Mkuu hapa issue sio kulipa kiasi gani, hoja ni kuwa hicho ni kitambulisho hivyo kuna ubaya gani kikitolewa bure kwa mjasiriamali mdogo?
Mfano bodaboda kabla hakuwa analipia tozo yoyote, sasa hivi anatakiwa kulipa hiyo elfu 20 je naye umemuondolea mzigo au umemuongezea?
Hawa wajasiriamali wadogo ambao wanatafuta fedha ya kujikimu wanahitaji kusaidiwa na sio kukamuliwa hela kama Meko anavyofanya sasa.
Wanahitaji kuwekewa utaratibu mzuri ambao baadae utawawezesha kuwa walipaji wa kodi na watengeneze ajira kwa wengine sio kuwalipisha elfu 20 kisha kuwaacha wazurure hovyo na kuishia kuwa machinga maisha yao yote.
Mbali na hayo, hii fedha inayo kusanywa haijulikani ni kiasi gani kimepatikana na wala inaenda kufanya kazi gani.
Yote kwa yote, unaye jaribu kumtetea 'kashalegea' na kasema kulipia vitambulisho sio lazima kwa hiyo hata wasipolipa hakuna shida.
View attachment 1578005