Je, wapinzani ni wakombozi?

kwa nn vyama vya upinzani visianzishe miradi ya maana ya kusaidia vyama vyao?

nnakumbuka chama cha cuf kilianzisha shirika la kununua mazao ya wakulima vijijini ili kuwanyanyua wakulima na kupata mapato walifikia wapi?

au na wao wana mafisadi?


wanaweza kuanzisha mashule, maduka, mahoteli, makampuni na kadhaa wa kadhaa sasa tatizo ni lipi?

kwa nn wawe mbele kuwachangisha au kupitisha kapu kama wasemavyo kwa gharama za mikutano na safari za viongozi kwenda nje ila haya ya kujiinua kwa wanachama wao na vyama vyao wanashindwa?


au na wao mafisadi tu
 
Mkuu Waridi,

Nafikiri umeshindwa kuielewa dhana ya kwenda vijijini, si ajabu hata hao Wapinzani nao hawajaelewa maana kamili ya usemi huo. Haina maana kupeleka misafara ya vigogo na magari makubwa au helikopta kwenda kuhubiri mikutano na kufungua matawi, HAPANA, mkifanya hivyo hamtafanikiwa maana sio rahisi kupata resources za kuwafanya muendelee hivyo kwa muda mrefu.

Dhana za kwenda vijijini ambazo wengine tunaona zingesaidia ni kwa chama kuwa na wawakilishi wilayani ambao wanaelewa matatizo ya wananchi na wanashiriki kutatua. KUle vijijini kuna matatizo mengi sana kuanzia dhuluma mbalimbali mpaka kwenye namna ya kupata haki zao. Pia kuna matatizo ya kiuchumi, kuanzia uzalishaji bora mpaka namna ya kupata bei nzuri kwenye mazao yao.

Vyama vinatakiwa kuwa na wawakilishi wilayani ambao wataelewa haya matatizo na watashiriki kuyashughulikia kwa msaada kutoka makao makuu ya vyama vyao.

Nikupe mifano michache, kule tunakotoka wengine, tuliamua kushughulikia tatizo la wazazi ambao watoto wao wamekufa mijini lakini masuala ya mirathi walishindwa kuyamaliza kwasababu mbalimbali. Tuliamua hivyo baada ya kuona baadhi ya watu tunaowafahamu wana matatizo hayo, jambo la kushangaza ni kwamba baada ya muda mfupi kulikuwa na wazee zaidi ya 20 ambao walikuwa na matatizo kama hayo. Cases nyingi ni straight forward lakini kwa watu ambao hawajui hata waanzie wapi, zinageuka kuwa case ngumu sana. Cases nyingi tuliweza kusaidia kwa mimi nikiwa Ulaya kutumia simu na kushirikiana na kijana aliye wilayani kuwashauri namna ya kufanya, kuwakopesha pesa ndogo za kufanyia mambo yanayohitajika mwanzoni nk. Huo ni mfano mmoja mdogo tu. Kuna cases nyingine nyingi ambazo chama cha siasa kilicho makini kinaweza kusaidia.

Mkiwa na watu wilayani ambao ni wabunifu na wanaelewa mambo yanayotakiwa kulingana na ilani yenu wanaweza kufanya kazi nyingi za kuwasaidia wananchi kwa gharama ndogo sana. Kwa kufanya hivyo wananchi wataelewa na kujua chama gani kiko upande wao na baada ya muda kujenga imani kwamba sio lazima matatizo yao yatatuliwe na CCM.

Mnajua kuna akina mama na watoto wangapi wanakufa kwa kukosa dawa ambazo zipo? Serikali imetoa pesa na dawa lakini wajanja wilayani wanataka wapewe pesa kidogo, chama chochote kitakachoweza kusimamia matatizo kama haya, kina nafasi ya kupata baraka za wananchi.

Mwaka jana kulikuwa na mabilioni ya JK, je ni chama gani ambacho angalau kilijitahidi kuwaandaa vijana kwenye wilaya husika ili wafaidike na mpango huo? Pesa nyingi zikaishia kwa wajanja.

Hiyo ndio maana ya dhana ya kwenda vijijini, ni kwenda vijijini na kuwa wafumbuzi wa matatizo ya wananchi kwa kutumia resources na solutions zilipo huko huko wilayani.

Kusubiri mpaka uchaguzi ufike na watu ndio wanafunga safari kwenda huko vijijini ni kujisumbua bura. CCM wanakuwa wana miaka mitano ya kukaa na wananchi, upinzani wanataka kutumia wiki moja kuwatongoza hao wananchi?

Mambo ya ruzuku ndio adui namba moja wa upinzani. Ingeliwezekana wangepigania ili ruzuku yote ifutwe.

Kuna watu wanasema CCM wanatumia pesa za kuchota BOT ndio maana wanakubalika vijijini. Utashangaa mimi nikisema kuna wilaya nyingi tu ambazo wala hizo pesa hazikufika. Pesa za EPA nyingi ziliishia mikononi mwa wajanja, ndio maana wabunge wengi wa CCM wanakuja juu kwasababu waliumia kujidhamini kumbe wenzao walikuwa na mapesa ya kumwaga.

Ondoa equation ya pesa, bado mambo mengi yanaweza kufanyika.
 
Juzi nilikuwa Kijiji kimoja ndani kabisa!Kuna mwenyekiti wa kijiji alifiwa na mkewe katika mazishi hayo nilikuta mashati ya kijani tu!wametawala mazishi hayo!Ukienda kwenye shughuli za harusi huko vijijini unatuka shati za kijani tu!ukienda kwenye sughuli za maendeleo unakuta kijani tu!Ofisi za CCM huko vijijini imekuwa kama ofisi za kutoa huduma za kijamii!
Wapinzani wanaonekana kipindi cha uchaguzi tu!Eti hawana uwezo wa kwenda vijijini !hizo pesa za kukodi helikopta wanazitoa wapi?Ukieenda baadhi ya mikoa hao wapinzani hawana hata ofisi za vyama vyao tena Mkoa!Wapinzani wakitaka kujiimarisha hawan budi kujikita vijijini au lasivyo watakuwa kila mara wakilalamika kuibiwa kura
 
Just imagine umekwama barabarani siku tatu kutokana ubovu wa barabara, either kutokana na mvua kubwa au kwa kuwa daraja limekatika, una njaa na kiu, ghafla unaskia 'tuk,tuk,tuk,tuk', ukitizama angani unaona kijihelkopta cha Muheshimiwa hichooo kinapita, halafu baada ya siku chache unasikia kwamba vyama vya upinzani wanalia njaa na wanaomba msaada! Si matusi haya?
 
Kada Mpinzani; You Are Not Fair; Huu Ni Ushabiki Usio Kuwa Na Elimu; Hilli Neno Lako Ktk Signature Ni Upotoshaji; Ambaye Ameenda Shule Na Anaishi Tanzani Lazima Akeleke Na Ujinga Wa Kuandika Slogan Isiyo Na Mguu Ukaacha Watu Wa Mabilion Na Ukaandikia Waliokkopa; Anagalieni Eti-mbowe Unanuka Kama Mafisadi Wengine,watakupaka Rangi Lakini Unanuka.rudisha Mabilioni.ww Ni Fisadi Tokea Zamani,1990. I Trusted U,but Now I Dont !
 

Kana ka nsungu,
Ukwasi wa chama fulani kimoja,kiasi kwamba mheshimiwa wake anaruka juu na Helkopta si kiwakilishi halisi cha hali ya vyama vya siasa kifedha,tunavyo vyama 18.
 
CHADEMA wanarusha helikopta ndio,na hivyo vyama vingine takribani 15 je?
 
 
Kana ka nsungu,
Ukwasi wa chama fulani kimoja,kiasi kwamba mheshimiwa wake anaruka juu na Helkopta si kiwakilishi halisi cha hali ya vyama vya siasa kifedha,tunavyo vyama 18.

Kwa Tanzania Bara unapoongelea upinzani siku hizi- you are talking about CHADEMA na hawa watu ndio wanatakiwa wawe mfano kwa vyama vingine vidogo vya upinzani.
 
________________________________________
Ni ukweli uliowazi kabisa kuwa idadi ya wanojutia uamuzi wao wa kuipigia kura CCM katika chaguzi zilizopita hasa ule wa mwaka 2005 inaongezeka siku hadi siku.


Wanchi sasa wanazidi kupata mateso badala ya maisha bora waliyoahidiwa na viongozi wa CCM.
Mambo kama Ufisadi, Kulindana, Majigambo na nyodo za viongozi, Ahadi hewa, na 'uchafu' kibao ambao unaendelea kufanywa na viongozi wa serikali ya CCM ni miongoni mwa mambo yanayo wachefua Watanzania.

Ukibahatika kukaa kwenye vijiwe utawasikia hata wale ambao kipindi kile waliokuwa huwaelezi kitu mbele ya JK wakimlaani huyu mtu na CCM yake, bila shaka sasa kwa mbaali wanaanza 'kuipata picha'.

Imefikia mahali sasa watu wanajiuliza ' Hivi huyu jamaa kuna watu wanamwongoza au?' maana haiingii akilini kwa mfano 'Jitu' limefilisi nchi, raia wema wanakueleza eti unawajibu 'Mwacheni mzee apumzike' Huyu jamaa alipitia jeshi kweli??

Lakini mbali na yote hayo, Swali linalobaki vichwani mwa wengi ni kwamba, Je, 2010 Tukiamua kuwapitisha Wapinzani kwa kishindo watatuletea maendeleo na maisha bora ambayo serikali ya CCM ilishindwa?

Je, Hakutokuwa na mafisadi kama hawa tunaowaona leo?
Swali lingine ni je kuna mgombea yeyote kati ya hawa tunaowajua kutoka upinzani atakua 'strong' ambaye hatokubali kumlinda mtu kama afanyavyo JK?

Pengine watu wangependa kujua zaidi iwapo kama Hivi 'vijisenti' vya ruzuku tu tayari watu wa Makao makuu wanajipendelea na kusahau wa mikoani, je Wakipewa Wizara si patakua hapakaliki?

Ingawa katika kambi ya upinzani kuna 'hazina' ya uchumi ambaye si mwingine bali ni Profesa Ibrahim Lipumba lakini bado lazima tujiulize je, maamuzi yake mara baada ya kufika Ikulu hayatakua ya kibabe kama maprofesa wengine wa hapa nchini na Duniani kwa ujumla? inasemekana kuwa hakuna rais Profesa katika nchi zote duniani.

Mfano rahisi ni Maprofesa ambao ni wakuu wa vyuo na taasisi mbali mbali hapa nchini achilia mbali Prof. Mwandosya ambaye analazimisha raia wa kigeni kuchangie maendeleo ya jimbo lake vinginevyo anatengenezea 'skendo' ili watimuliwe nchini.

Hawa jamaa(Maprofesa) huwa wanajiona hawakosei kwa sababu Elimu yao ni kubwa kuliko elimu zote. Kuna rafiki yangu hivi karibuni alimtaja Dr. Slaa kuwa anafaa. Ningenda kumwahidi yeye na wengine wote kuwa hivi karibuni kwa kupitia humu humu JF nitaweka hazarani 'Ukibaraka' wa Dr.Slaa.

Pia yupo huyu Freeman Mbowe ambaye bila kificho huyu jamaa ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa nchini, Je ataweza kujizuia kufanya biashara akiwa Ikulu?

Hata hivyo simaanishi kuwa
Tusiwape Wapinzani Kura bali pia sio mbaya tukajiuliza maswali ambayo ni muhimu kupata majibu yake kabla ya kufanya maamuzi mazito.


Mwisho ningependa kuwasalimu jamaa zangu wa PPT-MAENDELEO, TADEA, DP, JAHAZI na wengine ambao tunawasikia kipindi cha uchaguzi mkuu tu. Amkeni Jamani wakati ndo huu CCM wameshindwa kazi, I LOVE TAZANIA, I HATE MAFISADI.
 
Ndiyo kwasababu tatizo la sasahivi ni rushwa na siyo planning. Hivyo mtu yeyote atakaye pambana na rushwa ataleta maendeleo.
 
Ndibalema unajua Tanzania maisha mazuri hayawez kuja na haitatokea kuja kupia Chama chenye uhakika asilimia mia kuwa lazima kishinde.

Chama cha mapinduzi bila kuona kama kuna hatari ya kupoteza ktk chaguzi hakitakaa kiletee wananchi maendeleo. watakuwa kazi ni kugawana raslimali za nchi wakati wananchi wakiendea kupata mateso kila siku. Unaweza kuona pale karibia na Ofisi ya mtu kama Chenge kuna vijiwe, ukikaa ukajua watu walioko pale unaweza kukuta wakati mwingine hawana hata nauli ya kurudi majumbani. Lakini statement za vinara wa CCM unasikia zinavyosema.

Hawa CCM utafikiri wanawatawala waingereza au wamarekani siyo watanzania. Kwanza wanamapesa hata zaidi ya viongozi wanaotupa misaada.

Hili maendeleo yaje tanzania ni lazima kusiwe na mtu mwenye uhakika wa kumtawala mwingine.

Kinachotakiwa tanzania, kwanza maendeleo hayawezi kuja bila kuheshimiana. Lazima mwenye nacho awe na heshima na asiyekuwa nacho aheshimu aliyenacho.

Hili tuheshimiane tunahitaji process. Kenya wataendelea muda si mrefu kwa sababu wanaelekea katika kuheshimiana.
 
Tanzania ingekuwa pazuri kama tusingekuwa na vyama. Watanzania wengi hawana vyama na hii ingesaidia sana nchi kwamfano sasa hivi raisi inabidi achague mawaziri kutoka CCM na ni lazima wawe wabunge.Mawaziri wengi wanawajibika kwasababu ya rushwa na wanaobakia inawezekani hawana ujuzi au vipaji vya kuwa viongozi. Watanzania wengi ambao si wanasiasa na ni wasomi hawawezi kupata nafasi ya kusaidia kwasababu ya muundo mbaya wasomi wa nje hawawezi kuchaguliwa mawaziri mpaka wawe wanasiasa. TGanzania ingefaidika kama tusingekuwa na vyama na lengo lingekuwa kuboresha nchi na si kunufaisha chama. Vilevile kizazi kipya watu tuliozaliwa mijini hatujulikani vijijini kwetu na ni vigumu kupata ubunge kwani muda mwingi tumetumia kusoma na wengingine kusoma nje. Je sisi tuliozaliwa mijini tutasaidiaje baadae kama wabunge wanatoka vijijini?? na ndiyo ninaona wabunge na serikali ni lazima viwe vitu viwili tofauti na badala ya mawaziri tuwe na makatibu tu na itakuwa raisi kuwafukuza kazi na kuwachukulia hatua.
 

Ndugu yangu KAKINDOMASTER nimekuelewa na umeni'tachi hasa ulipozungumzia swala la planing. pia nchi hii hatutoheshimiana hadi siku wananchi waamue ku.......... Nimekusoma mkuu.
 
Nadhani umekuja na mengi sana ambayo ni hoja ndani ya hoja.

a. Je kuku aliyeko bandani ni mtamu kuliko aliyeko mezani? Je anaweza kunoga akiwa bado bandani? Tutawezaje kujua utamu wake...

b. Umechomekea vijembe vingi hilo la Prof. Mwandosya hebu tuwekee angalau chembe ya ushahidi wa mazingira manake peke yake linatosha kuwa hoja.

c. Kwanini unataka watu "wawaletee maendeleo". Nani anaweza kumletea mtu mwingine maendeleo. Kama wana "Musa na Manabii" na hawajawasikiliza unafikiri akitoka mtu toka kwa wafu watamsikiliza?
 
Kuna rafiki yangu hivi karibuni alimtaja Dr. Slaa kuwa anafaa. Ningenda kumwahidi yeye na wengine wote kuwa hivi karibuni kwa kupitia humu humu JF nitaweka hazarani 'Ukibaraka' wa Dr.Slaa.

Mkuu Ndibalema,

Heshima yako kaka, unajua heshima ni kitu cha bure, sasa wewe ukianza kujiheshimu na wengine humu tutakuheshimu,

Sasa with all due respect, kabla hujatupa ukibaraka wa Shujaa wa Taifa Dr. Slaa, labda kwanza ungetupa ushaidi wa kuwasafisha mafisadi aliotawataja,

Na pia si unajua kuwa kati ya aliowataja kuna waliosema kuwa wataenda mahakamani kumshitaki, Shujaa Dr. Slaa sasa vipi ukitueleza yaliyowasibu mpaka leo hawajenda huko kwenye sheria?

Mnajua huko upinzani mnahitaji kuelewana on priorities na ishu muhimu za taifa kwa muda huu, maana kwa mwendo huu wa kauli moja nzito huko inasema Mkapa ni fisadi na ushahidi juu, halafu kauli nyingine tena nzito huko inasema Mkapa ni safi sana you sure have a problem huko upinzani, tena a big one ila tu msituchangaye sisi wananchi ambao tuna our goals straight!

Halafu please, kila unapoingia hapa JF kumbuka kuwa unakuja kwa watu wazima wenye akili timamu!
 
Ndibalema "karibu" sana JF!

Hapa watu wanamkoma nyani giledi mchana kweupeeee bila udaku wana majungu!
 

Mazee Geeque,

Salute & Respect! Lovely!
 
________________________________________
Ni ukweli uliowazi kabisa kuwa idadi ya wanojutia uamuzi wao wa kuipigia kura CCM katika chaguzi zilizopita hasa ule wa mwaka 2005 inaongezeka siku hadi siku.

Huu ukweli uko wazi kwa nani, kwa vigezo vipi, na wewe umejuaje?


Wanchi sasa wanazidi kupata mateso badala ya maisha bora waliyoahidiwa na viongozi wa CCM.

Very bold! haya toa mifano ya mateso hayo ambayo "sasa" ndiyo yameanza kuonekana.

Mambo kama Ufisadi, Kulindana, Majigambo na nyodo za viongozi, Ahadi hewa, na 'uchafu' kibao ambao unaendelea kufanywa na viongozi wa serikali ya CCM ni miongoni mwa mambo yanayo wachefua Watanzania.

Sijui kama haya yameanza "sasa"... Na sijui kama yanaweza kumfanya mtu yeyote ayafurahie hata kama si Mtanzania.

Ukibahatika kukaa kwenye vijiwe utawasikia hata wale ambao kipindi kile waliokuwa huwaelezi kitu mbele ya JK wakimlaani huyu mtu na CCM yake, bila shaka sasa kwa mbaali wanaanza 'kuipata picha'.

Sasa hii bahati ya mtu mwingine na sisi tuilalie mlango wazi; mambo ya bahati hayatabiriki. Ndugu yangu Pundit anaweza kukueleza kwa kirefu suala hili na kwanini huwezi kukaa na kusubiria bahati.

Imefikia mahali sasa watu wanajiuliza ' Hivi huyu jamaa kuna watu wanamwongoza au?' maana haiingii akilini kwa mfano 'Jitu' limefilisi nchi, raia wema wanakueleza eti unawajibu 'Mwacheni mzee apumzike' Huyu jamaa alipitia jeshi kweli??

Huwezi kuendesha nchi kwa maneno ya Raia wema tu, vingenevyo nchi itatawaliwa kwa umbeya, tetesi, na hisia.

Lakini mbali na yote hayo, Swali linalobaki vichwani mwa wengi ni kwamba,

Inawezekana ni wachache wenye swali hilo? Umejuaje kuwa ni wengi?

Je, 2010 Tukiamua kuwapitisha Wapinzani kwa kishindo watatuletea maendeleo na maisha bora ambayo serikali ya CCM ilishindwa?

Kama ni swali hili sijui kama ni wengi wanafikiria; katika vitu muhimu katika maisha ya watu sidhani kama watu "wengi" wanafikiria uchaguzi wa 2010. Hapa tunahitaji angalau msingi wa kauli yako hii ili tuweze kujua assumption yako ni sahihi au la.


Je, Hakutokuwa na mafisadi kama hawa tunaowaona leo?
Swali lingine ni je kuna mgombea yeyote kati ya hawa tunaowajua kutoka upinzani atakua 'strong' ambaye hatokubali kumlinda mtu kama afanyavyo JK?

Swali langu kuhusu kuku linakuja hapa.


Pengine watu wangependa kujua zaidi iwapo kama Hivi 'vijisenti' vya ruzuku tu tayari watu wa Makao makuu wanajipendelea na kusahau wa mikoani, je Wakipewa Wizara si patakua hapakaliki?

Hawa watu wa makao makuu ya wapi? Maana umezungumza kama wote tuko kwenye ukurasa mmoja.

Ingawa katika kambi ya upinzani kuna 'hazina' ya uchumi ambaye si mwingine bali ni Profesa Ibrahim Lipumba

Yaani huyu ndiye "hazina" ya uchumi? au ulitaka kumaanisha "msomi wa uchumi"... ?

lakini bado lazima tujiulize je, maamuzi yake mara baada ya kufika Ikulu hayatakua ya kibabe kama maprofesa wengine wa hapa nchini na Duniani kwa ujumla? inasemekana kuwa hakuna rais Profesa katika nchi zote duniani.

Sijui kwanini lakini Plato alitoa maoni kama haya zaidi ya miaka 2000 iliyopita.


Mfano rahisi ni Maprofesa ambao ni wakuu wa vyuo na taasisi mbali mbali hapa nchini achilia mbali

huu mfano sijauelewa

Prof. Mwandosya ambaye analazimisha raia wa kigeni kuchangie maendeleo ya jimbo lake vinginevyo anatengenezea 'skendo' ili watimuliwe nchini.

Toa mifano na mwaga data, ni jinsi gani Mwandosya amekuwa akilazimisha raia wa kigeni wachangie maendeleo na jinsi gani ametengeneza skendo ili watimuliwe nchini?


Hawa jamaa(Maprofesa) huwa wanajiona hawakosei kwa sababu Elimu yao ni kubwa kuliko elimu zote.

Nadhani huwatendei haki kwa kauli ya jumla kama hiyo unless una takwimu angalau za kiswahili kuonesha msingi wa hukumu yako hii.


Kuna rafiki yangu hivi karibuni alimtaja Dr. Slaa kuwa anafaa. Ningenda kumwahidi yeye na wengine wote kuwa hivi karibuni kwa kupitia humu humu JF nitaweka hazarani 'Ukibaraka' wa Dr.Slaa.

Well, tunasubiri kwa hamu ulete huo "ukibaraka" 'hazarani'


Pia yupo huyu Freeman Mbowe ambaye bila kificho huyu jamaa ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa nchini, Je ataweza kujizuia kufanya biashara akiwa Ikulu?

Kwani lazima uwe mfanya biashara kabla ya kuingia ili uweze kufanya biashara ukiwa Ikulu?
Hata hivyo simaanishi kuwa

Tusiwape Wapinzani Kura bali pia sio mbaya tukajiuliza maswali ambayo ni muhimu kupata majibu yake kabla ya kufanya maamuzi mazito.

Angalau hii ni kauli ya mtu anayefikiri, lakini inaonekana tayari umeshafikia mahitimisho katika mambo kadhaa na umeshapata majibu yake (ambayo umetupatia) sasa kwanini sisi wengine tujiulize tena?



Mwisho ningependa kuwasalimu jamaa zangu wa PPT-MAENDELEO, TADEA, DP, JAHAZI na wengine ambao tunawasikia kipindi cha uchaguzi mkuu tu. Amkeni Jamani wakati ndo huu CCM wameshindwa kazi, I LOVE TAZANIA, I HATE MAFISADI.

sawa mkuu
 
Waungwana,
Nafikiri ni vema tukaangalia sifa nzuri na mbaya za kila upande, yaani wapinzani upande mmoja na CCM upande wa pili. Halafu kwenye upinzani ni vema tukawa specific tunapoongelea chama husika. Yaani mtu ataje kabisa chama anachoongelea kama ni CUF, CHADEMA, TLP, NCCR, muungano wao n.k., au mfumo gani wa wapinzani ambao anapendekeza.

Hili ni muhimu maana kila chama kina mazuri na mabaya yake. Tuanzie hapa then tuendelee bila kukandia chama chochote, including CCM, maana hii ni topic muhimu sana.




_________________
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…