Upinzani unaoonekana sasa hivi upo na sura mbili, ndani ya CCM kwa CCM na CCM against CHADEMA.
Nitawakosoa nyinyi ambao mnatumia lugha chafu kwenye siasa na kutoa ushauri kwenu nyote:
Ni hivi, unapokuwa huna hoja hutatoa mtizamo sahihi wa kile unachokisema matokea yake unapotaka kudraw attention utatumia matusi na lugha chafu kuwafanya watu waone hisia zako bila kujua zimeletwa na nini.
Chadema mna watu wazuri saaana na watu wabovu kupitas maelezo. Kitakachowasumbua sana ni kile ambacho baadhi yenu wanakifanya na si kizuri kwa chama chenu, kutumia jazba na matusi kujenga hoja. Ninawataka wana CDM wooote kujipanga, someni hoja za CCM kama mpinzani mkuu, angalieni yale ambayo mnaweza mkayafukia kwa hoja zenu mpya na nzito. Na hii ndiyo ilikuwa siri ya ushindi wa kishindo wa Baraka Obama pamoja na mapungufu yoooote ya kihistoria na "kihadhi" ya kugombea uraisi.
CHADEMA kichwa sasa lazima kiwaume kujua mgombea anayeuzika katika uraisi ujaon ni nani? Maana kwa sera zenu za mgombea ni mara moja safi, democrasia ya kweli, nani atakayezidi uzito wa Dr. Slaa katika kuuzika? Ukiniuliza mimi, nadhani ni mojawapo wa vijana ambao kifikra wako fresh an wana moyo wa kuthubutu hata hoja zao mpaka sasa zinamwelekeo na mvuto wa hali ya juu, tunawaona kwneye vyombo vya habari. Sio Zito tafadhali! Shida mtakayoipata ni kuwa hawa CCM wanoongoza tayari walishaichakachua katiba na kulazimisha nchi hii iongozwe na wazee zaidi. Hivyo kwa hoja yangu kampeni ya Katiba mpya isilale iwe kipaumbele mpaka mate ushindi.
CCM imechafuka inanuka na imejaa matope, kwasababu tu wako baadhi ya watu walijimilikisha chama. Na hii kafara anayojitoa Nape, haiwezi kusahauliwa na wanachama wake, ama sivyo watakuwa wamekosa fadhila. Achilia mbali udhaifu fulanifulani aliyonao ambao upo pande zote za siasa wa kutumia personality ya kiongozi wa upinzani kujenga hoja badala ya sera. Anafanya kazi nzuri kweli kweli Bwana Nape kwa CCM kwa sasa na wako wengi tu ndani ya CCM hawapendi anachofanya maana kinaharibu yale matope waliyojipaka ili wasionekane huko waliko.
CCM mna nafasi ya kushinda iwapo tu mtagawanyika kati yenu na kikazaliwa chama kipya kikiwa na wanamabadiliko wa kutosha ndani ya chama. CCM imepoteza umaarufu kwelikweli kwasababu za siasa za Makundi. Maana shida yenu CCM mlijikita sana kweney mfumo wa serikali na usalama hivyo inawawia shida upinzani kupata ushindi wa kweli. Ila kwa hivi mlivyo tayari kama kutafanyika utafiti wa umaarufu wa chama na uongozi, hamtaamini matokeo yake.
Msijidanganye nchi hii mnaipeleka pabaya msisubiri mkajikuta mmechelewa, ongezeni kasi ya mabadiliko, na wale wanaoona wanaweza kujiengua basi liwepo kundi kubwa la kutosha kuleta nguvu ya upinzani wa kweli.