Tumeshuhudia wasanii wote wenye majina makubwa wasiopungua 200, wakishiriki kwa pamoja kwenye tamasha lililoandaliwa na CCM, katika uwanja wa Uhuru hapo jana, kwa kile kiliichoitwa tamasha kubwa kabisa la kimuziki, kwa wasanii hao wote wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wakubwa na wanaiunga mkono CCM katika uchaguzi mkuu ujao, unaotarajiwa kufanyika mwezi wa October mwaka huu.
Wengi wetu tutakuwa tunajua kuhusu hao wanaoitwa askari wa kukodiwa, au kwa jina lingine wanaitwa mamluki, ambao kwa lugha ya kiingereza wanaitwa "mercenaries" kwa tabia zao za kupenda pesa na wako tayari kwa atakayewapa pesa watakayoridhika nayo kupigana kwa yeyote, hata kama watafahamu kuwa hao wanaotakiwa kupigana nao ni ndugu zao wa kuzaliwa, ili mradi tu umewapa pesa watakayokubaliana nayo kwa ajili ya kazi hiyo!
Hiyo ndiye tabia ya "mercenaries" kuwa wapo tayari kupigana na adui yeyote, ilimradi yule aliyewakodi, atakuwa ameweka mezani "kibunda" ambacho wataridhika nacho.
Hiyo tabia ya "mercenaries" siwezi kuitofautisha na wasanii wetu waliojitokeza kwa wingi pale uwanja wa Uhuru ili kuwaunga mkono CCM, katika kuwakandamiza wazalendo ambao maisha yao yameathirika vibaya kutokana na utawala huu wa CCM wa miaka yote 60 baada ya Uhuru.
Tunajua kabisa tabia ya wasanii wa nchi yetu kuwa huwa hawaendi kwenye "show" yoyote kabla ya kuwekewa donge nono, ambalo wenyewe watakuwa wamekubaliana nalo, ndipo hapo wanapotokea kwenye onyesho hilo.
Hawa jamaa tunawajua kwa tabia yao kuwa hawana mapenzi na mtu, bali kinachopendwa ni pesa tu, ndiyo itakayoamua kuwa waende kwenye onyesho hilo au laa.
Kutokana na tabia hiyo ya wasanii wetu, kwa hiyo tunakuwa na uhakika kuwa CCM "imekamuliwa" pesa za kutisha ili kuwaleta kwa pamoja wasanii wakubwa wote tuliowaona jana.
Kwa upande wa ile "nyomi" iliyojazana pale katika uwanja wa Uhuru, hao CCM wasichukulie kuwa ule umati wote uliojazana pale kiwanjani, kuwa ni wafuasi wao na wenye ukereketwa wa kindakindaki wa chama chao cha CCM, bali ule umati ulijazana pale uwanjani kuja kuwashangaa kina Diamond na Ali Kiba katika show hiyo ya bure na wala sivyo watakavyokuwa wanachukulia viongozi waandamizi wa CCM kuwa ule umati wote ni mashabiki wao wa CCM!
YEYOTE ALIYEWEZESHA HII ' IDEA ' NAMPA HESHIMA YAKE
Magoiga SN
Rafiki yangu mmoja ambaye ni kijana wa upinzani amenifuata inbox akiwa na lengo la kuniambia kuwa wananchi wote waliohudhuria tamasha la CCM uwanja wa Taifa jana walienda kwa sababu ya wasanii na siyo CCM, kwahiyo nisishangilie uwanja kujaa
Nilichomjibu:
Ni kweli, wapo walikwenda pale kwasababu ya wasanii na wapo waliokwenda pale kwasababu ni tamasha linaloihusu CCM ndiyo maana uliona wengi wamevaa nguo za chama, lakini kitu cha muhimu cha kukumbuka ni kwamba tamasha la jana lilihusu uzinduzi wa nyimbo 500 za kampeni za CCM zilizoimbwa na wasanii zaidi ya 200 nchini.
Nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa ni nyimbo zinazoihusu CCM , Rais Magufuli na utekelezaji wa ahadi na ilani ya uchaguzi tu, hakukuwa na Bedroom ya harmonize wala money money ya 20 Percent, yaani kwa lugha rahisi sana ni kwamba wananchi kwa hiyari yao wenyewe walikaa uwanjani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa saba usiku wakisikiliza na kucheza nyimbo zinazoisifia CCM, kumpongeza Rais Magufuli na serikali anayoiongoza, what a milestone
Wasanii wote walipanda jukwaani wakiwa wamevalia mavazi au sehemu ya vazi yenye nembo ya CCM nk, wasanii waliwaimbisha watazamaji, kuwachezesha na kuwashirikisha ktk uimbaji wa nyimbo za CCM. Yaani kuanzia saa moja asubuhi mpaka usiku wa maneno neno CCM, neno Magufuli, neno utekelezaji wa miradi ya maendeleo, neno amani na utulivu yalikuwa yakijirudia kila baada ya sekunde kadhaa. Ukumbi mzima ulitapakaa alama za CCM, rangi ya vazi la CCM, screen kubwa jukwaani haikukauka kauli mbiu za CCM, yaani ni sawa na kusema uwanja mzima influenced kwa kijani na njano kuanzia mazingira mpaka maudhui ya nyimbo zote
Kwa lugha nyingine ni kwamba, wananchi walikuwa wakicheza nyimbo ambazo ujumbe mkubwa ulihusu ubora na uimara wa CCMkaka chama cha siasa, Rais Magufuli kaka kiongozi makini na mafanikio makubwa yaliyopatikana ktk miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa
Watu wakiwa wanawasikiliza wasanii ambao wanawakubali na kuwapenda kuanzia saa moja asubuhi mpaka usiku wa manane wakiwa wanatumbuiza ujumbe wa aina moja kuhusu CCM, Rais Magufuli na miradi ya maendeleo iliyoelekezwa huku wakicheza na kufurahia ina faida kubwa sana ktk ushawishi na afya ya akili.
Mimi siyo mwanasaikolojia lakini wataalamu wa masuala ya 'marketing and branding' wanajua vyema hii mbinu, wataalamu wa masuala ya saikolojia wanajua vyema hiki kitu, kwahiyo ukweli ni kwamba hili tamasha la CCM kuzindua nyimbo za kampeni zilizoimbwa na asilimia 99 ya wasanii wote nchini siyo kitu kidogo
Akili ya kawaida ya kibinadamu inapenda kuunga mkono upande ambao unaonekana kuwa smart, upande ambao hata wale unaowapenda na kuwaamini wanauunga mkono, upande ambao una uhakika na kile ambacho unaakifanya.
Ndiyo maana hata ambao hawakuweza kufika uwanjani walikaa kwenye TV zao kufuatilia nini kinafanyika uwanja wa uhuru, ninachoweza kusema ni kwamba tamasha hili limefuatiliwa na watu wengi sana bila kujali itikadi zao, na nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa jukwaani ni nyimbo za CCM, na bado waliendelea kufurahia.
Aliyewaza na kusimamia utekelezaji wa hiki kitu (hii idea) nampa heshima yake, kama ni wewe Ndugu Hamphrey Polepole BIG UP sana.
Sasa chama kitazame namna ya kuifanya hii idea iwe ya kila mwaka, angalau mara moja kwa mwaka wasanii wawe wanafanya kitu kama hiki, kama mwaka huu kinefanyika Dar es Salaam, mwaka kesho inaweza kufanyika Mtwara, au Mwanza au Arusha nk nk, burudani ni tiba, na burudani ya nyimbo za CCM ni tiba ya uzalendo.
Magoiga SN