Ni bahati mbaya kwamba sijapata nafasi ya kupita hapa kwenye jarida letu tangu jana. Pamoja na michango katika mada zilizokuwepo, nimekutana na hii thread mpya ya Mh. Mzee Mwanakijiji. Niliamua kuanza kuisoma hii maana huwa namumini sana huyu mheshimiwa katika kuibua mambo kwa lugha nyepesi hadi kwa lugha ya mbwembwe ya mazingaombwe na ushairi! Lakini nasikitika kwamba huyu mheshimiwa sijui kitu gani kimetokea hapa maana katika siku za karibuni kweli amebadilika; sio Mwanakijiji niliyemjua. Naanza kujiuliza hivi ni yeye au kuna mtu amevamia jina lake. Maadamu hajakanusha kwamba sio yeye itabidi niendelee kuamini tu kuwa ni yeye. Labda tu ameokoka. Basi ngoja nami nikabiliana na huyu mlokole wetu mpya.
Kwanza, hakuna hata sehemu moja popote pale katika jarida hili, kwenye vyombo vya habari, katika sera au katika mikutano ya hadhara ambapo wapinzani wamewahi kusema kuwa wao wakiingia madarakani basi matatizo yote yatakuwa yamekwisha. Ndio nasema huyu mheshimiwa labda ameokoka kwa sababu sio kawaida yake ku-make sweeping statements namna hii.
Wanachosema wapinzani ni kuwa CCM imeirudisha nchi nyuma sana. Hatupigi hatua, hasa katika kipindi hiki cha JK. Mifano ipo wazi kabisa kuonesha kuwa hatuendi mbele kuanzia kwenye vigezo vya takwimu za kiuchumi za kitaalamu (macroeconomic indicators) kama vile kukua kwa pato la taifa, thamani ya shilingi, n.k. hadi kwenye maisha ya kila siku ya mtanzania. Kwa mfano takwimu za leo zinaonesha kuwa ukuaji wa uchumi wa Taifa umeshuka katika kipindi cha mwaka mmoja cha JK. Thamani ya shilingi imeshuka kuliko maelezo tangu hao wasanii waingie madarakani. Katika maisha ya kawaida, karibu kila bidhaa muhimu imepanda zaidi ya mara 100 katika kipindi cha mwaka mmoja cha ndugu yetu JK. Kwa mfano sukari ilikuwa inauzwa katika ya sh. 800-1200 hadi Mkapa anaondoka; sasa hivi inauzwa kati ya sh. 2400-3600! Hivi ni baadhi ya viashirio kuwa CCM wanaendesha serikali vibaya.
Sitaki kurudia mambo ya mikataba ya umeme. madini, rushwa, n.k. Haya hata wewe umekiri katika mawasilisho yako japo kwa kebehi. Sijui kwamba kama ni tatizo au la, hiyo nakuachia mwenyewe.
Kikubwa zaidi ambacho tunapigia kelele serikali hii ya chama cha majambazi ni uongo. Kwa kipindi cha chini ya mwaka mmoja serikali ya JK imeongopa zaidi ya mara tano. Mbili kati ya hizi ni muhimu kuzitaja:
i)Rais mzima alidanganya wananchi kuhusu umeme wa Richmond kuwa ungeanza Octoba. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza Rais kusema uongo bila aibu katika historia ya nchi yetu. Yaani hata hakuwahi kujutia
ii) Serikali ya CCM wamedanganya mara tatu kuhusu mradi wa mabasi yaendayo kasi. Kwanza walisema ungeanza Agosti 2006; halafu wakasema utaanza January 2007. Sasa leo wamesema utaanza March 2009 karibu na uchaguzi mkuu wa 2010!
Sasa katika mambo yote haya unataka wapinzani wasisema. kazi ya nini basi? Kwa hivyo wanachosema wapinzani ni kuwa nchi haiendi mbele kimaendeleo. Hi ni kwa sababu alipoiachia Nyerere, Mwinyi akaja akaturudisha nyuma, akaja Mkapa akaturidisha nyuma kutoka pale alipotuachia Mwinyi. Huyu kaka yangu JK ndo inaonekana anaturudisha nyuma tena kwa kasi mpya ya ajabu. Ndiyo, tutasemaje kama ameweza kuongeza deni la nje kwa $385milion chini ya mwaka mmoja katika kipindi chake cha uongozi? Halafu unataka tumpigie makofi, kwa yepi hasa?
Katika matatizo haya, wapinzani hatusemi eti tutayamaliza kama ukungu. Tunachosema ni kuwa: 1) Hatutakuwa wanafika kwa kuwapa wananchi ahadi za ghiliba ili watupigie makofi. Tutasema kile ambacho tunataka kukifanya na ambacho tuna uwezo nacho. 2) Tutaweka misingi imara ya demokrasia ili kwamba wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha viongozi. Na hapa ndipo palipo na matatizo. Viongozi wa CCM wanajua wapo juu ya sheria; wanachosema wao basi kinatosha. Ndio maaana mikataba ya maana wanasaini kisirisiri lakini Taifa zima linaumia. Mambo muhimu yanayotakiwa kwenye katiba hawataki kuyaweka maana hawataki kujifunga. Sasa nchi zozote zisiongozwa kidemokrasia lazima ziishie ilipoishia CCM. Ni ghiliba mtindo mmoja; hata mtu akiteuliwa UN wanachukua sifa wao. Mtu akipata scholarship ya kusoma nje wanasema ni kazi ya CCM. Watu wanahangaika na msongamano hakuna barabara Dar, wao wanasema eti kwa kuwa wameleta maendeleo kwa kasi mpya hadi magari yamejaa barabara hazitoshi! Yaani ni usanii tna ghiliba tu ndo kinachoendelea. Kwa mtindo tusifie kitu gani hasa?
Kwa kifupi, hakuna njia ya mkato katika kuiletea nchi yetu maendeleo maana uharibifu uliofanyika ni mkubwa. Lakini tunahitaji kupiga hatua, na tuonekana kwamba tunapiga hatua. Sasa hivi hatupigi hatua, na ushahidi upo kedekede. Tukisema tusionekana kwamba eti sisi tunafikiri tutamaliza matatizo kama ukungu.
Usiwalishe wapinzani maneno. I believe you are not playing part of CCM gimmicks and manipulations!