Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio wasanii tu hata sisi humu tunaogopa vitisho vya ccm na ndiyo maana tunajificha humu JF na kuishia kuwakaripia hao ccm tukiwa nyuma ya keyboard ila tunataka wasanii wasiogope vitisho vya ccm kwenye maisha halisi.Ukitaka kujua namna ambavyo CCM inavyowatisha wasanii, hebu rejea tukio la msanii Roma, la kutekwa lililomkuta mwanzoni mwa mwaka 2017
Kama muziki tu ambao ni burudani tunataka wasanii wasiende kufanya show zilizoandaliwa na ccm,kwa hali hiyo basi hadi madkatari wataacha kutibu wagonjwa wa ccm na wengine hawatawauzia chakula ccm.Ni kweli tunafahamu jinsi wasanii wetu walivyo pigika sana baada ya tasnia ya music na filamu kuyumba na kwa hiyo ni rahisi mtu dhaifu akiwa na njaa kukubali lolote hata kama moyoni halipendi mradi apate pesa ingawa wachache wanaojitambua wanaweza kukataa kutumika.
Kibaya ni kuwa wana angalia maslahi ya siku moja na yanayo wahusu wao bila kutazama maisha ya watanzania kwa ujumla wakiwemo babu zao, bibi zao, kaka zao, dada zao, wadogo zao, watoto wao, jirani zao nk ni kwa vipi wanaendesha maisha yao katika umaskini mkubwa. Wanatumika kwa msimu wa uchaguzi tu na baadaye kurudi kuishi maisha yale yale ya tabu na ndugu zao kwa miaka mingine mitano. Mtu anaweza kulinganisha na ile karatasi nyeupe nyepesi inavyotumika kusafisha na baadaye maji hutumika kuisafirisha mpaka kunako hitajika.
UHURU JRSio wasanii tu hata sisi humu tunaogopa vitisho vya ccm na ndiyo maana tunajificha humu JF na kuishia kuwakaripia hao ccm tukiwa nyuma ya keyboard ila tunataka wasanii wasiogope vitisho vya ccm kwenye maisha halisi.
cha bure,pili watz ndo watu unaowezawapata popote na mda wowote uutakaohasa ukiwawekea muziki watajaa kwa sababu wengi ni majoblessKama bado kuna wananchi ambao wameacha shughuli zao zote na kwenda kuangalia burudani ya muziki iliyoandaliwa na ccm basi kuna tatizo kwa hao wananchi wenyewe na hao wasanii si tatizo wao bali wapo kazini.
Wanamziki 200 kuimba nyimbo za kusifu chama lazima mtu apate wasiwasi lakini kama kuna maslahi ni powaa tu kwani siku ya kupiga kura ni siri ya mtu mwenyewe as anaweza kusifu kwenye public lakini akafanya mengine kwenye chumba cha kupigia kura.Kama muziki tu ambao ni burudani tunataka wasanii wasiende kufanya show zilizoandaliwa na ccm,kwa hali hiyo basi hadi madkatari wataacha kutibu wagonjwa wa ccm na wengine hawatawauzia chakula ccm.
Ulichoongea ndiyo ukweli mtupu kwa asilimia 100Wanamziki 200 kuimba nyimbo za kusifu chama lazima mtu apate wasiwasi lakini kama kuna maslahi ni powaa tu kwani siku ya kupiga kura ni siri ya mtu mwenyewe as anaweza kusifu kwenye public lakini akafanya mengine kwenye chumba cha kupigia kura.
Mtaje aliepaform kwa chadema na ccm 2015, otherwise huna tofauti na wapiga mitamaHakuna ushahidi wowote; mwaka 2015 waliperform kwa CHADEMA na kwa CCM. Wanajua kabisa jinsi ya kumtumikia kafiri wapate mradi wao.
Asante kwa kuniita mwomgo.
Ni kawaida tu hasa ukizingatia wasanii wetu wengi walitangaza nia hukohuko ccm.Wanamziki 200 kuimba nyimbo za kusifu chama lazima mtu apate wasiwasi lakini kama kuna maslahi ni powaa tu kwani siku ya kupiga kura ni siri ya mtu mwenyewe as anaweza kusifu kwenye public lakini akafanya mengine kwenye chumba cha kupigia kura.
Sasa kwa hali hiyo msanii analaumiwa nini kuwa et anatumika na ccm wakati wananchi ndio wako hivyo hawana shida na ccm wao ukiwaekea muziki wanaburudika tu bila kujali.cha bure,pili watz ndo watu unaowezawapata popote na mda wowote uutakaohasa ukiwawekea muziki watajaa kwa sababu wengi ni majobless
Mh..Tanzania gani unayoiongelea mkuu?Haijawahi tokea msanii yeyeto akaisapoti ccm na asife kimuziki sijui kuna laana gani
Una akili timamu au ni bangi zinaongea; ulikuwapo kwenye ufunguzi wa kampeini za UKAWA wewe? Huyo hapo ni nani, siyo msanii?Mtaje aliepaform kwa chadema na ccm 2015, otherwise huna tofauti na wapiga mitama
Wakati wa uchaguzi mkuu ndiyo wa mavuno kwa wasaniiTumeshuhudia wasanii wote wenye majina makubwa wasiopungua 200, wakishiriki kwa pamoja kwenye tamasha lililoandaliwa na CCM, katika uwanja wa Uhuru hapo jana, kwa kile kiliichoitwa tamasha kubwa kabisa la kimuziki, kwa wasanii hao wote wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wakubwa na wanaiunga mkono CCM katika uchaguzi mkuu ujao, unaotarajiwa kufanyika mwezi wa October mwaka huu.
Wengi wetu tutakuwa tunajua kuhusu hao wanaoitwa askari wa kukodiwa, au kwa jina lingine wanaitwa mamluki, ambao kwa lugha ya kiingereza wanaitwa "mercenaries" kwa tabia zao za kupenda pesa na wako tayari kwa atakayewapa pesa watakayoridhika nayo kupigana kwa yeyote, hata kama watafahamu kuwa hao wanaotakiwa kupigana nao ni ndugu zao wa kuzaliwa, ili mradi tu umewapa pesa watakayokubaliana nayo kwa ajili ya kazi hiyo!
Hiyo ndiye tabia ya "mercenaries" kuwa wapo tayari kupigana na adui yeyote, ilimradi yule aliyewakodi, atakuwa ameweka mezani "kibunda" ambacho wataridhika nacho.
Hiyo tabia ya "mercenaries" siwezi kuitofautisha na wasanii wetu waliojitokeza kwa wingi pale uwanja wa Uhuru ili kuwaunga mkono CCM, katika kuwakandamiza wazalendo ambao maisha yao yameathirika vibaya kutokana na utawala huu wa CCM wa miaka yote 60 baada ya Uhuru.
Tunajua kabisa tabia ya wasanii wa nchi yetu kuwa huwa hawaendi kwenye "show" yoyote kabla ya kuwekewa donge nono, ambalo wenyewe watakuwa wamekubaliana nalo, ndipo hapo wanapotokea kwenye onyesho hilo.
Hawa jamaa tunawajua kwa tabia yao kuwa hawana mapenzi na mtu, bali kinachopendwa ni pesa tu, ndiyo itakayoamua kuwa waende kwenye onyesho hilo au laa.
Kutokana na tabia hiyo ya wasanii wetu, kwa hiyo tunakuwa na uhakika kuwa CCM "imekamuliwa" pesa za kutisha ili kuwaleta kwa pamoja wasanii wakubwa wote tuliowaona jana.
Kwa upande wa ile "nyomi" iliyojazana pale katika uwanja wa Uhuru, hao CCM wasichukulie kuwa ule umati wote uliojazana pale kiwanjani, kuwa ni wafuasi wao na wenye ukereketwa wa kindakindaki wa chama chao cha CCM, bali ule umati ulijazana pale uwanjani kuja kuwashangaa kina Diamond na Ali Kiba katika show hiyo ya bure na wala sivyo watakavyokuwa wanachukulia viongozi waandamizi wa CCM kuwa ule umati wote ni mashabiki wao wa CCM!