Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #221
Ndiyo wamechoka, lakini hawajakata tamaa! Wamechoka kupambana na wezi wa fedha zetu na ambao wanaendelea kula kama mchwa! Ni lazima mtu uchoke.
Baada ya kupambana nao katika mahakama ya watu na katika uchaguzi ambao vijana wao walitiwa mapamba mbele ya macho ya CCM ikidaiwa ni "morani" lazima mtu achoke!
Anachoka mtu aliyefanya kazi; mtu mvivu hachoki! Jamaa hawa wameitumikia nchi yao kwa uthabiti na ujasiri mkubwa. Mrema alianza na sakata la Benki Kuu miaka 15 iliyopita leo hii historia inamlipizia kisasi chake; lazima achoke!
Kupambana na watu wenye nguvu kama kina Lowassa, RA, Chenge, JK, na timu yao nzima na kuweza kusimama kidete na kuitwa kila aina ya majina na kuweka kila aina ya mapingamizi usifanikiwe ni lazima mtu achoke!!
Mstahiki asante kwa posti hii kwani umethibitisha kuwa ndugu zetu hawa kweli "hawalali"! Maana wanaolala wanaonekana wakirukaruka na vyimbo za TOT kwani hawakosi usingizi kuhusu Buzwagi, Richmond, ATC, n.k !!
Na asante kwa kutuonesha hatimaye kwa ushahidi wa picha na maneno yako kwamba hawa jamaa wanahitaji kuungwa mkono ili wasikate tamaa! Sura zao siyo tu zinaonesha kuchoka bali pia zinaonesha kujali. Wanaonekana ni watu ambao wanatumia muda wao mwingi kuwaza kuwazua maslahi na mustakabali wa Taifa lao.
Sasa tukiwalinganisha hao na hawa:
Ni wazi kuwa "waliochoka" wanaokana wamefanya kazi.
Au ukiwalingisha hawa kina JK na kundi la "watatu" wenzangu tulipotaka kibaruani! Believe me, hata matabasamu yetu yanaonesha tumetoka kazini!!
Sasa to make the long story short..
Niko tayari saa yoyote, mahali popote, na wakati wowote nitakaomriwa kusimama na wale wote ambao wanakosa usingizi kwa kuiwazia nchi yao, wanaokesha usiku kucha kupanga na kupangua jinsi ya kupambana ufisadi, na wale wote ambao siyo tu wanacheka cheka kwa sababu ya kupigiwa makofi, bali wanasema ukweli hata kama hakuna mtu wa kuwashangilia!! yes sir! Binafsi napenda nihesabiwe miongoni mwa wale waliochoka kwa kazi ngumu wanayoifanya kwa ajili ya Taifa lao, lakini hawaweki manyanga au kususa kazi (kama alivyofanya mmojawapo hapo juu)!
Binafsi nimechoka na ufisadi, ubadhirifu, wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, mikataba mibovu, unyanyasaji wa kijinsi, mazingaombwe ya kisiasa, ubabe wa uongozi, uharamia wa pesa, unafiki wa washangiliao na kwa hakika nimechoka na wale wote ambao wanafikiri kuwa Tanzania ni mali yao na sisi wengine ni wapangaji!!! NA MIMI NIMECHOKA!! Count me in sir miongoni mwa wachokao, lakini wasiokata tamaa wala kusalimu amri!!!!