Je, Wakatoliki Kuimba na kucheza nyimbo za Walokole ni dhambi?

Je, Wakatoliki Kuimba na kucheza nyimbo za Walokole ni dhambi?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Ni dhambi kwa Wakatoliki kuimba au kucheza nyimbo za injili kutoka kwa madhehebu mengine (ikiwemo za walokole) toka TAG, kama zina ujumbe unaompa Mungu utukufu.

Kanisa Katoliki linakataza kusikiliza au kuimba nyimbo za Wakristo wengine mradi tu mashairi yake hayaendi kinyume na imani na maadili ya Kikristo.?

Kuhusu sababu zinazofanya nyimbo hizo ziimbwe kwenye harusi, magari, na majumbani lakini zisipigwe kanisani (kwenye Misa), kuna sababu kuu zifuatazo:

Misa ya Katoliki ni Liturjia takatifu iliyoandaliwa wa warumi toka italia , Kila kitu kinachofanyika kanisani wakati wa Misa kina taratibu madhubuti (Liturjia) kilichoandaliwa na warumi na kina mwongozo kutoka Roma. Nyimbo za Misa lazima ziendane na sehemu ya Misa husika na ziwe zimeidhinishwa na mamlaka ya Kanisa ili kulinda mafundisho sahihi ya imani.

Maisha ya nje ya Kanisa kwa mkatoliki , kama Harusi, magari, na majumbani ni maeneo ya kijamii na kifamilia. Kwenye maeneo haya, waumini wana uhuru wa kufurahia sanaa, muziki, na burudani mbalimbali za Kikristo bila kubanwa na sheria za kiliturjia?

Unaweza kumpa lift padre ukiwa unapiga nyimbo za Rose Mhando , Jimmy Kimutuo, Agape Gospel Band, Kilimanjaro Revival choir, ?

Nyimbo za Walokole zina mdundo wa kuchangamka na ni Nyimbo nyingi za injili za walokole zina midundo inayofaa kwa kumsifu Mungu kama Daudi alivyofanya, sherehe, kucheza, na kufurahia. Kwenye harusi au nyumbani, watu wanahitaji mazingira ya sherehe na changamko, jambo ambalo nyimbo hizo hulileta vizuri sana huku za kikatoliki hazichezeki na zina kinanda na ngoma zinazofanana miaka na mikaka.
 
Nyimbo nyingi za wakatoliki ziko vizuri.... hasa zinazohusu kitabu cha zaburi.... zimetulia vizuri sana...
 
Back
Top Bottom