Je, Wananchi wanafahamu kuwa Wabunge wanapaswa kuwajibika kwa niaba yao badala ya vyama vyao?

Je, Wananchi wanafahamu kuwa Wabunge wanapaswa kuwajibika kwa niaba yao badala ya vyama vyao?

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Na je, wananchi wanafahamu kwamba wabunge wao wako bungeni kwa niaba yao na kwamba wakifanya kinyume wawawajibishe?

Katiba ya Tanzania, ibara 63 (2) iko wazi kwa jambo hili: “Sehemu ya pili ya Bunge (baada ya Rais) itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.”

Hivyo wabunge, kwa niaba ya wananchi wanaunda chombo chenye madaraka ya kuisimamia na kuishauri Serikali, kuisahihisha na kuhakikisha mipango yake inalenga kuwanufaisha wananchi wote.

Hadi sasa mtu kuwa mbunge ni lazima awe katika chama cha siasa. Mgombea binafsi hajakubalika, lakini chama cha siasa hakina uwakilishi bungeni. Chama kinakuwa ni chombo cha kumpitisha tu mbunge, apigiwe kura kuwakilisha wananchi.

Hivyo kuna haja ya elimu ya uraia kwa wabunge wetu na wananchi. Ni muhimu wabunge wakafahamu wajibu wao na wanajibika kwa nani, pia na wananchi wakafahamu nguvu zao juu ya wabunge wao.
 
Mbona tunawapa!, si wanatumia Kodi zetu!
 
Back
Top Bottom