Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Sheria ya Makosa ya Adhabu namba 16 na Kanuni zake haimzuii mtu kumiliki wala kuvaa mavazi rasmi ya Jeshi ikiwa vazi hilo rasmi litavaliwa kwaajili ya matamasha au maigizo yanayowakilisha Jeshi lolote la Polisi kwa "Nia Njema"
Kifungu cha 178 kifungu kidogo 1, 2 na 3 cha Sheria hii pamoja na kanuni zake (Kanuni msambamba ya 178) vinazuia uvaaji wa mavazi rasmi ya Jeshi lolote la Polisi kwa mtu yoyote ambae hatumikii Jeshi lolote la Polisi bila ya ruhusa ya Rais.
Pia inazuia uvaaji wa sare hizo kwa njia inayodhalilisha Jeshi la Polisi. Zaidi ya hapo, Sheria hii inazuia mtu yoyote ambaye hayupo katika utumishi wa Jeshi kuingiza, kuuza au kumiliki kwaajili ya kuuza bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa Mkuu wa Polisi.
Sheria hii haizuii umiliki wala uvaaji wa mavazi hayo katika matamasha, kumbi za muziki au michezo kama sarakasi nk, au mahali popote pale michezo hiyo inaporuhusiwa kuchezwa hadharani katika kuliwakilisha Jeshi "Kwa Nia Njema".
Hii inamanisha kwamba mahali pekee ambapo Polisi wanaweza kwenda kuchukua sare hizo ni kwenye maduka au mahali popote zinapouzwa au kuhifadhiwa kwaajili ya kuuza na sio kwa watu binafsi au majumbani ambapo hazitundikwi/kuoneshwa au kuhifadhiwa kwaajili ya kuuzwa.