaya zikajitenga na Roma na roma yenyewe ikaizaa VATICAN ndiyo hii dhana na kutenganisha dola na dini ikaanza kupigiwa chapuo.
Kama unavyosema leo dunia ni jamii chotara, siyo ethnical - ukiunganisha dini na dola utapata upinzani tu. Ndiyo maana tunasema DINI wafanye yao NA serikali ifanye yake. Halafu hawa TEC Kitima wanataka kuwa kote kote- wanatukwaza na kutuweka majaribuni; hivi uzinzi tumeacha baada ya kuwasikia hadi waache kuusema sasa warukie bandari? Bandari iko wapi kwenye hizo amri kumi za Mungu?
 
I DID NOT KNOW WHETHER PASCAL MAYALA WAS THAT MUCH STUPID.YOU HAVE BEEN FIGHTING FOR PRESIDENTIAL APPOINTMENT FOR SIX YEARS,LITTLE DID YOU KNOW THAT THE QUESTION YOU ASKED MAGUFULI REGARDING TO THREE ARMS OF THE STATE IS THAT WHICH PUT YOU TO THE STREET TO DATE. AMKA!!!
 
Bado unaendelea kuhangaika na waraka wa TEC ? Au kwa sababu kuna nafasi za teuzi ziko wazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…