Je, wapinzani ni wakombozi?

Papaaa Muwazi,

Huu wio wa wapinzani wanaochochea vurugu wakamatwe ni wa kwako au wa RPC Saibulu? Maana nimesoma habari na kujaribu kulinganisha na kichwa cha habari I just dont get it....
 
Huu pia ni udhaifu wa vyama vya upinzani. Kwa nini bado wanaendelea kukubali mambo kama haya ya kuwanyima 'political space' yatokee.

Hili la kuzuiwa kufanya mikutano, pamoja na mengine ya mhimu yaliyomo katika katiba ndio yanayozidi kuwaminya wapinzani. Kazi yao ya kwanza ingekuwa kuyavalia njuga yooote yanayowabana, hata kabla ya kufikiria kwenda Ikulu. Hivi hivi wataendelea kusota tu siku zote.

Please, wapinzani, pitieni vipengele vyoote vinavyowanyima usawa katika kufanya shughuli zenu zifanikiwe. Hakikisheni vyote vinaondolewa haraka; ikiwezekana kabla ya uchaguzi ujao.
 
..inasikitisha sana lakini mapambano yanaendelea,hawa wapinzani tusiwadharau maana ukiangalia vizuri na njaa zao na kuonewa onewa na serikali ndio waliotufungua macho na wizi mkubwa kabisa katika Historia ya Tanzania kuanzia BOT mpaka Buzwagi...kudos to Wapinzani ingawaje mazingira ya siasa ni magumu sana,hawa watu wanahitaji support kubwa sana maana hata issue tunazongelea sasa humu JF nyingi wameanzisha wao ingawaje mwanzoni tuliwaona kama wendawazimu
 
Hivi huyu angekuwa mbunge wa CCM anataka kuwapongeza wananchi kungekuwa na sokomoko? Polisi wangezuia maandamano?
 
Kalamu, wapinzani watabadilisha nini wakati ni wachache sana bungeni. Mimi na wewe tunashuhudia kila siku jinsi wanavyoburuzwa na spika na hoja zao kubezwa na wabunge wa ccm. Kitila Mkumbo amesema wazi hapa mara nyingi kuwa tatizo hapa ni kungoa mti ambao ni ccm haya mengine ni matawi tu ambayo hayana athari kubwa sana kwa ccm.

Wapinzani wamejaribu sana suala la kubadili katiba lakini ccm wamekataa katakata. Inaonekana ccm wanasubiri yatokee yale ya Kenya na Ivory Coast ndio wakubali kubadili katiba!
 
Tetesi nilizozipata ni kwamba huyu haziivi na Rita Mlaki, nikipata habari zaidi nitawaletea

PM
 
Tetesi nilizozipata ni kwamba huyu haziivi na Rita Mlaki, nikipata habari zaidi nitawaletea

PM

Utaziweka wapi wakati uko off. Umekalia umbea tu na sasa utaleta habari wapi? simamia hoja kwa hoja kabla sijakupeleka:

walewenyeumbeawanaoogopakusimamiaumbeawaoJF.co.nimezidiumbea
 
maana vichwa vya habari vinavutia utadhani tabloids, maana zinasomeka "Waziri apigwa konzi".. halafu ndani ziko "mtoto khalfan Waziri amepigwa konzi na baba yake pale sokoni na kuangua kilio kikali"..
 
Utaziweka wapi wakati uko off. Umekalia umbea tu na sasa utaleta habari wapi? simamia hoja kwa hoja kabla sijakupeleka:

walewenyeumbeawanaoogopakusimamiaumbeawaoJF.co.nimezidiumbea

Sister karibu maana hivi vidonge tulivikosa sana; nikaogopa nikifikiri huenda mafuriko ya Kenya yamekukumba!
 
Ndio maana anajiita paparazi. Huyu ni spin doctor wa kutupwa!
 
Utaziweka wapi wakati uko off. Umekalia umbea tu na sasa utaleta habari wapi? simamia hoja kwa hoja kabla sijakupeleka:

walewenyeumbeawanaoogopakusimamiaumbeawaoJF.co.nimezidiumbea

Heshima yako mkuu,
Duh,umenivunja mbavu apo! Anyaway,heri ya mwaka mpya.
 
maana vichwa vya habari vinavutia utadhani tabloids, maana zinasomeka "Waziri apigwa konzi".. halafu ndani ziko "mtoto khalfan Waziri amepigwa konzi na baba yake pale sokoni na kuangua kilio kikali"..

Kwi kwi kwi ,

yaani nimecheka sana hapa!

waziri kapigwa konzi kumbe anamwongelea khalifan waziri!
This guy is a joke na inabidi nimpeleke:

aliyewekaheadingyawazirikumbeanamwongeleamtotokhalifani.co.umbea
 
Sister karibu maana hivi vidonge tulivikosa sana; nikaogopa nikifikiri huenda mafuriko ya Kenya yamekukumba!

Asante Kitila,

Nipo na nimejaa tele na nilisalimika mafuriko ya kenya! labda kitu nilichojifunza ni kutokaa siku moja zaidi ya niliyopanga kukaa Amsterdam next time nikipita ulaya.

Asante!
 
Honestly sione habari inahusiana vipi na maelezo ya huyu mkuu. Ila inawezekana ana mambo yako. Nafikiri ameenda shule sasa je shule haijamsaidia? Maana ile issue ya kawe iko wazi sana hata RONDA alishindwa kuitolea maelezo ya kueleweka sasa wewe ambaye unaleta umbeya kuwa kuna beef kati ya Mdee na Mlaki hayo yako. nenda basi ukamtee mlaki. Haki lazima itendeke acha watu wanaojitolea muda wao kufanya kazi ambazo wengi tunashindwa wafanye.
 
Asante Kitila,

Nipo na nimejaa tele na nilisalimika mafuriko ya kenya! labda kitu nilichojifunza ni kutokaa siku moja zaidi ya niliyopanga kukaa Amsterdam next time nikipita ulaya.

Asante!
Naona umerudi kwa kasi na vidoti kom
 
Kwa kweli tumetoka mbali. Ikumbukwe kuwa hii saratani ya kutumia vyombo vya dola kukandamiza wale wenye mtazamo tofauti na serikali ya CCM ilianza wakati wa Mwalimu (watu waliteswa na vyombo vya usalama kule karibu na makaburi ya Kinondoni au karibu na kanisa la St. Peters, Oysterbay). Hata kama alikuwa na nia njema, alichofanya kimegeuzwa na kuwa shina la uonevu ambao umepitwa na wakati.

Wapinzani wanahitaji heko kwani hata kama hatua zao ni ndogo katika kukataa huu uonevu, wanapiga hatua. Roma haikujengwa katika siku moja, na upinzani utaendelea kushamiri siku hata siku.

Kwa Mh. Rais na IGP Mwema, waelekezeni watendaji wenu (RPCs, OCDs etc) kuwa tumevulia nguo demokrasia (si upinzani), basi shurti tuoge maji ya ukweli unaoambatana na demokrasia hii, hata kama ukweli huu unaugusa serikali, huupendi au unauma! Hii ndio demokrasia ya kweli.
 
Ni kweli kabisa lakini haijalishi kama kutesa kulianza awamu ya kwanza, wakati wa ukoloni, au wakati warumi wakitawala dunia nzima. Kinachojali sasa hivi ni walioko madarakani waache mambo ya upuuzi na kulinda raia badala ya kukandamiza raia.
 
maana vichwa vya habari vinavutia utadhani tabloids, maana zinasomeka "Waziri apigwa konzi".. halafu ndani ziko "mtoto khalfan Waziri amepigwa konzi na baba yake pale sokoni na kuangua kilio kikali"..

hahahah nimecheka mie...haya sasa kwa wale wanaopenda kununua gazeti kwa vichwa vya habari i cant immagine idadi ya matusi mnunuaji aliyoyamwaga!
 
Huyu Paparazi Muwazi ni kichaa mwingine na time waster kama Nabii kaingia hapa ? JF ina credibility sana sasa naona wanazuka watu wengi wa udaku na habari za ajabu .What is happening with JF ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…