Je, wapinzani hawapotoshi kuhusu vitambulisho vya ujasiliamali?

Kenge hawasikii mpaka damu ziwatoke masikioni,chadema ninkuachana nao tuu nakuwaona malofa na mafala.

Kiumbe kenge kwa mara ya kwanza kwenye bandiko lako linatoka kuelekezwa CDM.

Jiridhishe mara ngapi limetumika kuwamaanisha wale mboga mboga.

Hili copyright.

Ulikolileta si kwenyewe.
 
hiyo elfu 20,000 ni kodi au ushuru? unazijiua principles za government revenue & expenditure?, hiyo 20,000 inaenda kusapoti bajeti ipi, nani anafanya monitoring ya makusanyo na matumizi yake?, vile vitambulisho havina picha na havijawa linked na NIDA, kundi linalotozwa 20,000 tayari sheria ilitamka kuwa income yao ni exempt, sasa kama income yao ni exempt unapata wapi guts za kuitetea ili itozwe, makada muwe mnaenda shule kutafuta maarifa na sio kutafuta uteuzi
 


Mnaucheza mziki wa Mnyaturu huyu
 
Mimi ni miongoni wa wanaounga mkono hivi vitambulisho viwepo ili Machinga wabaki salama. Nakumbuka niliwahi kukuta Lori la Manispaa wanasomba bidhaa za Watu wakati ule niliumia sana.

Ingawa siungi mkono walivyokaa kiholela na kuharibu kabisa sura za miji...nilidhani Maofisa wa Mipango miji walioajiriwa na kulipwa na serikali wanapaswa kutafuta namna ya kuwapanga Watu hawa badala ya kila Mtu kukaa pembeni na kusema "tuwaache maana bwana Mkubwa kawaruhusu"
 
Iitwe kodi au ushuru lakini ni bora kuliko kuachwa hali iwe kama ilivyokuwa awali.

Haiwezekani wakaachwa wakae kati kati ya mji bila kulipa chochote...itakuwa ni vurugu badala ya biashara, ndio yale ya Mtu kubeba soksi mbili na kuzurura kwa kisingizio cha umachinga.
 
inabidi bunge litunge utaratibu maalum, 20,000 base yake ilikuwa nini? ililenga nini
 

..michango ni hiyari.

..pia ni kiwango kilicho ndani ya uwezo wako.

..Je, hivi vitambulisho aliyesema uwezo wake ni buku 2 alipewa?

..Au mmachinga aliyekuwa hana uwezo alisaidiwa kupewa hicho kitambulisho?
 

..wapeni ajira VIWANDANI.

..Jiwe aliahidi Tanzania ya viwanda.
 
Kwahiyo wewe unataka kutuambiaje?!
 
Ukienda sokoni kununua tenga la nyanya ujue limelipiwa ushuru. Ukienda kununua bidhaa dukani ujue ina vat. Pamoja na kitambulisho.
Watu walivichukia kwa sababu maafisa wa kata walilazimishwa kuviuza na wakuu wao. Yaana kulikuwa na utata. Utaratibu ungekuwa mzuri labda

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
..michango ni hiyari.

..pia ni kiwango kilicho ndani ya uwezo wako.

..Je, hivi vitambulisho aliyesema uwezo wake ni buku 2 alipewa?

..Au mmachinga aliyekuwa hana uwezo alisaidiwa kupewa hicho kitambulisho?
Serikali isiyokusanya Taxes and levies ni CORRUPT..
 
Utawala wa Lissu kila kitu kitakuwa bure! Vitambulisho vya machinga bure, bima ya afya bure, leseni za biashara bure, na hapatakuwepo na kodi ya aina yoyote!
Najua swali lako ni lile alilo uliza Dr Magufuli - kwamba hela ya kuendesha serikali itapatikanaje? Ni kwamba mali zetu (kama madini, misitu, fukwe etc) zitawekwa rehani kwa mataifa yalioendelea, na tupate hela tule bata.
Mambo ya hapa kazi tu ni ya utumwa! Lazima watu wawe na uhuru wachague wanayotaka! Hakutakuwa na Polisi maana kila mtu atafanya atakavyo.
Sasa kama CHADEMA/Lissu hawatafafanua vizuri, watu wengi wanafikiria itakuwa hivyo!
 
Kama unafatilia kampeni za Lissu anafafanua vema sana kila anapopita.

Anaposema UHURU anamaanisha watu wawe huru kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo bila kuonewa na serikali kama ilivyo sasa ambapo wakulima wanahangaika kutafuta mbegu na pembejeo wenyewe ila wakivuna serikali inawajazia ushuru wa mazao kila kona na inawalazimisha kuuzia mazao yao hapa nchini au kwa serikali kwa bei za hasara tena huku wakikopwa. Wafanya biashara wamekuwa wakibambikwa kodi zisizolipika na kusababisha wafunge biashara zao kwa kufilisika.

Anaposema HAKI anamaanisha watu wasitendewe unyama na wala unyanyasaji na serikali ama watendaji wake.

Watu wasibambikwe makesi ya uchochezi na uhujumu uchumi ili tu kuwafilisi mali zao kwa hila ama kuwanyamazisha wasiikosoe serikali. Watumishi wapande madaraja na mishahara kama inavyosema sheria ya kazi, sio kuwaburuza na kuwaonea kwa kigezo cha kufanya maendeleo.

Kutopeleka maendeleo baadhi ya maeneo ambayo yamechagua upinzani huku serikali ikikusanya kodi za watu hao. Kujiamulia matumizi ya fedha zetu bila idhini ya bunge kama vile kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato unao gharimu zaidi ya bilioni 39 kusipo na tija yoyote.

Anaposema MAENDELEO YA WATU anamaanisha, tutumie rasilimali/mapato/mikopo tunayopata kwa kuzingatia vipaumbele vyetu kama taifa.

Haya masuala ya kujenga madaraja/SGR/ Mabwawa na kununua Ndege wakati wananchi wanashindia mlo mmoja, ukienda hospitali hakuna madawa ya kutosha, wauguzi na Madaktari hawatoshi, hakuna vifaa tiba. Huduma duni za maji na mizigo ya kodi inayopandisha gharama za maisha kwa mwananchi.

Serikali haitoi ajira kwa kigezo cha kufanya miradi mikubwa ambayo hata hivyo haijafata taratibu za kisheria na wala haifanyiwi ukaguzi kujua kama ina tija kwa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…