Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu pia ni udhaifu wa vyama vya upinzani. Kwa nini bado wanaendelea kukubali mambo kama haya ya kuwanyima 'political space' yatokee.
Hili la kuzuiwa kufanya mikutano, pamoja na mengine ya mhimu yaliyomo katika katiba ndio yanayozidi kuwaminya wapinzani. Kazi yao ya kwanza ingekuwa kuyavalia njuga yooote yanayowabana, hata kabla ya kufikiria kwenda Ikulu. Hivi hivi wataendelea kusota tu siku zote.
Please, wapinzani, pitieni vipengele vyoote vinavyowanyima usawa katika kufanya shughuli zenu zifanikiwe. Hakikisheni vyote vinaondolewa haraka; ikiwezekana kabla ya uchaguzi ujao.
Suluhu yanukia mgogoro wa ardhi Kawe
Na Mwandishi Wetu
MWELEKEO wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi ya shule iliyoko Kawe, jijini Dar es Salaam, umeanza kuonekana, baada ya Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Halima Mdee, kufanikiwa kuwashawishi wakazi hao kukubali kukutana na wapinzani wao kujadili suala hilo.
Wakazi hao walifikia hatua hiyo siku moja baada ya Mbunge huyo ambaye amejitolea kuushughulikia mgogoro huo, kukamatwa na kushikiliwa na polisi wa kituo cha Kawe kwa saa kadhaa Jumatano wiki iliyopita baada ya kuzuka mapigano ya kurushiana mawe kati ya makundi mawili ya wananchi wanaogombea ardhi hiyo.
Kati ya makundi hayo, moja linadaiwa kutumiwa na kigogo mmoja katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni anayetuhumiwa kumega sehemu ya ardhi hiyo ambako kumejengwa Shule ya Msingi ya Kawe ?B? na Shule ya Sekondari ya Ukwamani na kuwa uzia baadhi ya wafanyabiashara kinyume cha sheria.
Habari kutoka katika eneo hilo zinaeleza kuwa wakazi hao walikubali kukutana na wapinzani wao kwenye kikao maalum kati yao na mbunge huyo, kilichofanyika katika eneo hilo, Ijumaa wiki iliyopita.
Alipoulizwa na mwandishi wa Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita, Mdee alithibitisha kuwa wakazi hao wamekubali kukutana na wapinzani wao.
"Kwa kweli mambo si mabaya. Tulikuwa na kikao cha pamoja jana (Ijumaa wiki iliyopita), tumekubaliana mambo kadhaa, ikiwamo kukutana na wavamizi na kuleta wapimaji, hivyo tunasubiri kuwasikiliza," alisema Mdee.
Mdee alisema wanatarajia kukutana na upande wa pili wa mgogoro Alhamisi wiki hii, huku wapimaji wakitarajiwa kufanya kazi hiyo leo.
Hata hivyo, wakati matumaini ya kupatiwa ufumbuzi mgogoro huo yakianza kuonekana, Mdee alisema jana kuwa anazo taarifa za kigogo huyo kuandaa baadhi ya vijana katika misikiti mbalimbali kwenda kufanya fujo katika kikao cha Alhamisi kwa madai kwamba mbunge huyo anatumiwa na viongozi Kikristo na Waislamu wasio na msimamo mkali kushughulikia mgogoro huo.
"Ni vitu vya ajabu kabisa. Hata hivyo, sitaacha kuwatetea wananchi wanyonge," alisema Mdee.
Tetesi nilizozipata ni kwamba huyu haziivi na Rita Mlaki, nikipata habari zaidi nitawaletea
PM
Utaziweka wapi wakati uko off. Umekalia umbea tu na sasa utaleta habari wapi? simamia hoja kwa hoja kabla sijakupeleka:
walewenyeumbeawanaoogopakusimamiaumbeawaoJF.co.nimezidiumbea
Ndio maana anajiita paparazi. Huyu ni spin doctor wa kutupwa!
Utaziweka wapi wakati uko off. Umekalia umbea tu na sasa utaleta habari wapi? simamia hoja kwa hoja kabla sijakupeleka:
walewenyeumbeawanaoogopakusimamiaumbeawaoJF.co.nimezidiumbea
maana vichwa vya habari vinavutia utadhani tabloids, maana zinasomeka "Waziri apigwa konzi".. halafu ndani ziko "mtoto khalfan Waziri amepigwa konzi na baba yake pale sokoni na kuangua kilio kikali"..
Sister karibu maana hivi vidonge tulivikosa sana; nikaogopa nikifikiri huenda mafuriko ya Kenya yamekukumba!
Naona umerudi kwa kasi na vidoti komAsante Kitila,
Nipo na nimejaa tele na nilisalimika mafuriko ya kenya! labda kitu nilichojifunza ni kutokaa siku moja zaidi ya niliyopanga kukaa Amsterdam next time nikipita ulaya.
Asante!
Kwa kweli tumetoka mbali. Ikumbukwe kuwa hii saratani ya kutumia vyombo vya dola kukandamiza wale wenye mtazamo tofauti na serikali ya CCM ilianza wakati wa Mwalimu (watu waliteswa na vyombo vya usalama kule karibu na makaburi ya Kinondoni au karibu na kanisa la St. Peters, Oysterbay). Hata kama alikuwa na nia njema, alichofanya kimegeuzwa na kuwa shina la uonevu ambao umepitwa na wakati.
Wapinzani wanahitaji heko kwani hata kama hatua zao ni ndogo katika kukataa huu uonevu, wanapiga hatua. Roma haikujengwa katika siku moja, na upinzani utaendelea kushamiri siku hata siku.
Kwa Mh. Rais na IGP Mwema, waelekezeni watendaji wenu (RPCs, OCDs etc) kuwa tumevulia nguo demokrasia (si upinzani), basi shurti tuoge maji ya ukweli unaoambatana na demokrasia hii, hata kama ukweli huu unaugusa serikali, huupendi au unauma! Hii ndio demokrasia ya kweli.
maana vichwa vya habari vinavutia utadhani tabloids, maana zinasomeka "Waziri apigwa konzi".. halafu ndani ziko "mtoto khalfan Waziri amepigwa konzi na baba yake pale sokoni na kuangua kilio kikali"..