Je, wapinzani ni wakombozi?

Je, wapinzani ni wakombozi?

Nilijua hiyo itasababisha controversy,

actually binadamu ni worse than Punda, angalau Punda anaweza kusema ung'amuzi wake wa mambo ni mdogo.Binadamu hata baada ya ung'amuzi mkubwa wa mambo bado anakuwa fisadi by nature.Ndiyo maana ukomunisti umeshindwa Urusi, wakati wengine wakipanga foleni kupata mikate ya rationing, wakuu wa chama cha kikomunisti walikuwa wanajivinjari katika ma Dacha yaliyo kwenye posh suburbs za Muskva.Na hata maduka yao yalikuwa tofauti kwani walikuwa na Supermarket zao zina kila kitu kutoka west.

Lord Acton alisema power corrupt, absolute power corrupts absolutely.Binadamu is worse than Punda na hawezi kutegemewa ku act responsibly bila ya kuwekewa sheria, at least as far as the context of government is concerned ambako all sorts of weird groupthink and mob psychology zinatokea na kuwafanya hata watu rational waanze kufanya mambo ya ajabu within a group.

Hujasema lolote kuhusu usawa wa binadamu na punda inapokuja kwenye kujifanya mambo kwa hiari bila koboko. Aya ya kwanza umeongelea Ufisadi wa ma apparatchiks wa Russia. Aya ya pili umeleta msemo wa mja mmoja wa Kiiingereza ambao hausemi lolote kuhusu kufanana kwa asili ya binadamu na Punda. Pointi ya mwisho kuhusu group thinking na mob psychology inasaidia kuudhoofia hoja yako kwamba Binadamu ni kama Punda kwa sababu umekubali kuna wakati binadamu anakuwa rational isipokuwa kwenye vikundi - ambavyo anajiunga kwa hiari. Lakini hakuna punda ambae ana rationale ya kwenda bila kiboko! Bado hujanishawishi kwamba asili ya Binadamu ni kama asili ya Punda!
 
CCM walioongoza muda huu wote utakuta wanaongelea kuhusu kufufua uchumi at the same time wanasema watanzania hawajitumi kufanya kazi.Leo hii Kenya inatuburuza kiuchumi huku kwetu tumekumbatia chama bovu.

Leo hii CCM hawataki kusikia kiu kama elimu ya uraia maanake hiyo ndiyo itakua kiama kwao.


So,inabidi walazimishwe kwa nguvu kukubaliana na suala la katiba.Hivi jamani opposition tukaunganisha nguvu hata kama ni nje ya bunge kumobilize watu kuingia mtaani kushinikiza mabadiliko hasa kwenye katiba.je haitawezekana?maanake bungeni CCM wanaabuse the legislative system
 
Hujasema lolote kuhusu usawa wa binadamu na punda inapokuja kwenye kujifanya mambo kwa hiari bila koboko.!

actually binadamu ni worse than Punda, angalau Punda anaweza kusema ung'amuzi wake wa mambo ni mdogo.Binadamu hata baada ya ung'amuzi mkubwa wa mambo bado anakuwa fisadi by nature!

Sijasema lolote? What more do you want me to say?


Aya ya kwanza umeongelea Ufisadi wa ma apparatchiks wa Russia.

Selective omission

Aya ya pili umeleta msemo wa mja mmoja wa Kiiingereza ambao hausemi lolote kuhusu kufanana kwa asili ya binadamu na Punda.

Somo ni relevant sana katika ku address the bigger isue, having addresed the punda issue above,not to be distracted by this Kuhani Mkuu fela whose ilk is responsible for Africa's backwardness ever since the glorious days of the Pharaohs of ancient Egypt, I built onwards and sommersaulted back to the main issue like Big Daddy Kane on the track.

Pointi ya mwisho kuhusu group thinking na mob psychology inasaidia kuudhoofia hoja yako kwamba Binadamu ni kama Punda kwa sababu umekubali kuna wakati binadamu anakuwa rational isipokuwa kwenye vikundi - ambavyo anajiunga kwa hiari.

You fail or select to notice the persuasive argument that, if person A does not know how to read and is ignorant, and person B knows how to read but is equally ignorant, in the mathematical equations of cross multiplication person B will come better off due to the allowance of the impediment arising from lack of access to information, not sheer resourcefulness.Instead you focus on distractions based on non absolutes such as "kuna wakati" what about the other "nyakati"? ![/QUOTE]

Lakini hakuna punda ambae ana rationale ya kwenda bila kiboko! Bado hujanishawishi kwamba asili ya Binadamu ni kama asili ya Punda!

Hujaelewa hata ninachozungumzia.Asili ya binadamu sio kama asili ya Punda, asili ya binadamu ni mbaya zaidi ya asili ya Punda.Simjui hata Punda mmoja aliye amass chakula cha wizi worth USD 25 M huku wenzake wanakufa na njaa.

Ushaanza Alfu-Lela-U-Lela hapa
 
Bin Maryam,

I feel you on this. Kuna watu wanasema "be careful what you wish for, you may receive it".Basically I am envisioning watu washaitoa CCM na tuna upinzani kwenye power bila institutional changes. Watakubali kuji clip wings in the interest of government efficiency and integrity au ndiyo tutaona kama mambo aliyoleta Kibaki alipochaguliwa mara ya kwanza?

My fear is that human nature is too unrealiable, that is why we need clear institutional changes at least simultaneously with regime change, if not before.


Kuna utafiti mmoja uliofanya. Katika utafiti huu, timu mbili zenye kiwango kilicho karibu zilijiandaa Kwa mashindano. Timu ya kwanza ilijiandaa kwa kufanya mazoezi ya nguvu na kutumia muda mrefu mazoezini. Na timu ya pili ilitumia mazoezi na kusoma wapinzani wao kabla ya michezo kwa kuangalia video.

Matokeo ya utafiti huu ni kuwa timu iliyotumiwa muda kusoma wapinzani wao kwa kuangalia video ilipata mafanikio mengi kuliko ili timu iliyotegemea mazoezi ya nguvu.

Kwa mtaji huu kuondoka CCM madarakani itawasaidia CCM kukaa na kuangalia makosa yao kama vile hile timu iliyotumia video.

Na CCM kuendelea kutawala na kujirekebisha kwa kutumia tume ni sawa na hile timu inayotumia mazoezi pekee kama njia moja ya kupata ushindi.

CCM kuondoka madarakani ni kwa mapungufu. Na hayo mapungufu yanaonekana wao wakiwa nje ya utawala. Wao kuendelea kukaa madarakani hakuwafundishi chochote kile. Na hii sio kwa CCM pekee yake bali kwa vyama vingine vya siasa, mameneja wanaongoza mashirika yetu, wabunge, wakuu wa wilaya au mikoa.

Na kuhusu taasisi unazotaja ni kitu chepesi sana. Taasisi hizo si nyingine bali ni watu wanaoziongoza au kuzifuata. Hivyo mafanikio na mafungufu ya taasisi hizo ni sawa na watu wanaoziongoza.

Mfano: kuhusu taasisi. Mwanzoni mwa 90, ilifikirika kuwa matatizo ya mabenki yetu ni ukosefu wa matumizi ya zana bora kama vile computers. Na kumbuka NBC wakaanza kuweka ma-computer katika matawi yao. Lakini pamoja na computers hizo, NBC iliendelea kuwa nyuma kutimiza malengo yake. Matatizo ya NBC hayakuwa katika matumizi ya computers bali kwa waendeshaji wake.

Kwa hiyo taasisi unazosema are as good as the people who operate them.
 
Pundit bado nasubiria kuona ukisema namna ambavyo institution zitabadilishwa kabla ya kuwapa wapinzani uongozi.

Hapo ndo mimi naona kizunguzungu....maana jamaa hawataki. Sasa kama hawataki sijui tuna alternative gani tena...
 
Unaweza vipi kubadili institutions bila kubadili fikra za watu?

..kwa kuonyesha mfano kuwa mabadiliko ya aina yoyote ile yanawezekana na hakuna mfano mzuri kama kuking'oa chama tawala kutoka madarakani. Kama hilo linawezekana kwa nini mengine (including fikra, spirit, confidence, etc.) yasiwezekane?
 
Tatizo ni kwamba watu hatujiamini na hatuamini nguvu ya umma, tumeona waandishi habari na watu wa upinzani walivyofunua maovu mpaka PM kajiuzulu.Miaka michache tu iliyopita jambo kama hili halikuweza hata kufikirika.

Uzuri wa maswala ya institutional changes ni kwamba ni maswala ambayo yako cross party.By that I mean kuna individuals kwenye vyama vyote, -ikiwamo CCM although the higher you go there the more dissapointing the picture becomes- ambao wana genuine interest na reform.Kuna watu kama kina Nyalali walishaandika siku nyingi tu umuhimu wa kuwa na mgombea binafsi, jambo ambalo CCM inalipinga kwa sababu inajua kuna wabunge wengi machachari wanadhibitiwa na chama na kama wakiwa na nafasi za kusema wenyewe kama wabunge wa tiketi ya mgombea binafsi CCM watakoma.

Kwa hiyo kinachotakiwa ni pressure juu ya pressure.tena huyu huyu muungwana ndiye anayefaa kupigiwa mi pressure yote maana ana crack.Tusije kusubiri subiri tukaletewa jizi-jeuri-uaji kama Mkapa mkiandamana mnakula shaba na jitu halisikii kitu kisha linapindisha maneno kwa kusaidiwa na hao "Economic Hitmen" kama halina akili nzuri, kama umemsoma Rev. Kishoka katika "Thank God for Kikwete" utaweza kuoanisha maudhui yake na yangu hapa.

Tunaweza, tunachotaka sasa ni kupata escape velocity tu itakayotuwezeka kupata lift off ya uhakika.For a minute I was beginning to think kujiuzulu kwa Lowassa kungeweza kutumiwa kama hiyo lift off, lakini naona hatuja capitalize vizuri hapo.Next on the ajenda ni kumshitaki Mkapa.

Kwa miaka mingi sana watu walikuwa wanafikiri haiwezekani binadamu kukimbia maili moja katika dakika nne, wakajaribu sana watu wengi wakashindwa (at least recorded events).Mwaka 1954 Roger Bannister akaweza kuivunja hii rekodi, mara baada ya kuivunja na watu kujua kuwa inavunjika watu wengi tu waliweza kuivunja.

Tunachohitaji ni "a Roger Bannister" moment ya kutuwezesha kufahamu kwamba tunaweza.Kutoka hapo itakuwa kama wanavyosema watoto wa mjini "kumsukuma mlevi".
 
Tulipowaondoa wakoloni tulifanya wakati huo huo kuingiza watu wapya. Tulifanya hivyo tukiamini kuwa wakoloni ndiyo kizuizi cha maendeleo yetu na hivyo wao wakiondoka tukishika sisi wenyewe basi mambo yatakuwa mazuri.

Matokeo yake ni yapi? Wale tuliowaingiza si walifanya vizuri mwanzo lakini baadaye wameanza kugeuka na kuitwa wakoloni weusi? Na kuna watu wamefikia kudiriki hadi kusema "bora mkoloni"!

Sasa, tunapotamania kuiondoa CCM na utawala wake huku tukitumaini kuwa wale watakaoingia watakuwa bora zaidi. Matumaini hayo yanajiandaa kufeli kama sheria ya pili ya thermodynamic (the law of entropy) of which my esteemed friend Pundit is very familiar with inavyotuhakikishia.

Kwa hiyo naamini tunapanga na kufikiria kuing'oa CCM ni lazima tuwe very focused kuwa hatuing'oi CCM ili tubadilishe tu (cosmetic change) bali tubadilishe kwa kilichobora. Lakini pia hatuna budi kutambua hata hicho kilichobora nacho kitavuruga (the law of entropy). Jukumu letu basi ni kuhakikisha hicho kilichobora kinazuiwa kuvuruka kwa kiasi kikubwa kama wale tuliowatoa.

To me the question is, tunajuaje kilichobora ambacho chapaswa kuchukua nafasi badala ya CCM na viongozi wake? Je tunatafuta chama au watu?


Mwanakijiji:

Nilifanya utafiti mbuzi hapa. Na hitimisho nalopata japokuwa kichwa changu hakikubali ni kuwa kuna credit inabidi Nyerere nimpe.

Mkoloni aliacha vitu vyenye gharama na ambavyo vingeweza kutusaidia katika maendeleo ya haraka lakini tumevitupa. Utafiti wangu mbuzi unaonyesha kuwa sense ya ownership ni kitu kinachochangia kwa mtu kuwajibika na kile alichonacho.

Wakati mkoloni anatawala hakuna mwaafrika aliyejisikia kuwa shirika la reli ni mali yake, shule anayosoma ni mali yake. Vitu vyote vilivyomzunguka mwafrika vilikuwa ni mali ya serikali ambayo kwa kiasi kikubwa ilitumika kumnyonya.

Mpaka sasa bado kuna watu wengi tu ambao hawaoni umiliki wao wa mali za serikali. Hivyo mtu yupo tayari kuipotezea nchi mamilioni ya pesa hili apate visenti kidogo vya yeye kujijengea nyumba na familia yake.

Na tusione aibu kwa hili kwa sababu inaonyesha wakati utawala wa warumi ulipoporomoka nchi zilizorithi au kujitokeza zilishindwa kuendeleza miundo mbinu iliyoachwa na watawala wa kirumi.

Kwa mfano watu walibomoa mifereji ya maji (aqueduct) kupata matofali ya kujengea vibanda vyao na kusahau kuwa mirefeji hiyo ndio iliyokuwa chanzo chao cha maji.

Na katika utafiti wangu huo mbuzi, nilipata kitabu kinachosema kuwa inachukua zaidi ya miaka 40 kwa waliotawaliwa bila kuwa na sense ya ownership kuweza ku-master skills za waliowatawala.

Tukirudi kwenye mada, kama kuna idadi ya kutosha ya watanzania wanaoona kuwa taasisi ni mali ya taifa na ziendelezwa kwa ajili ya maendeleo ya taifa basi mabadiliko ya sasa hayatakuwa kama yale ya 1961 au 1967. Hivyo hakuna sababu ya CCM kung'ang'ania madarakani.
 
Pundit... that is where I'm going.. unaweza vipi kubadilisha taifa la watu ambao hawajiamini? Unaweza vipi kubadilisha Taifa la watu ambao wanaona hawawezi? Je Taifa la watu wanaojihisi ni duni kuwa walichonacho ndicho wanastahili linajengwaje?

Bila kubadilisha fikra unaweza vipi kufanya watu waamini wanaweza na hivyo wanapaswa kubadilisha wasichokitaka (CCM). Ndio maana binafsi siamini kuwa lengo la kuiondoa CCM madarakan in and in itself linatosha kufanya watu washabikie.
 
Pundit... that is where I'm going.. unaweza vipi kubadilisha taifa la watu ambao hawajiamini? Unaweza vipi kubadilisha Taifa la watu ambao wanaona hawawezi? Je Taifa la watu wanaojihisi ni duni kuwa walichonacho ndicho wanastahili linajengwaje?

Bila kubadilisha fikra unaweza vipi kufanya watu waamini wanaweza na hivyo wanapaswa kubadilisha wasichokitaka (CCM). Ndio maana binafsi siamini kuwa lengo la kuiondoa CCM madarakan in and in itself linatosha kufanya watu washabikie.

...unaweza kwa kuonyesha kuwa yote (au niseme mengi) yanawezekana...tunaanzia na kuing'oa CCM....how earth shaking that would be?
 
Unaweza vipi kubadili institutions bila kubadili fikra za watu?

Pamoja na institutions nimetaja pia kuinua elimu na pia elimu ya uraia. Hata kama una sheria nzuri vipi, kama mkandamizwaji hajui anakandamizwa au hajui kudai haki yake basi sheria hizo haziwezi kuwa effective.

Leo wanaosoma magazeti ni 3% ya population, katika hao wanaoelewa na kumaliza habari muhimu labda ni 1.5 % katika hao nao 0.75 watakuwa wamesoma habari zisizo sahihi, 0.75% iliyobaki labda 0.5 tu ndiyo watasoma habari sahihi na kuzifanyia kazi hata kama ni kwa kuzieneza tu.Kwa hiyo effective readership inaweza kuwa as low as 0.5 ya population, ambao hata hao nao 0.25 bado wanaweza kuwa ni mafisadi wasiotaka kuielewesha jamii.

Tunabakia 0.25 baadhi yetu tunaokuja hapa JF, wanafunzi fulani wa vyuo vikuu, wengine washua washajichokea etc etc.

Bottom line inabidi kuwaelimisha na kuwa involve watu zaidi katika political process.
 
Wait a minute....hivi debate hapa ni ipi?...kwamba wapinzani hawawezi kutuletea maendeleo wakipewa nchi/ wapinzani hawako tayari kuongoza au tunahitaji mabadiliko ya kikatiba kwanza kabla ya wapinzani kuwa tayari kushika madaraka au kwamba tunahitaji mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili tuweze kupiga hatua mwenye maendeleo?
 
Wait a minute....hivi debate hapa ni ipi?...kwamba wapinzani hawawezi kutuletea maendeleo wakipewa nchi/ wapinzani hawako tayari kuongoza au tunahitaji mabadiliko ya kikatiba kwanza kabla ya wapinzani kuwa tayari kushika madaraka au kwamba tunahitaji mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili tuweze kupiga hatua mwenye maendeleo?

Chicken and egg what comes first or whatever....but the what we need is Chama Cha Mafisadi to go out, the rest will follow. If it is kubadili katiba let the wapinzani promise that, if its building strong and accountable institutions let them promise that as well. If they won't fulfil, we will vote them out either rather that remaining with the mafisadi's we know who are for fact mafisadi. Better the wapinzani we don't know rather than the CCM we know that are mafisadi. There are countries which have succceded for taking out of office the failing, ailing and corrupt regimes, the list of successful changes is longer that the few aborted changes as the case of Kenya. So we better bank on change than know change. If you are ready for change, please stand up!

Asha
 
Nyani.. swali lenyewe lina makosa.. hakuna mtu "atakayewapa" wapinzani nchi; wapinzani wanaweza kuichukua nchi kwa kutuata taratibu za kidemokrasia... yaani hawatapewa kama zawadi; kupewa kwao nchi kutatokana na wao kustahili na kuonesha kuwa wanastahli kupewa kwa kupigiwa kura.

Ndipo hapo mjadala ulipogeuka; kwanini watu wawape nchi? Lazima kuwe na sababu. Kwanini wawape nchi wapinzani na wawape ili kiwe nini...?
 
Nyani.. swali lenyewe lina makosa.. hakuna mtu "atakayewapa" wapinzani nchi; wapinzani wanaweza kuichukua nchi kwa kutuata taratibu za kidemokrasia... yaani hawatapewa kama zawadi; kupewa kwao nchi kutatokana na wao kustahili na kuonesha kuwa wanastahli kupewa kwa kupigiwa kura.

Ndipo hapo mjadala ulipogeuka; kwanini watu wawape nchi? Lazima kuwe na sababu. Kwanini wawape nchi wapinzani na wawape ili kiwe nini...?

Hilo la swali kukosewa hata mimi nililiona....

Ni kweli lazima kuwe na sababu na sababu yenyewe ni CCM wameshindwa kuongoza.

Umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini CCM inaendelea kuwa madarakani huku taifa likibomoka badala ya kujengeka?
 
Hilo la swali kukosewa hata mimi nililiona....

Ni kweli lazima kuwe na sababu na sababu yenyewe ni CCM wameshindwa kuongoza.

Umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini CCM inaendelea kuwa madarakani huku taifa likibomoka badala ya kujengeka?

Mkuu

Haya tunayoyajadili sasa yote CCM wanayajua vizuri sana. Walishayaona, walishajua ulaji wao umesimamia wapi. Ndio maana mwanasheria Mkuu wa serikali na waziri Mhuusika wakisikia mtu yeyote anataja suala la kuandika katiba huwa wanakuwa wakali sana.

Matatizo yote yanayohusu maendeleo yamekamatiwa hapa hapa.

Ndio maana kunahitajika kubadili strategy hili kuweza kufikia hapa. Transition yoyote huwa haiwezi kuja kirahisi.

Kunaitaji wakati mwingine wapinzani wawe more technical katika kuvuka kikwazo hiki. Hapa tulipofikia ndipo kuna daraja la kwenda ngambo ya pili. Ambako aliyeko madarakani ameondoa baadhi ya mbao.
 
Hilo la swali kukosewa hata mimi nililiona....

Ni kweli lazima kuwe na sababu na sababu yenyewe ni CCM wameshindwa kuongoza.

Umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini CCM inaendelea kuwa madarakani huku taifa likibomoka badala ya kujengeka?

Wana ccm wanajua kuwa badala ya kuamuka na kuwatoa toka huko madarakani, watanzania tutaanza kujadili kwanza nini kitatokea baada ya ccm kwenda na matokeo yake nothing will ever get done!
 
Back
Top Bottom