Je Watanzania Huwa Na Nyimbo Za Kikabila Zinazosifika?

What a poor research,
Mimi natokea Iringa, Naona jinsi huijui Tanzania.
Umekuwa ni wa Kawaida sana kaka.
 
Kila siku nagombana na Wakikuyu wakikutana wawili hata wakiwa group la watu kumi wasio Wakikuyu hu-switch to Kikuyu bila aibu.
 

Hamna sehemu nilitaja kwamba nimehama mada, nilitumia neno 'point', na tangia hapo mwanzo hamna sehemu nilikana kwamba makabila yenu ya ndani hayana nyimbo za kitamaduni. Kauli yangu ni kwamba, kabila na jamii zote dunia hii zina mambo na tamaduni zao za asili. Lakini nyie mlichokifanya ni kutelekeza na kuona wanaozidumisha kuwa washamba na eti wanaotumia kingereza mnawaona watumwa. Mumekomaa kwenye kulazimisha kila mtu atumie Kiswahili muda wote.

Asili ya mtu huanza na lugha, pale anapozaliwa na kukuta watu wa kwao wanaongea lugha fulani, halafu wakati anakua, anaanza kujifunza tabia, mila na desturi za kwao. Akifikia umri wa kutengamana na watu wa nje ndio anakumbana na desturi za wengine, hatimaye anajitambua kwamba yupo ndani ya taifa lenye watu wa aina tofauti na mila zao tofauti lakini wameletwa pamoja kwa kutumia utaifa.

Hivyo anakumbatia huo utaifa, ila siku zote anafaa akumbuke ana asili ya alikotoka kwa babu zake, kabila lake, lugha yake ya asili, vyote hivyo lazima aviheshimu na kuvitunza. Kadiri anavyosafiri anapata kutambua mambo mengine mengi nje ya taifa lake, anaanza kujua kwamba kijiji chake, kipo ndani ya wilaya ambayo ipo ndani ya mkoa ambao upo ndani ya nchi ambayo ipo ndani ya bara ambalo lipo ndani ya dunia ambayo ipo ndani ya sayari n.k. Hawezi akaishia kwenye kutambua moja na kujifungia humo, lazima awe na uelewa wa jinsi anavyohusiana na maumbile ya sayari hii.

Sisi Kenya tunajivunia asili zetu, tatizo mlishakaririshwa na Nyerere kwamba mtu kujivunia asili yake ni ukabila. Nimesema mara sio haba humu kwamba ubaguzi ni tabia za mtu binafsi na hausababishwi na kabila. Nimewapa mfano wa Somalia ambapo wanaongea lugha moja na dini moja lakini ubaguzi kwa kwenda mbele. Hata kwenu hapo nmewahi kuona ubaguzi wa kidini wa kikanda n.k. pamoja na kwamba huwa mnajinadi watu wasiokua na ubaguzi wowote.
Leo hii nenda pale Zanzibar, wakiwa kwenye mfungo halafu uthubutu kuonekana ukila chochote, juzi kuna jamaa yangu hapo aliniambia mapolisi waliingia sehemu ya chakula na kutwaa vyote, waliwakuta watu wanakula mchana, wakiwemo waliotokea Tanzania bara wasiokua waislamu, na watalii wachache eneo linaitwa CCM, walivuruga amani na kutwa chakula chote. Huo ni ubaguzi maana unamlazimisha mtu aendane na imani yako.
Jana humu JF tuliona Dar es Salaam wafuasi wa kanisa katoliki wamezuiwa kwamba wasiingie kwenye desturi yao ya kuandamana kuadhimisha Eukaristi, kisa mwezi wa mfungo na watakinzana na wenzao.

Kenya tuna matatizo ya kikabila, ila utapata tunabaguana pale likija suala la kisiasa katika upigaji kura, lakini sio kwenye maisha ya kawaida. Mkikuyu na Mjaluo wanauziana kwenye maduka na kuishi pamoja bila matatizo, tunatumia lugha ya taifa Kiswahili, na lugha ya biashara Kingereza, lakini nikiwa na Mkikuyu mwenzangu haja gani niongee Kiswahili wakati tuna lugha yetu ya asili. Kiswahili ni pale kuna mtu hatuendani naye kwenye mazungumzo. Siasa za wanasiasa ndio huwa zinatuharibia, ila tunajivunia tamaduni na desturi zetu, umoja wetu.
Wakenya tunaongea lugha nyingi sana na wanasayansi wamebaini uwezo wa kuongea lugha nyingi unaboresha mtu hata kimawazo, hivyo tunahamasisha watoto wetu waweze kuongea lugha nyingi tu, mfano hai upo kwenye wanangu mimi, binafsi mimi Mkikuyu lakini mke wangu Mluhya, nimejitahidi kuhakikisha watoto wangu wanaongea lugha zetu mbili za asili, wanajua babu zao, desturi na asili ya kwetu. Wakiwa mjini wanaongea Kiswahili na Kingereza, japo pia wanafunzwa Kifaransa shuleni, na mara moja moja naongea nao kilugha na kuwafundisha nyimbo zetu za asili kwa lugha zetu.

Mimi hapa bnafsi nimejifunza lugha nyingi sana zikiwemo kadhaa za kwenu. Halafu hamna cha utumwa kwa mtu kujivunia uwezo wa kuongea Kingereza, hiyo ni lugha ya dunia na imeunganisha mataifa mengi sana na inatumika sana kitaalam, hivyo kujifunza hadi unaweza kuiogea, ni jambo la kujivunia na siwezi kujutia hata siku moja. Kingereza kimenisaidia sana kwenye taaluma yangu pale ambapo Kiswahili kilishindwa pakubwa, hivyo nina sababu nyingi za kukipenda na kujivunia pale ninakitumia bila matatizo.
Ttatizo lenu mna dhana ya sizitaki mbichi.....
 

Wewe umetiririka insha, ila sijui nikujibu nini maana unazunguka zunguka bila kueleweka pa kutokea. Fahamu kwamba Kenya tunajivunia Kiswahili maana pia ni ukweli kwamba kilibuniwa kwenye Pwani zetu. Tumehusika katika kukipigia debe kwa majirani zetu Wahabeshi, Somalia, Sudan zote mbili na hata Uganda na DRC na Afrika na duniani kote.

Hivyo hayo yote unavyobwabwaja sijui tatizo nini, kwa kifupi ni kwamba sisi hatujaghubikwa kwenye lugha moja, tuna uwezo wa kuongea lugha nyingi na ndio desturi yetu. Tumedumisha asili yetu na tamaduni zetu na tunazipokeza kwa watoto wetu, hatupo radhi kuishi maisha ya kizombi ya kujua lugha moja tu basi, na hata lugha yenyewe unakuta wachache ndio wanaifahamu na kuitumia ipasavyo.
 

Hii ndio nini, kwani watu kudai haki ya kuvaa watakavyo tatizo liko wapi, wewe hapo hiyo suruali uliyovaa hivi una taarifa mababu zetu Afrika hawakuvaa suruali??
 
Sijabwabwaja Mzee, nimekupa somo kubwa sana hapo, kufupisha na kuhitimisha ni kwamba hata mkomae na vilugha vyenu, kisheng kiingereza, hamtoweza kukizuia kiswahili kukuwa na kutawala ukanda wetu hadi Africa nzima.
Utaita ni utumwa or whatever, but you will not avoid Swahili.
And Swahili haikuzaliwa pwani yenu, mnapenda sana kujimilikisha, Swahili imezaliwa pwani ya Africa mashariki.
 

Kwani Pwani yetu sio ya Afrika Mashariki, nenda kapate tena somo la jiografia, pili naomba ufahamu kwamba hamna siku tumethubutu kuzuia Kiswahili, tumegoma kuruhusu kutekwa nacho na kuwa kama mazombi.
Lugha zetu za asili ndio lugha za kwanza, maana zinatuunganisha na mababu zetu, zinatupea asili na utambulisho wa kule tunakotokea, lugha zingine za kukuja tunazipokea na kuzikuza lakini haitowahitokea kwetu sisi tutelekeze lugha za asili.

Kiswahili kimebuniwa kwenye Pwani zetu na kilitukuta tukiwa na lugha zetu, mila zetu, asili yetu. Babu zetu walikua na tamaduni zao kabla Mwarabu hajaja na kuvuruga kwa ushirikiano wa mzungu. Leo hii Mnyamwezi au Mhehe unavaa milegezo hapo Dar na kukana asili yako eti wewe Mswahili, mfanye nyie lakini sisi tutaendelea kudumisha na kuzitunza lugha zetu.

Wakenya tumehusika pakubwa katika kufanikisha usambazaji wa Kiswahili, hivyo hamna sehemu tumekiponda au kukizuia, kinazagaa kwajili ya juhudi zetu. Lakini hakitatumeza tuishi kama mazombi yasiokua na asili.
 
Hii ndio nini, kwani watu kudai haki ya kuvaa watakavyo tatizo liko wapi, wewe hapo hiyo suruali uliyovaa hivi una taarifa mababu zetu Afrika hawakuvaa suruali??
enheeee nilijua tu utasema hilo! Na hapo ndo pengine bado hujaelewa! Yawezekana kweli suruali hizi mababu hawakuanza nazo hapo awali! Lakini hebu jiulize, ilikuwaje sisi tukazivaa!

Najua utasema zililetwa na wazungu, tuseme ndio, lakini ukweli ni kuwa jamii ndo ilizihitaji kwanza halafu ndio zikavaliwa! Wala wazungu hawakutulazimisha kuzivaa, na tena enzi za utumwa bado walitaka babu zetu waendelee kujifunga ngozi!

Ilifikia sehemu utamaduni wenyewe ukahitaji kuwa na vazi hilo, na jamii ikalitumia bila shida yoyote!


Wanachokidai hao ndugu zako ni kitu ambacho jamii haikihitaji! Kwa kisingizio cha utandawazi[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] Halafu na wewe huoni shida katika hilo huku ukiendelea kujisifu kuwa unadumisha tamaduni zako!

Sasa utadumishaje tamaduni ambazo jamii haizihitaji?
 
Watanzania wengi wanazungumza Kiswahili kuliko makabila yao.


Sababu tumeshazitoa nyingi sana, Sisi hatutaki kwenye mkusanyiko wa watu uzungumze kitu ambacho wengine hawaelewi, hapo ni kama mnawateta wenzenu au basi mazungumzo yenu yanakuwa kelele kwa wenzenu!


Ndo maana kwenye mkusanyiko ambao hatuna uhakika kuwa watu wote waliopo pale ni wa kabila moja, ni vyema kutumia kiswahili ambacho watu wote wanaelewa!
 
Ati lugha ya kwanza inawaunganisha na mababu zenu, ha haa, mababu wanakufa wameshakufa, wa kazi gani, au mnatambika, lazima wa Kikuyu mtakuwa mnatambika.
Sikiliza buda,hata Yesu alisema, wacha wafu wazike wafu wenzao, akasema tena, cha kwanza kitakuwa cha mwisho.
So I can say that you conservatives are holding on to that which is about to die by being engulfed with Swahili.
Hold on while it last
 

Watu tunadumisha tamaduni zetu na asili zetu ila kwa hiari sio kwa shuruti, hao akina dada wanataka haki ya kuvaa watakavyo maana miili ni yao na haituhusu. Hivi unajua tamaduni haslisi za Kiafrika wanawake walivaa vipi, bora hata hizo mini-skirts.
Hadi leo kuna jamii ambazo hayo mambo ni ya kawaida, agalia hii picha

 
Ndo muache sasa kujisifu maana hao wasichana walikuwa wanadai zinazoitwa haki zao huko kenya! Utamaduni wenu umebakwa huko!


BTW hiyo picha ya SA naona imekukaa
 
mbna si tunaimba singeli segere ndo nyimbo za jadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…