RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
Je, ushawahi kupigwa tochi ambayo huielewi? Yaani umefuata vibao vyote vizuri kabisa lakini unafika mbele unaoneshwa picha kwenye 50kph zone imepita na 85kph au zaidi?
Twende pamoja. Kawaida ukifika eneo linalokutaka uende mwendokasi fulani kuna kibao(50kph mfano) na ukimaliza eneo hilo kipo kinachokuonesha kikomo 50kph kimeisha.
Mara nyingi Kama sio mara zote ukiona kibao cha kukuamuru uende 50kph upande wa pili wanaokuja wana kibao kinachowaruhusu waende zaidi ya 50kph.
Baada ya kuelewana kwenye hivi vibao twende kwenye mada. Wale jamaa zetu baada ya kuona tumekuwa watiifu wa 50kph na mapato yamepungua 'wameamua kutoa' vibao vinavyokuonesha isizidi 50kph au tuseme wezi wameviiba. Sasa wewe ukija hujui kuwa umeingia 50kph zone hivyo unaingia na speed zako kama zote. Ndio unapigwa tochi ambayo utabaki unajiuliza hiki kibao kiko wapi ambapo sijakiona?
Nimejuaje kama kibao kimetolewa/limetoka/hakipo? Ni hivi tochi hii utapigwa kwa mbele wakati unaingia hio zone na aliekupiga tochi atahakikisha kibao cha opposite direction kinachoruhusu 50kph kinaoneka! Yaani wewe unaenda upande ambao 50kph hairuhusiwi na ushahidi wake ni hiko cha opposite kinachoruhusu zaidi ya 50kph(kumbuka hivi vipo pamoja kulia na kushoto).
Huyu anaekupiga tochi anajua cha kukataza hakipo ndio maana kaja mbele ili akuoneshe cha kuruhusu mwenzio anaekuja opposite direction. Ukielewa ninalosema utaweza kujitetea ingawa utapotezewa muda sana.
Tufanyaje kuepuka hili? Hakikisha ukiona kibao upande wowote wa barabara unakisoma. Ukiona cha kuruhusu upande kinzani jua upande wako cha kuzuia wamekitoa vinginevyo utapigwa tochi na kubaki unajiuliza hii ni wapi!