________________________________________
Ni ukweli uliowazi kabisa kuwa idadi ya wanojutia uamuzi wao wa kuipigia kura CCM katika chaguzi zilizopita hasa ule wa mwaka 2005 inaongezeka siku hadi siku.
Huu ukweli uko wazi kwa nani, kwa vigezo vipi, na wewe umejuaje?
Wanchi sasa wanazidi kupata mateso badala ya maisha bora waliyoahidiwa na viongozi wa CCM.
Very bold! haya toa mifano ya mateso hayo ambayo "sasa" ndiyo yameanza kuonekana.
Mambo kama Ufisadi, Kulindana, Majigambo na nyodo za viongozi, Ahadi hewa, na 'uchafu' kibao ambao unaendelea kufanywa na viongozi wa serikali ya CCM ni miongoni mwa mambo yanayo wachefua Watanzania.
Sijui kama haya yameanza "sasa"... Na sijui kama yanaweza kumfanya mtu yeyote ayafurahie hata kama si Mtanzania.
Ukibahatika kukaa kwenye vijiwe utawasikia hata wale ambao kipindi kile waliokuwa huwaelezi kitu mbele ya JK wakimlaani huyu mtu na CCM yake, bila shaka sasa kwa mbaali wanaanza 'kuipata picha'.
Sasa hii bahati ya mtu mwingine na sisi tuilalie mlango wazi; mambo ya bahati hayatabiriki. Ndugu yangu Pundit anaweza kukueleza kwa kirefu suala hili na kwanini huwezi kukaa na kusubiria bahati.
Imefikia mahali sasa watu wanajiuliza ' Hivi huyu jamaa kuna watu wanamwongoza au?' maana haiingii akilini kwa mfano 'Jitu' limefilisi nchi, raia wema wanakueleza eti unawajibu 'Mwacheni mzee apumzike' Huyu jamaa alipitia jeshi kweli??
Huwezi kuendesha nchi kwa maneno ya Raia wema tu, vingenevyo nchi itatawaliwa kwa umbeya, tetesi, na hisia.
Lakini mbali na yote hayo, Swali linalobaki vichwani mwa wengi ni kwamba,
Inawezekana ni wachache wenye swali hilo? Umejuaje kuwa ni wengi?
Je, 2010 Tukiamua kuwapitisha Wapinzani kwa kishindo watatuletea maendeleo na maisha bora ambayo serikali ya CCM ilishindwa?
Kama ni swali hili sijui kama ni wengi wanafikiria; katika vitu muhimu katika maisha ya watu sidhani kama watu "wengi" wanafikiria uchaguzi wa 2010. Hapa tunahitaji angalau msingi wa kauli yako hii ili tuweze kujua assumption yako ni sahihi au la.
Je, Hakutokuwa na mafisadi kama hawa tunaowaona leo?
Swali lingine ni je kuna mgombea yeyote kati ya hawa tunaowajua kutoka upinzani atakua 'strong' ambaye hatokubali kumlinda mtu kama afanyavyo JK?
Swali langu kuhusu kuku linakuja hapa.
Pengine watu wangependa kujua zaidi iwapo kama Hivi 'vijisenti' vya ruzuku tu tayari watu wa Makao makuu wanajipendelea na kusahau wa mikoani, je Wakipewa Wizara si patakua hapakaliki?
Hawa watu wa makao makuu ya wapi? Maana umezungumza kama wote tuko kwenye ukurasa mmoja.
Ingawa katika kambi ya upinzani kuna 'hazina' ya uchumi ambaye si mwingine bali ni Profesa Ibrahim Lipumba
Yaani huyu ndiye "hazina" ya uchumi? au ulitaka kumaanisha "msomi wa uchumi"... ?
lakini bado lazima tujiulize je, maamuzi yake mara baada ya kufika Ikulu hayatakua ya kibabe kama maprofesa wengine wa hapa nchini na Duniani kwa ujumla? inasemekana kuwa hakuna rais Profesa katika nchi zote duniani.
Sijui kwanini lakini Plato alitoa maoni kama haya zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Mfano rahisi ni Maprofesa ambao ni wakuu wa vyuo na taasisi mbali mbali hapa nchini achilia mbali
huu mfano sijauelewa
Prof. Mwandosya ambaye analazimisha raia wa kigeni kuchangie maendeleo ya jimbo lake vinginevyo anatengenezea 'skendo' ili watimuliwe nchini.
Toa mifano na mwaga data, ni jinsi gani Mwandosya amekuwa akilazimisha raia wa kigeni wachangie maendeleo na jinsi gani ametengeneza skendo ili watimuliwe nchini?
Hawa jamaa(Maprofesa) huwa wanajiona hawakosei kwa sababu Elimu yao ni kubwa kuliko elimu zote.
Nadhani huwatendei haki kwa kauli ya jumla kama hiyo unless una takwimu angalau za kiswahili kuonesha msingi wa hukumu yako hii.
Kuna rafiki yangu hivi karibuni alimtaja Dr. Slaa kuwa anafaa. Ningenda kumwahidi yeye na wengine wote kuwa hivi karibuni kwa kupitia humu humu JF nitaweka hazarani 'Ukibaraka' wa Dr.Slaa.
Well, tunasubiri kwa hamu ulete huo "ukibaraka" 'hazarani'
Pia yupo huyu Freeman Mbowe ambaye bila kificho huyu jamaa ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa nchini, Je ataweza kujizuia kufanya biashara akiwa Ikulu?
Kwani lazima uwe mfanya biashara kabla ya kuingia ili uweze kufanya biashara ukiwa Ikulu?
Hata hivyo simaanishi kuwa
Tusiwape Wapinzani Kura bali pia sio mbaya tukajiuliza maswali ambayo ni muhimu kupata majibu yake kabla ya kufanya maamuzi mazito.
Angalau hii ni kauli ya mtu anayefikiri, lakini inaonekana tayari umeshafikia mahitimisho katika mambo kadhaa na umeshapata majibu yake (ambayo umetupatia) sasa kwanini sisi wengine tujiulize tena?
Mwisho ningependa kuwasalimu jamaa zangu wa PPT-MAENDELEO, TADEA, DP, JAHAZI na wengine ambao tunawasikia kipindi cha uchaguzi mkuu tu. Amkeni Jamani wakati ndo huu CCM wameshindwa kazi, I LOVE TAZANIA, I HATE MAFISADI.
sawa mkuu