digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,508
- 23,368
Walimu: Injini ya Maendeleo au Mashine Isiyotambua Thamani Yake?
Leo nimeketi na kutafakari kwa kina. Nimejiuliza swali gumu lakini la lazima:
Je, walimu ndiyo kundi la watumishi wajinga, wasio na mshikamano, wasiojua kesho yao?
Ni swali chungu, lakini si matusi—ni mwaliko wa kujitazama upya. Walimu tunategemewa kama injini ya maendeleo ya taifa. Tunafundisha madaktari, wanasheria, marais, na hata wachumi wanaotunga sera. Lakini kwa nini sisi wenyewe tunabaki nyuma, tukikubali kunyonywa bila kupaza sauti?
Hoja zangu zimejikita kwenye maswala ya Mikopo,Walimu Tunakatwa Zaidi, Tunakopeshwa Kwa Riba Kubwa nk,huku sisi wenyewe tuna benki yetu ambayo tulilaghaiwa kuwa itakuwa mkombozi kwetu.
Leo nimepitia mfumo wa ESS na kuchunguza taasisi zinazotoa mikopo kwa watumishi wa umma. Matokeo yamenishtua kabisa kwani SACCOS ya Uhamiaji Riba ya mkopo ni asilimia 12 kwa wanachama wao, Benki ya Azania: Inakopesha kwa asilimia 15.5 kama riba kwa mtumishi yeyote wa umma,wakati huo dude Mwalimu Commercial Bank,Benki yetu sisi walimu. Tunachangia zaidi ya TSh 20,000 kila mwezi kama ada ya ya uanachana lakini riba ya mkopo ni asilimia 17—sawa na benki za kibiashara kama NMB na CRDB!
Je, hii si dhuluma ya kiuchumi? Benki inayojengwa kwa jasho letu inatunyonya kuliko taasisi za nje. Tunakubali kwa sababu hatuna mshikamano wa kutosha kuhoji au kudai mabadiliko. Nabaki kujiuliza tatizo ni Nani? Serikali, Benki, au Walimu Wenyewe? Ni rahisi kulaumu serikali au benki, lakini ukweli ni kwamba Kukosekana kwa umoja miongoni mwa walimu kunawapa nafasi wengine kututumia kwa maslahi yao, Vyama chetu cha walimu na taasisi yetu ya kifedha(Mwalimu commercial Bank) inaonekana kuendeshwa kwa utashi wa kisiasa au kibiashara, si kwa maslahi ya walimu(wakopaji) hivyo nasema Ukimya wetu ni kibali cha kuendelea kunyonywa.
📢 Nawasihi Walimu wenzangu Tuamke!,Walimu wenzangu, huu si wakati wa kulalamika tu. Ni wakati wa Kuhoji kwanini taasisi /Bank yetu inatutoza riba kubwa wakati Kila mwezi unachukua zaidi ya Bilioni Moja Toka kwenye mishahara yetu. Pia tudai uwazi wa matumizi ya michango yetu ikiwezekana uasi nchi nzima uanzishwe dhidi ya CWT.
Hitimisho,Walimu tuamke. Tujitambue. Tujipange. Tujitete.