Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #101
It was practically wrong and politically damaging for Zito to say that we (chadema) cannot lead the country better than CCM, if he truly made this remark, which I doubt!!!!
MWANASIASA!MKJJ:
Sina uhakika kuwa umri wa chama ni kigezo kizuri cha kuona kuwa kitaweza kuongoza vizuri au la. Angalau mifano haituambii hivyo. Chama cha John Kufour nadhani kilikuwa na umri mdogo sana ukilinganisha na cha Rawlings kilichoshindwa. Lakini ni ukweli kwamba chama cha Kufour kimeweza kuleta maendeleo ya ajabu kama vile Ghana ndiyo kwanza ilipata uhuru katika miaka kumi aliyoongoza. Vilevile kilichokuwa chama tawala Senegal kabla ya chama cha Rais Wade kiliongoza ile nchi kwa zaidi ya miongo minne, lakini maendeleo yaliyopatikana katika miaka kumi ya utawala wa chama cha Wade kila mtu ni shahidi. Mfano mwingine wa karibu zaidi ni Kenya. Pamoja na matatizo yote ya chama cha NARC, ni ukweli usiopingika kuwa wakenya wengi leo wasingependa warudi katika enzi za KANU. Kwa hivyo umri wa chama cha siasa katik hili sidhani kwamba ni hoja.
Sikubaliani na Zito anaposema kuwa chadema ikipewa nchi sasa hivi haitaongoza vizuri. Bahati mbaya sijasikiliza mazungumzo yako na Zito, lakini kama kweli alisema hilo na kama viongozi wote wa chadema wanafikiri hivyo, basi kuna tatizo. Kuna ugonjwa unaitwa hypochondriasis. Huu ni ugonjwa lakini sio wa kimwili bali wa kisaikolojia. Ni pale mtu anapohisi anaumwa wakati haumwi, na madaktari wakimwambia haumwi haamini kuwa haumwi. Sasa huenda Zitto na viongozi wengine wa chadema wana huu 'ugonjwa'. Lakini mimi kama mwanachama wa kawaida wa chadema najua kabisa tunaweza kuongoza tena vizuri sana kuliko hao ccm kwa sababu chadema ina dira na sera bora zaidi kuliko CCM na ina watu wenye elimu ya kutosha na uzoefu wanoweza kuongoza serikali. Yeye mwenyewe Zito ana uwezo wa kushika nafasi yeyote katika serikali ikiwemo ya urais; bahati mbaya inaonekana hajui au ana-underestimate uwezo wake.
Nafikiri pia kuna tatizo la kufikiri kuwa chama kingine kikiingia madarakani basi kila kitu kitabadiliko. Kinachobadilika ni sera (policies) na baadhi ya sheria na viongozi wa kisiasa. Watendaji wengi wa serikali watabaki kuwa walewale. Jeshi litabaki kuwa lilelile. Polisi ni walewale. majengo na ofisi zilezile. magari yaleyale isipokuwa yatapunguzwa, n.k. Sasa sijui hii dhana kwamba tutashindwa kuongoza inatoka wapi.
Tatizo kubwa la vyama vya upinzani so kukosa uwezo wa kuongoza kwa maana ya dira, sera na mikakati ya kuongoza nchi. Isipokuwa ni kukosa taswira ya kuweza kuchagulika. Na bahati mbaya katika nchi zetu taswira ya chama ni kigezo kikubwa cha kuweza kuchaguliwa kuliko sera na mikakati ya chama ya kuongoza. Ingekuwa wananchi wanaangalia sera na uwezo wa viongozi CCM ingekwishafukuzwa madarakani siku nyingi. Ni katika Tanzania pekee ambapo Rais anaweza kusema uongo zaidi ya mara tatu na wananchi wakaona ni jambo la kawaida. Hili ndio jambo la kufanyiwa kazi na vyama vya upinzani. Kuwafanya wananchi waanze kujali mambo makubwa kama sera za maana dhidi ya mundane issues kama sura za viongozi na ukongwe wa chama.
It was practically wrong and politically damaging for Zito to say that we (chadema) cannot lead the country better than CCM, if he truly made this remark, which I doubt!!!! Clearly, there are things you can't say in politics however true they may be!
Mkandara!Mwanasiasa,
Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Kuna kitu kinamsumbua Zitto nje ya yote aliyoyasema. I mean kila statement yake inazidi kunitia wasiwasi zaidi. Na hasa mahojiano yake na MJJ kuna vipande kaboronga kama vile mtu anayetafuta support ya wananchi zaidi ya Chadema. Nina mashaka kama hayakutokea yale yaliyomkuta Harper.
Mwakijiji,
Nakushukuru tena kwa kurejesha hii hoja ya "wapinzani ni wakombozi".
Nimesoma hoja za mwanasiasa, nakubaliana nami. Lakini kwa bahati mbaya nami sijasikiliza mahojiano ya Zitto. Huku nilipo ni ngumu ku-down load mahojiano. Nitachangia hoja hii nikishayasikiliza mahoajiano husika.
Lakini dhana ya kwamba wapinzani hawana uzoefu wa kuungoza sikubaliani nayo kabisa. Nitachambua kwa facts baada ya kusikiliza!
Dhana hii ilitumika sana pale Ubungo katika hatua za awali ikisemwa kwamba Mnyika hana uzoefu Keenja ana uzoefu.
Kwa kweli wakati ule nijibu dhana hii kwa maswali ambayo naamini yanaweza kutumiwa pia katika muktadha wa Taasisi(ikiwemo CHADEMA)
1. Hivi tunataka UZOEFU au UZEEFU? Uzoefu is a very subjective term. Watu wengi wanafikiri uzoefu ni miaka! Unaweza kuwa na miaka michache ukawa na uzoefu zaidi ya mwenye miaka mingi(wachambuzi wajadili)
2. Hivi tunahaja ya kuwa na UZOEFU au MZOEFU wa KUHARIBU? Kati ya mzoefu wa kuharibu na asiyekuwa na uzoefu wa kuharibu yupi bora? Je CCM wana uzoefu wa nini?
3. TANU iliingia madarakani ikiwa na miaka michache kuliko serikali ya mkoloni, je TANU ilipaswa kuachwa ili MZOEFU mkoloni aendelee? Miaka ya serikali ya TANU takribani 15 na ile ya MZOEFU CCM ya kuanzia 1977 mpaka 2007(30) ipi ilikuwa bora? Kwa nini uzoefu wa CCM usiwe mzuri kuliko TANU kimaadili, kukua kwa uchumi, elimu na tofauti ya pengo kati ya masikini na matajiri?
4. Hivi UZOEFU haupandi na kuanza kuporomoka? (In other words is experience not subjective to the law of diminishing return?)
5. UZOEFU hauzai URASIMU na UHAFIDHINA wa kukataa mabadiliko na fikra mbadala? Je uzeofu hauleti ugonjwa wa kufanya mambo kwa mazoea?(Matokeo ya ugonjwa huu ni kulindana na kurudia rudia-rejea dhana ya mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale wa chama kile kile wakiendeleza yale yale kwa ari,kasi na nguvu mpya).
6. UZOEFU sio kitu mahususi? (is experience a specialization?) Mathalani CHADEMA ina uzoefu na falfafa ya nguvu ya umma ama inauzoefu na sera ya Majimbo, je kama unayataka haya si afadhali uipe fursa CHADEMA badala ya kuwashauri CCM kuyafanya haya kwa kuwa hawana uzoefu nayo?
7. UZOEFU sio chanzo cha ubinafsi?(the feelings of only me can because only me can!). Matokeo yake ni kutengeneza kikundi cha watawala wachache wale wale.(closed cycle). Lakini ukichagua kikundi ambacho kiko tayari kufungua macho nje kitachukua hata watu walio nje ya vyama ama mfumo wa utawala na kuwaingiza kwenye mkondo wa uongozi.
8. Chama ni uongozi, hivi ukichukua wakuu wa wilaya, mikoa, baraza la mawaziri mmoja mmoja je wote wana UZOEFU wa miaka mingi unaosemwa? Kama hapana ni kwanini wamewekwa? Je, ukongwe wa chama ni sababu ya yoyote yule kuvikwa uzoefu ili mradi tu anatoka chama husika?
9. Je, Mtu au taasisi inazaliwa na UZOEFU? Kama hapana, kwa nini hatuwi na watu au taasisi hizo hizo milele? Wengine wanaingiaji? Lazima kuna mwanzo Fulani. Je, UZOEFU ni sawa na kibao cha kukopa kesho ambacho kila siku kinasomeka hivyo hivyo na kila siku kumzuia mtu kukopa?
10. Mambo ya Msingi ya uongozi-sifa za asili za uongozi zinahitaji UZOEFU, mathalani UADILIFU, KUCHUKIA UFISADI? Je, yanahitaji uzoefu wa asili au uzoefu wa miaka?
11. Je, ni bora aliye muaminifu katika mambo madogo hastahili kupewa mambo makubwa ?(UZOEFU BORA KATIKA MAMBO YA NJE YA UTAWALA MATHALANI KUENDESHA VIZURI CHA CHA SIASA)
Haya ni maswali ya kuchokoza mjadala. Mengine yanajichanganya yenyewe kwa yenyewe. Ni chakula cha fikra tu(food for thought).
Nitachangia rasmi mada hii baada ya kusikiliza mahojiano ya Zitto.
Natabaruku
JJ
Ndugu yangu kwanza soma kisha elewa, halafu ndio ukimbilie keyboard, Kwanza kumbuka Mwl. Nyerere alikuwa akipigania uhuru, na alianza ku mobilize watu kuanzia ngazi ya mjumbe wa nyumba 10 na ndio maana aliweza kukubalika na kujulikana kwa urahisi. na hatimaye kufanikiwa.Son of a Dead Millionare,
ndugu yangu unapotosha hapa kidogo.. ni maoni yako lakini bob hata siwezi kuamini kama sii propaganda.
Kwa nini chama cha Upizani kisiweze kutawala ikiwa Nyerere ambaye hakuwahi kutawala hata kijiji zaidi ya kuwa mwalimu wa shule aliweza kutawala nchi UPYA toka mikononi mwa mzungu. tena bila wasomi wala miundombinu ya uzalishaji. We had nothing!
Kutawala nchi ni sawa na kuwa mzazi, kila mtu husema fulani hawezi kulea lakini akisha oa na kuzaa maisha huwa tofauti na yale ya Usera!..
Kuna kila uwezekano wa CUF ama Chadema kuwa viongozi wazuri kuliko CCM. Kwa sababu hiyo ndiyo itakuwa challenge na nafasi pekee ktk maisha yao kupata Uongozi kisha CCM wana nguvu na sauti kama wapinzani wazuri kuliko wao.
Ushindani halisi utaanzia hapo na SODM, trust ukiwa nje ya Utawala mshikaji usiombe. Pia kama utapewa madaraka ku- prove kwamba makosa yaliyokuwa yakitokea ni ya viongozi basi utawala tamu ya utawala huanzia hapo.
kama unakumbuka Zitto alimtolea mfano Harper wa Canada, huyu jamaa chama chake hakijawahi kutawala nchi zaidi ya serikali ya jimbo lao Calgary. Miaka yote calgary ilikuwa tajiri lakini wananchi wake hawakupata kabisa chochote cha kujivunia lakini bado walikichagua chama hicho miaka nenda rudi.
jamaa kashika nchi sasa hivi, na mshikaji uchumi wa jimbo hilo una boom kiasi kwamba inatisha. Kila unayemsikia anakimbilia huko na sasa hivi hakuna hata nyumba za kutosha...
Kila mtu domo wazi pamoja na kwamba watu wengi hawakipendi chama hicho nahasa huyu bepari mkubwa Harper. lakini jamaa ndio analeta ajira na utajiri pamoja na kwamba msimamo wake kisiasa haupendwi na watu.
Chagua mwenyewe kusuka ama kunyoa!