WARAKA HUU UMETUMWA KWANGU NA THOMAS NGAWAIYA USOMENI
NA MWENYE MAONI JUU YA WARAKA HUU ATOE.
ITACHUKUWA MIAKA 100 KWA WAPINZANI WA TANZANIA KUELEWANA NA KUELEWEKA NDANI YA JAMII.
Muungano wao ni danganya toto.
Uchu wa madaraka wengi wameficha makucha yao
Hata wakiungana hawatazidi 5%, hivyo ni vigumu kupata ushindi.
Kuna mambo mengi sana yanayofanya Watanzania kujiuliza kuhusu viongozi wa upinzani Tanzania, moja ni juu ya ubinafsi wao;
Hakuna uongozi uliobora ndani ya vyama vyao. (mfano kupeana madaraka kifamilia, mfano mzuri CHADEMA).
Wapinzani wengine uhubiri ukabila mfano; siasa ya u-majimbo.
Hakuna amani ndani ya vyama hivyo. (hoja ya jino kwa jino)
Hawana uwezo wa kujenga uchumi wa nchi kwani kwa miaka 16 wamekuwa wakitegemea ruzuku ya serikali kwa kuendesha vyama hivyo.
Vyama vingine vinatumia udini jambo ambalo linahatarisha amani.
Hoja zote hizi ni kati ya maswali wanayojiuliza wananchi kuhusu kama kweli haya yatatukomboa kisiasa na kiuchumi Tanzania.?
Jibu ni hapana; Kwani ni vyama hivyo hivyo vinavyozungumzia umajimbo Tanzania na hivyo inamaanisha ukabila kwa kutaka kutugawa..
Ni vyama hivyo hivyo vinavyohubiri ubinafsi kwa kuamua kugombea nafasi za uongozi kila mara au uraisi kwa watu walewale bila kupisha wengine hata kama uwezo wao umechuja na kwa hali hiyo inaonyesha kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya upinzani. Wananchi wanajiuliza endapo hapana demokrasia ndani ya vyama hivyo ni vipi watajenga demokrasi baada ya kupewa madaraka ya nchi nzima?
Jambo jingine ni kuhusu kupanua na kujenga uchumi wa ndani ya nchi. Ili kupanua uchumi wa nchi utahitaji ubunifu wa hapa na pale. Vyama hivyo vimedumu kwa zaidi ya miaka 16 na hadi sasa vyama vyote hivi hutegemea ruzuku ya Serikali kwa kujiendesha kwani hakuna hata senti moja inayotokana na michango ya wanachama wao na wala miradi yeyote wananchi wanajiuliza ni vipi hapa napo vyama hivi vimeshindwa kujikwamua kiuchumi ndani yao na kutegemea ruzuku ya serikali muda wote je! Watajengaje uchumi wa nchi ikiwa wao kwao wameshindwa?
Tangu vyama hivyo vianzishwe viongozi huzua migogoro ya hapa na pale isiyokuwa na kichwa wala miguu, na kufukuzana kila kukicha na hivyo kufanya wananchi kujiuliza kama wangepewa nchi ingetawalika? Pia Watanzania wanaangalia migogoro mingine ilivyo ndani ya nchi nyingine za Afrika kama Somalia, Sudan, Kongo, Uganda, Kenya, Burundi nk. Na kulinganisha na amani iliyopo Tanzania. Ndio maana 95% ya wale waliokuwa upinzani wameamua kurudi kwenye chama tawala.
Kwa hali hii jamii ya watanzania wameona na kuamua kutounga mkono vyama hivi vya upinzani kwa kuwa hawana jipya na badala yake wanahubiri chuki tu ya kuyumbisha Taifa letu lenye amani na viongozi wenye busara .
Mwisho jamii inajiuliza juu ya viongozi waliopo kwenye upinzani kwani ni wale waliokuwa ndani ya CCM na kuchujwa kwa sababu ya kukosa sifa na wao wakaanzisha vyama hivyo kutokana na chuki binafsi na siyo kwa masilahi ya Watanzania kama walishindwa kuungana wakati wakiwa asilimia ishirini ni leo ambapo wamebakia asilimia tano ?
Hii ndio picha halisi tunayoona sisi Watanzania kuwa wapinzani hawana nafasi ndani ya nchi hii hadi baada ya miaka 100, yaani karne ijayo, ambapo kutakuwa na kizazi kipya na chenye mawazo na mtazamo mwingine.
Ningependa kuwahasa wapinzani kuwa badala ya kufikiria muungano wa unafiki ni vema kama wana mawazo mazuri wakayasema au kuyatenda sasa kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla na pia wajue kuwa chuki,ubinafsi,ukabila na udini kamwe havitaweza kujenga amani ya nchi wala kuleta maendeleo ya kiuchumi zaidi ya kuleta vita na mfarakano. Wananchi wa Tanzania tuepuke upinzani tujenge nchi yetu kwa amani na utulivu daima ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI.
Muungano huu nafananisha na wagonjwa wawili kuungana na kupata mmoja mwenye afya bila tiba.
Thomas Ngawaiya
Waraka huu umetumwa kwa bwana Mroki Mroki. Unaweza kusoma habari nyingine na picha kwenye blogu yake hapa:
Mroki Mroki