Je, wanaharakati wa kisiasa barani Afrika wanapigania kwa dhati mabadiliko ya kidemokrasia au maslahi yao binafsi?

Je, wanaharakati wa kisiasa barani Afrika wanapigania kwa dhati mabadiliko ya kidemokrasia au maslahi yao binafsi?

Mimi naona kama demokrasia ni mkakati wa mataifa ya magharibi kusimika ajenda zao kwenye mataifa mbali mbali baada ya kuweka vibaraka wao.........ukitazama wanasiasa wanaoungwa mkono na mataifa ya magharibi wanabeba ajenda ambazo hata kwenye jamii za kiafrika ni kituko.......kama ndoa za jinsia moja!!!!
 
Mwafrika ni dhaifu mbele ya pesa. Tofauti na wenzetu wao Jamii kwanza sisi tumbo kwanza. Thus si ajabu kumkuta mtawala wa kiafrica anaomba pesa nchi iwe masikini anaficha ulaya eti anawekea kizazi chake utadhani nae aliwekewa utajiri na baba yake
 
Mkuu, does Africa has its own definition of democracy?
 
Mimi naona kama demokrasia ni mkakati wa mataifa ya magharibi kusimika ajenda zao kwenye mataifa mbali mbali baada ya kuweka vibaraka wao.........ukitazama wanasiasa wanaoungwa mkono na mataifa ya magharibi wanabeba ajenda ambazo hata kwenye jamii za kiafrika ni kituko.......kama ndoa za jinsia moja!!!!
Ndoa ya jinsia moja ni kitu ambacho sitakuja kukubaliana nacho mpaka siku ninaingia kaburini. Mark my words.
 
Do African Political Activists sincerely fight for Democratic Change or they simply keep alive a well-known old saying "It's Our Turn to Eat"?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu wa Tanzania;

Katika msimu wa joto wa mnamo mwaka 2009, aliyekuwa Rais wa Marekani bwana Barack Hussein Obama alisafiri kwenda nchini Ghana, kama kituo chake cha mwisho wa safari yake ya kwanza ya kimataifa kama Rais, na kutoa hotuba yake katika bunge la nchi hiyo katika jiji la Accra. Katika hotuba yake, alijadili uhusiano wa taifa lake na Afrika, na ushirikiano uliohitajika kuhakikisha mabadiliko katika bara zima.

View attachment 1539363

Alipokuwa jijini Accra, Rais alizungumzia juu ya mada (maudhui) nne ambazo alisema ni muhimu kwa mustakabali mwema wa bara hili la Afrika - demokrasia, fursa, afya, na utatuzi wa migogoro kwa njia za amani. Rais Obama alitoa hotuba yake ya kwanza ya sera za USA juu ya bara la Afrika akiwa katika taifa mwenyeji ambalo linanafasi ndogo sana kiuchumi au kisiasa kulinganisha na mataifa yenye nguvu zaidi kama Afrika Kusini na Misri.

View attachment 1539364Hata miongoni mwa watu wa Ghana, uchaguzi wa nchi sahihi kwa Obama umesababisha ukakasi Kwanini aende Ghana? Baadhi ya Wachambuzi wa msauala ya kisiasa walisema mpangilio wa mazignira wenyewe unasaidia kukiri mafanikio ya kisiasa na kidemokrasia ya Ghana. Inaonekana alichagua Ghana kwa alama yake ya kisiasa.

Alifanya ziara yake ya kwanza kwa nchi ambayo imekuwa na mabadiliko ya kidemokrasia ambayo kiongozi wa upinzani bwana John Atta Mills kutoka chama cha National Democratic Congress alishinda dhidi ya a Rais wa wakati huo ndugu John Kufuor wa chama cha New Patriotic Party. Huo ni ujumbe wenye nguvu sana kwa jamii zingine za Kiafrika, na kwa viongozi wengine wa Kiafrika.

View attachment 1539367

HAYA NI MANENO MACHACHE YA RAIS OBAMA ALIPOKUWA ANALIHUTUBIA BUNGE LA GHANA:

================

"Here in Ghana, you show us a face of Africa that is too often overlooked by a world that sees only tragedy or a need for charity. The people of Ghana have worked hard to put democracy on a firmer footing, with repeated peaceful transfers of power even in the wake of closely contested elections."

Ninaomba nisimuongelee ndugu John Atta Mills kwa maana yeye ni marehemu na kwa mila na desturi za kiafrika marehemu huwa hapaswi kusemwa vibaya.

Sasa juzi wakati ninasoma makala kadhaa hapa mtandaoni ndio nikakutana na hii scandal kubwa sana ya Airbus ya Rais John Mahama aliyechukua nafasi ya hayati John Atta Mills ambao wote walitokea chama kimoja cha kisiasa cha National Democratic Congress, ya wizi wa pesa kiasi cha £5million.

View attachment 1538177

Sasa kuanzia hapa nikajawa na maswali mengi sana kuliko majibu kwamba,

Do African Political Activists sincerely fight for Democratic Change or they simply keep alive a well-known old saying "It's Our Turn to Eat"?

NB
: Hii mada inalenga katika kuangazia mustakabali mzima wa demokrasia katika bara la Afrika, hivyo ninaomba tuepuke kabisa matusi, mabishano na malumbano ya CCM, CHADEMA, ACT-WAZALENDO, NCCR, CUF.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
CHADEMA ndio waliotaka kuingia na kuitafuna hii nchi
 
Back
Top Bottom