Je, wamachinga ni watu wavivu wasiopenda kazi?

Je, wamachinga ni watu wavivu wasiopenda kazi?

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Sijui kama ni tafsiri sahihi ili kuna wanaosema wamachinga maana yake ni wazururaji,watembea hovyo. Je, kuna ukweli kwenye hili?

Binafsi nafikiri kuna ukweli kwamba Wamchinga ni watu wavivu, ambao wanajificha mjini kufanya kazi ambazo hazina tija.Wamchinga wa zamani walikuwa wanabeba maduka yao begani ila hawa wasiku hizi wanajaa kwenye barabara za magari na njia za waenda kwa miguu.

Je, ni sahihi kusema kwamba sasa Wamachinga wanaozagaa kwenye maeneo ambayo sio maalum waondoshwe kwa sababu ya uvivu na uzembe na uchafuzi wa mazingira?

Pamoja na ni kwamba nina mtazamo wangu lakini napenda tujadili kwa kina.
 
Nitaingia kuijadili hoja hii baada ya miaka mitano au sita, nafikiri kipindi hicho utakuwa angalau umefikisha miaka ishirini na moja!
 
Imagine wamachinga wote wabebe bidhaa zao watembeze barabarani. Akili yako haina akili
 
Sio wavivu mkuu, wengi mtaji wao ni mdogo kwahyo umachinga unakuwa ndiyo kimbilio.

Ila baada ya muda mtaji ukikua wananza biashara kubwa iyo ya umachinga wanawaachia ndugu, jamaa na marafiki.

Kuliko mtu akae buree tu bila kujishughulisha ni bora akafanya umachinga hukohuko akili inafunguka, anapata kuona fursa nyingi, anapata kujuana na kuaminiwa na watu wengi.
 
Dah. Kivipi yaani?

Mtu anaehangaika na kupitia kazi yake hiyo mkono wa familia yake unaenda kinywani na watoto wanasoma mnasemaje anazurura na hana Kazi?

Kazi hiyo mnayotaka awe nayo ni ipi? Na Mume muwezeshaje awe nayo.

Tupunguzeni pumba na dharau.
 
Dah. Kivipi yaani?

Mtu anaehangaika na kupitia kazinyake hiyo mkono wa familia yake unaenda kinywani na watoto wanasoma mnasemaje anazurura na hana Kazi?

Kazi mnayotaka awe nayo ni koi? Na Mume muwezeshaje awe nayo.

Tupunguzeni pumba na dharau.
@kerucee
Shikamoo kipenzi
 
Nafikiri kukaa kwao mbele ya maduka ni hao wenye maduka ndio wanawapa bidhaa za kuuza.

Zamani walikuwa wanachukua bidhaa na kuzunguka na mzigo unapoisha anarudi kuchukua mwngine

Mwisho wakaona bora wakae hapo hapo na mzigo ukiisha inakuwa rahisi kuchukua dukani

Mwisho wa siku walipoona hawafukuzwi ndio wakaongezeka mpaka kufikia maelfu

Baadae wakapewa green light na Marehemu hapo ndio mpaka wa vijijini wakavamia majiji na kupata kibali cha 20

Najua huwa serikali haifanyi kitu ikawa historia ila watakurupuka kwa muda wa miezi kadhaa halafu watarudi tena

Huwa maamuzi ni magumu sana ila sijui kama wa Tz tunaweza
 
Imagine wamachinga wote wabebe bidhaa zao watembeze barabarani. Akili yako haina akili
Mkuu,Usipanick,Kwa sababu havibebeki ndo wapange hadi katikati ya lami?Tuwe wawazi katika hli bana
 
Mnakaa nyumbani kula nyumbani hamuyajui maisha its OK kuongea huo upumbavu...
 
Waondolewe barabarani bhana, tuache kutetea vitu vya ajabu. Wamegeuza miji kuwa magulio
 
Siku si Chinga tuu hata mama nitilie, wachoma chapati, wachoma mihogo n.k wote wamo brbrn
 
Mkuu,Usipanick,Kwa sababu havibebeki ndo wapange hadi katikati ya lami?Tuwe wawazi katika hli bana
Katikati ya lami sio sahihi nakubali. Lakini kusema ni wavivu wafanye kutembeza kama zamani unadhani itakuaje? Itakuwa kama maandamano ya nyumbu.
Barabarani ni sahihi kabisa wakitolewa.
 
Sijui kama ni tafsiri sahihi ili kuna wanaosema wamachinga maana yake ni wazururaji,watembea hovyo. Je, kuna ukweli kwenye hili?

Binafsi nafikiri kuna ukweli kwamba Wamchinga ni watu wavivu, ambao wanajificha mjini kufanya kazi ambazo hazina tija.Wamchinga wa zamani walikuwa wanabeba maduka yao begani ila hawa wasiku hizi wanajaa kwenye barabara za magari na njia za waenda kwa miguu.

Je, ni sahihi kusema kwamba sasa Wamachinga wanaozagaa kwenye maeneo ambayo sio maalum waondoshwe kwa sababu ya uvivu na uzembe na uchafuzi wa mazingira?

Pamoja na ni kwamba nina mtazamo wangu lakini napenda tujadili kwa kina.
Nini maana ya kufanya kazi?

Ova
 
Back
Top Bottom