Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Tanzania tubadili mfumo wa elimu uendane na mazingira ya sasa. Tuwekeze zaidi elimu kwa vitendo kuliko kukariri. Leo nikiwa mkoani Mwanza nimeenda shule flan kufuatilia tender , kwa bahati mbaya nikadondosha ATM kadi mmoja wa watoto wa kidato cha nne kaikota.
Baada ya kuitafuta nikisema nimepoteza ATM kadi yangu yule mwanafunzi alikuwa kimya ; wakati naondoka akanifuata akaniambia mzee kuna hiki kitu iliangushwa pale una kazi nacho?
Ilinilazimu nifanye naye mahojiano na kubaini hana uelewa kuhusu money transfer, uwepo wa benki na kazi zake wala matumizi ya ATM katika kupata huduma.
Ni jambo dogo kwa wengi lakini kwa wachambuzi linakueleza kwamba vipo vitu vy msingi vya watoto kufunzwa utotoni. Mfano
1. Umuhimu na utaratibu wakumiliki line ya simu na simu kwa ujumla
2. Historia ya uhifadhi wa fedha duniani kutoka watu wanahifadhi ndani, vikaja vitabu, zikaja ATM na sasa uwepo wa money transfers tofautitofauti
3. Huyu mtoto atalazimika kuwa NIDA, lazima from primary level mtoto afahamu umuhimu wa NIDA card, nani anapewa na kwa matumizi gani.
4. Watoto wanazaliwa kwenye familia zenye uwezo tofauti, lazima tuanze kuwafundisha watoto kuhusu mirathi na watu wanaostahili kupewa mirathi hii ni kutokana na umri vifo vya wazazi wakiwa wadogo kuwa vingi
5. Huduma za afya now days zinategemea bima na unapanda ngazi kwa ngazi kabla ya kufikishwa hospitali ya rufaa. Tunao watoto wanalea bibi na babu zao kama siyo wazazi. Hawa watoto wanapaswa kufahamu bima ya afya ni nini na matumizi yake. Wanapaswa kufahamu muundo wa huduma ya afya upoje na utaratibu wa kukata rufaa upoje! Haya ni mambo ambayo Ulaya wanafundishwa nakujionea toka nyumbani.
6. Kuna masuala ya nishati, kuna lishe nk
Mtoto mwenye maarifa kama haya hata akifeli masomo ya darasani atatoka na elimu ya kumsaidia kusihi Duniani. Lakini tunapolazimisha kuwafundisha watoto mambo yasiyo na applicability tukaacha haya madogo madogo ni madhara haya mtoto yupo kidato cha nne hata ATM haipo kwenye upeo wa nafsi yake. Na unaweza kumkuta kijana kama huyu wazazi wake ni wasomi waziri ila wameqaficha watoto taarifa na maarifa.