Je, wapinzani ni wakombozi?

kama sheria inasema siku 7 basi itakuwa ni ujinga kunyamazia kitu hiki badala ya kupinga mahakamani mara moja.
 
NEC imenishangaza,eti imewaongeza wapiga kura 56 tuu huku ikikataa kuwaandikisha wapiga kura wengine wenye vigezo
 
NEC is just like a revised CCM. Kwa hiyo lazima itekeleze matakwa ya boss wake CCM.
 
Tume imetoa ufafanuzi na kukanusha kuwa hivyo vituo 55 unavyovisema havipo na kama kuna ushahidi wa kuvitambua vitue hivyo si muutoe ili hatua zichukuliwe!
 
Tunahitaji
ukombozi
wa kweli
yatupasa kupiga kelele. Tusikae kimya siku si nyingi tutakuwa tumepata ukombozi. Kuendelea kubaki kuwa mwana ccm ni kwamba wewe ni maiti.
 
Hoja hizi si za kupuuza hata kidogo. Zifanyiwe kazi mara moja ili kuepuka majuto ni mjukuu.
 

Mzee MM, mimi nijikite kwenye para ya mwisho. Ninakubaliana na wewe 100% kwa assessment yako. Ila mimi binafsi bado ninaona wapinzani ni wakombozi kwa sababu zifuatazo
  1. Kitendo cha CCM kushindwa uchaguzi na chama mbadala kuchukua uongozi itakuwa ni one big step towards having a government which is accountable to the people not party tycoons.
  2. Unapokuwa madarakani kwa kuahidi kufanya kitu fulani, ni dhahiri utajitahidi ukijua kuwa kutofanya hivyo ni kuwafanya waajiri kukuweka kando uchaguzi mwingine
  3. Kitendo cha CCM kushindwa kitawafanya watu wanaoona siasa ni ajira kukaa pembeni na kuacha watu wanaoona siasa ni wito na uzalendo wa kufanyia nchi mazuri
  4. Kutokuwa na chama monopoly wa serikali maana yake ni kuwa vyama vitashindana katika kuonesha nani ameweza kuipeleka nchi katika prosperity. Hivyo basi kupisha vichwa makini vyenye uwezo wa kijasiliamali wa kuendeleza nchi kuwa kidedea kila wakati.
  5. Kwa CCM kushindwa itakuwa ni reset button kwa nchi kujiangalia upya katika kipindi kingine baada ya kupoteza miaka karibu 50 baada ya uhuru bila kuwa na mikakati practical, ukiacha slogans za kuombea kura.
  6. Ule mtindo wa kupeana vyeo kwa urafiki na kujuana bila kujali uwezo utaisha, maana kumuweka mbumbumbu katika nafasi ya utendaji ni kujichimbia kaburi uchaguzi ujao.
  7. Pia ni matumaini yangu kuwa CCM ikiwa nje ya madaraka Tanzania itapata mageuzi ya kweli ya kiuchumi na kisiasa. Kutakuwa na utendaji mzuri wa serikali na uwajibikaji tofauti na kulindana kunakofanywa na CCM
  8. Ni matumaini yangu kuwa vyombo vya dola vitakuwa huru bila kuwa affiliated na chama chochote na hivyo kutokumuogopa mtu yeyote kwa amri ya yeyote, hii ni baada ya kupata katiba ya watanzania (Siyo hii ya CCM inayopigiwa chapuo sasa)

Kwa maana hiyo bado ninaamini kuwa Tanzania yenye uongozi bora na imara itakuwa ni Tanzania yenye kujali watu zaidi kuliko makundi ya kirafiki yanayofanywa na CCM. Ni matumaini yangu kuwa CCM nje ya power itakuwa ni chachu nzuri ya kuwapukutisha kupe wote walioji-attach kwenye chama na kutoka povu kwa kujifanya makada wazuri wakivizia nafasi za uongozi ili waliibie Taifa na Watanzania.

Ni ukweli usiopingika kuwa Matatizo haya ambayo yamejengwa polepole kwa kipindi cha miaka hamsini hayawezi kumalizwa na chama chochote cha siasa kwa usiku mmoja au muhula mmoja au miwili, ila nina hakika kuwa watanzania watakuwa better-off when CCM is out of power. Pia ninaamini kiusalama wa Taifa na ustawi wa amani itakuwa ni national security interest when CCM agrees to let Tanzanians choose freely their leaders without intimidations and chakachua. Ule usemi wa mtoto akililia wembe mpe una maana kubwa sana hapa katika kunyamazisha kilio cha watanzania, kwani wengi wana kiu ya mabadiliko, kama watayapata pasi watatulia, ila kama watanyimwa basi wanaweza shawishika kufanya kitu kibaya na kusababisha maafa yasiyo ya lazima.
 

mkuu, mi nafikiri kwanza katika bold uwe umejiridhisha vya kutosha kuwa wananchi huwa wanipa ccm pindi wanapopiga kura, una uhakika huwa wanaipa au ccm wanajipa wenyewe kwa kuiba ama kujiwekea kura ili kuzidisha wingi wa kura unaopelekea ushindi. ushahidi tunao sehemu n yingi ccm wamekuwa wakiiba kura hata tabata katika uchaguzi uliopita mgombea wa ccm alitaka kuuwawa na wananchi baada ya kukimbia na box la kura akisaidia na askari.
haya bado huwezi kusema vyama vya upinzani hawajafanya lolote wameshafanya baadhi ya mambo na kushinikiza mengi hapo ndio wapo wachache! kumbuka mkuu kuwa ikipigwa kura ya ndio au siyo lazima ccm washinde bungeni sasa mabadiliko ni magumu kuonekana ama kuja kirahisi. wangekuwa wengi hapo tungesema jambo la lawama. nafikiri wakipewa nchi wanaweza kubadilisha maisha ya mtanzania ikiwa kwa sasa kwa udogo wao wameshafanya vitu vingi ikiwa pamoja na kufanya uwazi wa mambo mengi yanayosaidika kudai mabadiliko.
udhaifu wa wapinzani ni kweli kuna migongano na mikwaruzo lakini hii haimaanishi hawawezi kufanya vizuri wakishika madaraka. kumbuka kuwa waliopo katika vyama vya upinzani ni binadamu wenye interest tofauti na tabia tofauti hata ndani ya ccm kuna migongano na mizozano.
wakipewa nafasi wataweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…