Je, wapinzani hawapotoshi kuhusu vitambulisho vya ujasiliamali?

Hii serikali ya ajabu sana, me pia walifika kwenye moja ya ofisi yangu ndogo wakalazimisha nilipie kitambulisho wakati me nilikuwa nalipa kodi TRA.

Niligoma sababu nilijua kwa biashara ile sipaswi kuwa nacho ila walitaka kutumia nguvu nikaona sio kesi nikaongea na Mkurugenzi nikalipia elfu 20.

Baadaye mwaka huo huo akaja Meneja wa TRA na timu yake kudai kodi, me huwa sipo pale nikapewa taarifa nikamwambia asifunge ofisi yangu nilishalipia na nitampelekea uthibitisho ofisini.

Nilivofika nikaenda TRA na kitambulisho cha Mjasiriamali, jamaa akawaka kinoma me namcheki tu, nikamwambia ondoa jazba twende taratibu.

Nikamrukia hewani Mkurugenzi, baada ya malumbano akataka kunikana nikamwambia siku ile nilikurekodi na nitaenda na ushahidi hadi kwa Meko tuone we ni nani unayepinga agizo lake, akamwambia meneja muache huyo kijana wetu.

Na me kwa kuwakomoa hadi leo silipi TRA natereza na kitambulisho mwanzo mwisho baada ya kuona kodi zenyewe zinatumika kununua wapinzani na kurudia chaguzi za kijinga tu hamna la maana.
Jiwe anasema vitambulisho sio lazima ila mimi mwaka juzi alivyoanzisha niliona jamaa wanawalazimisha wafanyabiashara pale Mbagala Zakiem wakilazimishwa kuvilipia huku wamezungukwa na askari wenye SMG.
 
Tatizo kubwa la vitambulisho vya Magufuli ni kutokuwa na kanuni inayoeleweka. Hakuna anayefahamu fedha hizi zinakwenda wapi na kwa kazi gani. Tena zinatozwa hata kwa wasio wajasilia mali kwa mfano vibarua katika kazi za binafsi na umma, watumishi wa nyumbani, bar maids, wafanyakazi rasmi wa umma na binafsi nk.

Sasa hii ni kodi ya kichwa au ya mapato? Mbaya zaidi zinakusanywa na wanasiasa makada wa CCM.
 
Hizo hawakusanyi TRA, mnazipeleka wapi hizo pesa tena eti hamtoi risiti
 
Hizo hawakusanyi TRA mnazipeleka wapi hizo pesa tena eti hamtoi risiti

Wewe una kitambulisho?

Nia ya zoezi hili haikuwa mbaya kabisa ililenga kuwasaidia watu wenye kipato duni waweze kutafuta makate wao wa kila siku.

wewe tu peke yako ndiye unayeleta utata ila walengwa wanfurahia hivi vitambulisho.
 
Una maanisha nini unaposema pesa zinakwenda wapi?

Hauoni maendeleo ya miundo mbinu na maboresho ya huduma za kijamii?

Hii nchi ina wataalamu na watu wenye weledi katika kuweka mipango ya maendeleo, mbona Lissu anawachangisha wanachi hao hao maskini wakati walishalipa kodi zao na mkalipwa ruzuku.

Tuache ufitini.
 
Fikiria mchuuzi akiamka asubuhi anakuwa na mtaji wa kiasi gani. Kwa namna unavyowaza ni kuwa kila mtu hawezi kukosa 20,000/= ukweli ni kuwa wengi hiyo fedha wanaipata baada ya siku kadhaa.
 
Kwa taarifa yako hizo fedha anachukuwa Magufuli na huenda kiasi anaigawa kwa CCM.

Michango ya Lisu anaomba kwa hiari ya mtu na siyo lazima kama ma-dc wanavyolazimisha.
 
Kwa taarifa yako hizo fedha anachukuwa Magufuli na huenda kiasi anaigawa kwa CCM.

Thibitisha,

Ninachojua zinalipa pia ruzuku ambazo hata wapinzani wanapewa na kwa makusudi wanaamua kuwachangisha tena wananchi
 
Kenge hawasikii mpaka damu ziwatoke masikioni,chadema ninkuachana nao tuu nakuwaona malofa na mafala.
Wamesababisha mpaka Mwenyekiti wenu akate mauno kama Wema Sepetu pale Dodoma jana ili kuvutia watu
 
Hayo malipo ya vitambulisho ilikua inapelekwa wapi . na kwanini yalikua haitolewi risit. Malipo yoyote bila risit ni wizi tu. Ikuru ilirumiwa na mtu kukusanya the so called malipo ya vitambulisho bila risit ?
 
Rais wa wanyonge
 
Thibitisha,

Ninachojua zinalipa pia ruzuku ambazo hata wapinzani wanapewa na kwa makusudi wanaamua kuwachangisha tena wananchi
Thibitisha . maana mie najua zinaingia mfukoni kwa magufuli. Hapa ni kwamba hata ukusanywaji wa hizi malipo za vitambulisho ni utata mtupu. Maana si tra wanaokusanya
 
Wewe una kitambulisho?

Nia ya zoezi hili haikuwa mbaya kabisa ililenga kuwasaidia watu wenye kipato duni waweze kutafuta makate wao wa kila siku.

wewe tu peke yako ndiye unayeleta utata ila walengwa wanfurahia hivi vitambulisho.
Muuza supu wa mtaji wa 10,000 kitambulisho cha 20,000 chanini
 
Kwahiyo kwa sasa Ushuru hautozwi na Halmashauri mbalimbali nchini kwasababu ya elfu 20 za vitambulisho?
 
Kwenye masoko ushuru km kawa mfano sis wauza viat karume mchikichin ushuru wa halmashaur tunalipia mia tano pa dei ila wale wanaotembeza au kupanga barabaran ndio wanapaswa kuwa na hivyo vitambulisho.
 
Aliyekwambia ukiwa na Kitamburisho cha Ujasiliamari hulipi Ushuru sokoni ni nani?

Ushuru unalipa kama kawaida, kile walichoambiwa kama faida ya Kitamburisho ni kufanya biashara popote ukiwa na Kitamburisho.....

All in all WALILAZIMISHWA...!
 
Aliyekwambia ukiwa na Kitamburisho cha Ujasiliamari hulipi Ushuru sokoni ni nani?

Ushuru unalipa kama kawaida, kile walichoambiwa kama faida ya Kitamburisho ni kufanya biashara popote ukiwa na Kitamburisho.....

All in all WALILAZIMISHWA...!
Labda wao walilazimishwa lkn sisi tunauza viat deile na vitambulisho hatuna na hatukamatwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…