Kitila,
Kwenye elimu, afya na ustawi wa jamii chukua zangu 5...
Umesema kuwa Chadema:-
1. Mtasema kile ambacho mnataka kukifanya na ambacho mna uwezo nacho...
Nadhani wananchi wanadai kujua mbali na kusema kipi mtakifanya ambacho mtakuwa na uwezo nacho..How? ina maana mtaweza kweli kuwaambia wananchi kuwa Umeme hauwezi kupatikana kutokana na uwezo wetu mdogo ama?..
2. Pia hilo la kuweka misingi imara ya demokrasia ili wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha viongozi. Bila shaka misingi hii inatokana na hoja ya JK kuwaongopea wananchi!
Je, Unaweza kutupa baadhi ya proposal zenu za mfumo huu kutengua nguvu za rais wa nchi!...
Kisha ni sehemu zipi za katiba ambazo mnataka mabadiliko na yepi mapendekezo yenu? Na yalifanyiwa uchunguzi wa kitaalam (takwimu) kupata support ya wananchi walio wengi?
Naam Mkandara, nimerudi nilitoka kidogo. Haya ni maoni yangu kuhusu maswali yako hapo juu:
1) Ndugu yangu mimi hata mwanangu wa miaka minne huwa simdanganyi. Simuahidi kile kitu ambacho sitamfanyia maana najua nitakosa uaminifu wake kwangu. Sasa hata katika hili mimi nikiwa kiongozi sitaaidi mambo ambayo kwa hakika najua sitayafanya.
2) This a tall order question. Kwa maoni yangu kuna matatizo matatu makubwa kuhusu katiba yetu:
i) Mchakato wa uundwaji wa katiba haukushirikisha wananchi. Kumbuka katiba tuliyonayo ilitungwa kwa tume ya Msekwa kisha ikaenda kwa Mwalimu Nyerere. Kisha ikiapitishwa na NEC ya CCM, halafu ikaenda bungeni lililokaa maalimu kwa ajili ya kupitisha katiba (Constituent Assembly). Bunge lilikuwa na wajumbe 222. 101 kati ya hawa walikuwa wateule wa Rais! Kwa hiyo wananchi wa Tanzania hawajawahi kushiriki kutunga katiba yao. Katiba yeyote ya kidemokrasia utungwaji wake hushirikisha wananchi. Kwamba hatujawahi kushiriki kutunga katiba inaeleza ni kwa nini hatuijali-wote watawala na watawaliwa.
ii) Katiba iliyopo ilitungwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja na ilikuwa inakidhi mazingira haya. Tume ya Nyalali iliweka wazi kabisa bila kutengeneza katiba mpya mfumo wa vyama Tanzania utadorora maana Katiba iliyopo ina-support mazingira ya chama kimoja. Tume ya Nyalali ilisema pia haiwezekani kubadili tu katiba ya sasa ikaleta maana bila kuiandika upya kwa watawala na watawaliwa kushiriki kikamilifu.
iii) Ukiacha mchakato wa utungwaji wake, katiba ya sasa ina kasoro nyingi mno. Kwa mfano, huwezi kuamini nikikwambia kuwa katiba yetu haiongelei chochote kuhusu umilikaji wa raslimali asili ikiwemo ardhi, madini,n.k. Matokeo yake viongozi wetu ndio wenye maamuzi na mambo haya maziti ya nchi. Si ajabu basi tunashuhudia mikataba ya ajabu ajabu inayoambatana na uporwaji wa raslimali zetu, tangu enzi za Loliondo hadi sasa katika madini.
Pia gogoro la Zanzibar kwa kiasi kikubwa linachangiwa na mapungufu katika katiba yetu. Kwa mfano, badala ya serikali kutengeneza utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu nafasi ya Rais wa Zanzibar, wao na CCM yao wakijifungia wakamuengua Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais-which was a terrible mistake. Kisa, waliogopa kwamba Rais wa Zanzibar akitoka CUF itakuwaje! Hii inakuonesha jinsi ambavyo CCM wamejifungia katika box. Yaani hawezi kufikiria in a big picture, wao ni ccm kwanza, nchi baadaye! Matokeo yake ndio hivyo kwamba wazanzibar wanaona kabisa walikuwa cheated katika hili. Hata hatua ya mgombea wa urais kupitia ccm anapitishwa na NEC yenye wajumbe lundo kutoka bara ina matatizo makubwa. Ndio maana Rais wa sasa wa Zanzibar hana moral command ya kutosha zanzibar maana anajua alichaguliwa na wabara na kwamba wazanzibar ndani na nje ya ccm hawakumchagua!
haya ni maoni yangu ya haraka kabisa kuhusu swali lako kuhusu katiba.