Je, wapo mafundi waaminifu?

Kila nikiwaza kujenga hofu yangu inaingia pale ninapofikiria mafundi watakavyonibia cement, nondo na material mengine. Je, ni kweli wapo mafundi ambao wanaweza kuwa waaminifu katika ujenzi.
Umasikini wako upo kwenye woga wako..!!
 
Kuwa na imani ndugu bado watu wema wapo. Nashukuru nimeshuhudia hili, mafundi waaminifu wapo.
 
mafundi wapo wahaminifu nimewai mfungia mtu mifumo ya umeme mtu samfahamu anifahamu nilionganishwa nae kwa simu siku anakuja alikuta kila tulichokubaliana kimefanyika usiwe bahiri
 
Kuna baba yangu mkubwa ni fundi ujenzi afu ni msabato na umri umesogea,ila naambiwa akirudi nyumban kutoka site lazima awe amebeba chochote kama sio bati basi misumari,na kama sio robo tatu ya mfuko wa cement basi gpysum powder mfuko mzima😂😂
 
Jichanganye eti fundi mwaminifu!! Mara unajenga kwa SIMU utafurahi.




KAZI ni kipimo cha UTU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…