Je, walimu ndiyo kundi la watumishi, wasio na mshikamano, wasiojua kesho yao?

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
10,508
Reaction score
23,368
Walimu: Injini ya Maendeleo au Mashine Isiyotambua Thamani Yake?

Leo nimeketi na kutafakari kwa kina. Nimejiuliza swali gumu lakini la lazima:
Je, walimu ndiyo kundi la watumishi wajinga, wasio na mshikamano, wasiojua kesho yao?

Ni swali chungu, lakini si matusi—ni mwaliko wa kujitazama upya. Walimu tunategemewa kama injini ya maendeleo ya taifa. Tunafundisha madaktari, wanasheria, marais, na hata wachumi wanaotunga sera. Lakini kwa nini sisi wenyewe tunabaki nyuma, tukikubali kunyonywa bila kupaza sauti?

Hoja zangu zimejikita kwenye maswala ya Mikopo,Walimu Tunakatwa Zaidi, Tunakopeshwa Kwa Riba Kubwa nk,huku sisi wenyewe tuna benki yetu ambayo tulilaghaiwa kuwa itakuwa mkombozi kwetu.

Leo nimepitia mfumo wa ESS na kuchunguza taasisi zinazotoa mikopo kwa watumishi wa umma. Matokeo yamenishtua kabisa kwani SACCOS ya Uhamiaji Riba ya mkopo ni asilimia 12 kwa wanachama wao, Benki ya Azania: Inakopesha kwa asilimia 15.5 kama riba kwa mtumishi yeyote wa umma,wakati huo dude Mwalimu Commercial Bank,Benki yetu sisi walimu. Tunachangia zaidi ya TSh 20,000 kila mwezi kama ada ya ya uanachana lakini riba ya mkopo ni asilimia 17—sawa na benki za kibiashara kama NMB na CRDB!

Je, hii si dhuluma ya kiuchumi? Benki inayojengwa kwa jasho letu inatunyonya kuliko taasisi za nje. Tunakubali kwa sababu hatuna mshikamano wa kutosha kuhoji au kudai mabadiliko. Nabaki kujiuliza tatizo ni Nani? Serikali, Benki, au Walimu Wenyewe? Ni rahisi kulaumu serikali au benki, lakini ukweli ni kwamba Kukosekana kwa umoja miongoni mwa walimu kunawapa nafasi wengine kututumia kwa maslahi yao, Vyama chetu cha walimu na taasisi yetu ya kifedha(Mwalimu commercial Bank) inaonekana kuendeshwa kwa utashi wa kisiasa au kibiashara, si kwa maslahi ya walimu(wakopaji) hivyo nasema Ukimya wetu ni kibali cha kuendelea kunyonywa.

📢 Nawasihi Walimu wenzangu Tuamke!,Walimu wenzangu, huu si wakati wa kulalamika tu. Ni wakati wa Kuhoji kwanini taasisi /Bank yetu inatutoza riba kubwa wakati Kila mwezi unachukua zaidi ya Bilioni Moja Toka kwenye mishahara yetu. Pia tudai uwazi wa matumizi ya michango yetu ikiwezekana uasi nchi nzima uanzishwe dhidi ya CWT.

Hitimisho,Walimu tuamke. Tujitambue. Tujipange. Tujitete.
 
Ukiacha ujinga wa walimu, wafanyakazi wengne waliobaki uko serikalni 99% ni wezi hivo kimantiki hakuna tofaut baina yao
 
Please Moderator rudisheni heading niliyokuwa nikeweka ambayo ni Je, walimu ndiyo kundi la watumishi wajinga, wasio na mshikamano, wasiojua kesho yao? ,neno ujinga sio tusi,lakini pia iko katika Mfumo wa swali ambao ninahitaji majibu,sioni haja ya kuedit heading
 
Tuamke,tudai haki!

Nimesikitika sana ujue!

Mwalimu aache kufundisha vijana Kwa ueledi akadai haki zake kwenye majukwaa na maandamano!!

Majasusi,watunga sera,kwenye kupanga mstakabali wa kesho wa taifa hili wanaacha walimu wanyanyaswe sio Hadi wasldai haki zao kwa jasho na damu ndio wasikilizwe wapate haki zao!!

Kweli!!?

TATIZO NI PALE SIASA ILIPOPEWA KIPAUMBELE KULIKO TAALUMA,HAYA YOTE YASINGE KUWEPO YAANI MAPESA YAMEWEKEZWA KWENYE SIASA KULIKO TAALUMA MTAMBUKA KWENYE TAIFA!

MWALIMU HAPASWI kuingia bars baraninkudai haki Bali kila kitu kingefanywa kuwa SAWA na wenye maamuzi wa mstakabali wa taifa hili!!

Kama wait walifeli kuliona hili basi tatzo hili limetengenezwa kiufundi Hali iwe hivyo!!

Mwanasiasa akistaafu apate million zaidi ya 200 halafu mtaaluma astaafu apate million 70 n.k!!
 
Please Moderator rudisheni heading niliyokuwa nikeweka ambayo ni Je, walimu ndiyo kundi la watumishi wajinga, wasio na mshikamano, wasiojua kesho yao? ,neno ujinga sio tusi,lakini pia iko katika Mfumo wa swali ambao ninahitaji majibu,sioni haja ya kuedit heading
Unaita wenzako wajinga!
Hivi kuwa mwanachama wa CWT ni lazima?
 
Unaita wenzako wajinga!
Hivi kuwa mwanachama wa CWT ni lazima?
Maana ya “Ujinga”Kimsingi, ujinga ni hali ya kutokujua jambo fulani. Si lazima iwe kosa la mtu—inaweza kuwa matokeo ya kukosa fursa ya elimu, taarifa, au uzoefu. Katika muktadha wa elimu au maarifa, mtu mjinga ni yule ambaye hajafundishwa au hajapata maarifa fulani, lakini anaweza kufundishwa na kuelewa.

⚠️ Je, ni Tusi?
La, si tusi ikiwa linatumika kuelezea hali ya kutokujua kwa lengo la kusaidia au kuelimisha. Mfano: “Wengi hawajui madhara ya mikopo ya riba kubwa—ujinga huu unatuumiza.”

Ahsante
 
Ila kwenye vikao na mikutano huwa mna makelele mengi na ujuaji kama gunia nne Matokeo sifuri bin sufuri binti sufuria.
 
Maana ya “Ujinga”Kimsingi, ujinga ni hali ya kutokujua jambo fulani. Si lazima iwe kosa la mtu—inaweza kuwa matokeo ya kukosa fursa ya elimu, taarifa, au uzoefu. Katika muktadha wa elimu au maarifa, mtu mjinga ni yule ambaye hajafundishwa au hajapata maarifa fulani, lakini anaweza kufundishwa na kuelewa.

⚠️ Je, ni Tusi?
La, si tusi ikiwa linatumika kuelezea hali ya kutokujua kwa lengo la kusaidia au kuelimisha. Mfano: “Wengi hawajui madhara ya mikopo ya riba kubwa—ujinga huu unatuumiza.”

Ahsante
1000176358.jpg

Ndiyo maana moderator amelitoa
 
Kwa mishahara hii ya tarakimu sita ,ofsa hata huku idara nyingine ni hayo hayo tu.
 
Walimu: Injini ya Maendeleo au Mashine Isiyotambua Thamani Yake?

Leo nimeketi na kutafakari kwa kina. Nimejiuliza swali gumu lakini la lazima:
Je, walimu ndiyo kundi la watumishi wajinga, wasio na mshikamano, wasiojua kesho yao?

Ni swali chungu, lakini si matusi—ni mwaliko wa kujitazama upya. Walimu tunategemewa kama injini ya maendeleo ya taifa. Tunafundisha madaktari, wanasheria, marais, na hata wachumi wanaotunga sera. Lakini kwa nini sisi wenyewe tunabaki nyuma, tukikubali kunyonywa bila kupaza sauti?

Hoja zangu zimejikita kwenye maswala ya Mikopo,Walimu Tunakatwa Zaidi, Tunakopeshwa Kwa Riba Kubwa nk,huku sisi wenyewe tuna benki yetu ambayo tulilaghaiwa kuwa itakuwa mkombozi kwetu.

Leo nimepitia mfumo wa ESS na kuchunguza taasisi zinazotoa mikopo kwa watumishi wa umma. Matokeo yamenishtua kabisa kwani SACCOS ya Uhamiaji Riba ya mkopo ni asilimia 12 kwa wanachama wao, Benki ya Azania: Inakopesha kwa asilimia 15.5 kama riba kwa mtumishi yeyote wa umma,wakati huo dude Mwalimu Commercial Bank,Benki yetu sisi walimu. Tunachangia zaidi ya TSh 20,000 kila mwezi kama ada ya ya uanachana lakini riba ya mkopo ni asilimia 17—sawa na benki za kibiashara kama NMB na CRDB!

Je, hii si dhuluma ya kiuchumi? Benki inayojengwa kwa jasho letu inatunyonya kuliko taasisi za nje. Tunakubali kwa sababu hatuna mshikamano wa kutosha kuhoji au kudai mabadiliko. Nabaki kujiuliza tatizo ni Nani? Serikali, Benki, au Walimu Wenyewe? Ni rahisi kulaumu serikali au benki, lakini ukweli ni kwamba Kukosekana kwa umoja miongoni mwa walimu kunawapa nafasi wengine kututumia kwa maslahi yao, Vyama chetu cha walimu na taasisi yetu ya kifedha(Mwalimu commercial Bank) inaonekana kuendeshwa kwa utashi wa kisiasa au kibiashara, si kwa maslahi ya walimu(wakopaji) hivyo nasema Ukimya wetu ni kibali cha kuendelea kunyonywa.

📢 Nawasihi Walimu wenzangu Tuamke!,Walimu wenzangu, huu si wakati wa kulalamika tu. Ni wakati wa Kuhoji kwanini taasisi /Bank yetu inatutoza riba kubwa wakati Kila mwezi unachukua zaidi ya Bilioni Moja Toka kwenye mishahara yetu. Pia tudai uwazi wa matumizi ya michango yetu ikiwezekana uasi nchi nzima uanzishwe dhidi ya CWT.

Hitimisho,Walimu tuamke. Tujitambue. Tujipange. Tujitete.
Si walichangia kumchukulia fomu lakini?
 
Back
Top Bottom