Sikusema umehama mada, nilisema umeacha point ya awali ya mikoa ya katikati mwa Tanzania kutokuwa na nyimbo za asili, ndo nikawa nasubiri utaje hiyo mikoa ili nikuonyeshe utamaduni wao maana kwa hali kusafiri tu kawaida sio rahisi kujua mambo ya ndani kama haya!
Kuhusu suala la kuksanya nyimbo za makabila tofauti kutoonyesha kuwa nadumisha asili yangu kama unavyodai!
Labda nikueleze hivi, ukiongelea asili unagusa nyanja nyingi! Kuna asili ya kabila, nchi na pia rangi/races. Sasa ukiongea kuwa tumemezwa hatuna asili, unamaanisha asili ipi?
Asili ya kabila utakuta kila kabila lina utamaduni wao unaowatambulisha na kuwatofautisha na kabila jingine japo baadhi ya mambo yanaweza kufanana kati ya kabila moja na jingine! Hapa ndo utakuta lugha, mavazi, chakula, nyimbo, imani nk!
Asili ya nchi mara nyingi huwa na mambo machache kama lugha,(ambapo Tanzania kama taifa asili ya lugha yetu ni kiswahili), mavazi nk!
Asili ya rangi inaeleweka sina haja ya kueleza sana! Sasa wewe unapong'aka kuwa wengi wetu wamemezwa sijui unataka uambiweje uelewe? Kuhusu watu wanaoishi mjini nimeshafafanua sana kwa nini kiswahili kinachukua nafasi kubwa, sina haja ya kurudia! Lakini bado wazazi wanaporudi kwenye majumbani hujitahidi kuwafundisha watoto lugha za asili!
Kwa wale wazazi ambao wameoana wakiwa ni kutoka kabila mbili tofauti ambazo hazielewani, watoto wao hujikuta wanatakiwa kuelewa lugha zote mbili, ya baba na mama ili wakienda kusalim wazee kijijini isiwe shida kuwasiliana! Mfano kama baba Mpare na mama mhehe basi baba atajitahidi watoto waelewe kipare huku mama akijitahidi waelewe kihehe! Kiswahili hicho ni automatic! Kama wazazi wote ni kabila moja kazi huwa ndogo zaidi! Hivyo ndivyo tz ilivyo!
Kwa mantiki hiyo hiyo hoja uliyopandikizwa kichwani kuwa lugha za asili zinachukiwa ni uongo mliouanzisha hapo Kenya ili muendelee kujionuesha kuwa mko juu baada ya kuona speed yetu inawatia tumbo joto! Hivi bila hata aibu unaweza kusema mbele za watu kuwa tunachukia lugha zetu? Mambo mengine uwe unafikiria kwanza kabla hujasema!
Pia umesema eti kuna miji mingine unakuta wapo watu wengi wa kabila moja lakini hawaongei kilugha! Labda nikuulize kuwa ni mji gani huo? Utaje, maana mpaka ukasema umeshauona, hebu useme tukupe majibu hapa!
Suala la kuwa tunaona wanaoongea kiingereza kuwa ni watumwa!
Sio kweli kuwa huwa tunasema kuwa wanaoongea kiingereza ni watumwa, La hasha! Maana hata sisi tunakiongea!
Ambacho huwa tunasema ni kuwa wanaoona kuwa kiingereza ndo kila kitu kuliko lugha zote, na kujivunia kiingereza hicho huku sio asili yao hao ndo watumwa! Na hili linawahusu ninyi wakenya, huwa mnajisifia sana lugha hiyo na kuipa kipaumbele kuliko vitu vyote, huo ndo utumwa tunaousema! Na kwa hili hamtaukwepa utumwa hadi hapo akili zenu zitakapobadilika na kuona kiingereza na kijaluo ni lugha sawa, tofauti ni matumizi tu!
Ziko nchi nyingi sana Africa ambazo zinaongea kiingereza lakini hawajivuni kama ninyi hapo Kenya! Angalia SA, wao wanajivunia Kizulu au Hoxha kuliko kiingereza, lakini wanaongea kiingereza ili kuwaunganisha! Uganda wanaongea kiingereza bora kabisa hapa Africa kuliko nchi yoyote, lakini hawajivuni kama ninyi! Wao wanajivunia kiganda zaidi na lugha nyingine! Kiingereza huwaunganisha tu! Angalia hata Nigeria, Igbo, Hausa na Yoruba zinathaminiwa kuliko kiingereza, na hawajivunii kiingereza kama ninyi mfanyavyo hapo utumwani Kenya!
Huo uzi ngoja nikufuate huko maana unataka kufanya mawazo ya mtu mmoja yawe mawazo ya taifa lenye watu 50+m
Hamna sehemu nilitaja kwamba nimehama mada, nilitumia neno 'point', na tangia hapo mwanzo hamna sehemu nilikana kwamba makabila yenu ya ndani hayana nyimbo za kitamaduni. Kauli yangu ni kwamba, kabila na jamii zote dunia hii zina mambo na tamaduni zao za asili. Lakini nyie mlichokifanya ni kutelekeza na kuona wanaozidumisha kuwa washamba na eti wanaotumia kingereza mnawaona watumwa. Mumekomaa kwenye kulazimisha kila mtu atumie Kiswahili muda wote.
Asili ya mtu huanza na lugha, pale anapozaliwa na kukuta watu wa kwao wanaongea lugha fulani, halafu wakati anakua, anaanza kujifunza tabia, mila na desturi za kwao. Akifikia umri wa kutengamana na watu wa nje ndio anakumbana na desturi za wengine, hatimaye anajitambua kwamba yupo ndani ya taifa lenye watu wa aina tofauti na mila zao tofauti lakini wameletwa pamoja kwa kutumia utaifa.
Hivyo anakumbatia huo utaifa, ila siku zote anafaa akumbuke ana asili ya alikotoka kwa babu zake, kabila lake, lugha yake ya asili, vyote hivyo lazima aviheshimu na kuvitunza. Kadiri anavyosafiri anapata kutambua mambo mengine mengi nje ya taifa lake, anaanza kujua kwamba kijiji chake, kipo ndani ya wilaya ambayo ipo ndani ya mkoa ambao upo ndani ya nchi ambayo ipo ndani ya bara ambalo lipo ndani ya dunia ambayo ipo ndani ya sayari n.k. Hawezi akaishia kwenye kutambua moja na kujifungia humo, lazima awe na uelewa wa jinsi anavyohusiana na maumbile ya sayari hii.
Sisi Kenya tunajivunia asili zetu, tatizo mlishakaririshwa na Nyerere kwamba mtu kujivunia asili yake ni ukabila. Nimesema mara sio haba humu kwamba ubaguzi ni tabia za mtu binafsi na hausababishwi na kabila. Nimewapa mfano wa Somalia ambapo wanaongea lugha moja na dini moja lakini ubaguzi kwa kwenda mbele. Hata kwenu hapo nmewahi kuona ubaguzi wa kidini wa kikanda n.k. pamoja na kwamba huwa mnajinadi watu wasiokua na ubaguzi wowote.
Leo hii nenda pale Zanzibar, wakiwa kwenye mfungo halafu uthubutu kuonekana ukila chochote, juzi kuna jamaa yangu hapo aliniambia mapolisi waliingia sehemu ya chakula na kutwaa vyote, waliwakuta watu wanakula mchana, wakiwemo waliotokea Tanzania bara wasiokua waislamu, na watalii wachache eneo linaitwa CCM, walivuruga amani na kutwa chakula chote. Huo ni ubaguzi maana unamlazimisha mtu aendane na imani yako.
Jana humu JF tuliona Dar es Salaam wafuasi wa kanisa katoliki wamezuiwa kwamba wasiingie kwenye desturi yao ya kuandamana kuadhimisha Eukaristi, kisa mwezi wa mfungo na watakinzana na wenzao.
Kenya tuna matatizo ya kikabila, ila utapata tunabaguana pale likija suala la kisiasa katika upigaji kura, lakini sio kwenye maisha ya kawaida. Mkikuyu na Mjaluo wanauziana kwenye maduka na kuishi pamoja bila matatizo, tunatumia lugha ya taifa Kiswahili, na lugha ya biashara Kingereza, lakini nikiwa na Mkikuyu mwenzangu haja gani niongee Kiswahili wakati tuna lugha yetu ya asili. Kiswahili ni pale kuna mtu hatuendani naye kwenye mazungumzo. Siasa za wanasiasa ndio huwa zinatuharibia, ila tunajivunia tamaduni na desturi zetu, umoja wetu.
Wakenya tunaongea lugha nyingi sana na wanasayansi wamebaini uwezo wa kuongea lugha nyingi unaboresha mtu hata kimawazo, hivyo tunahamasisha watoto wetu waweze kuongea lugha nyingi tu, mfano hai upo kwenye wanangu mimi, binafsi mimi Mkikuyu lakini mke wangu Mluhya, nimejitahidi kuhakikisha watoto wangu wanaongea lugha zetu mbili za asili, wanajua babu zao, desturi na asili ya kwetu. Wakiwa mjini wanaongea Kiswahili na Kingereza, japo pia wanafunzwa Kifaransa shuleni, na mara moja moja naongea nao kilugha na kuwafundisha nyimbo zetu za asili kwa lugha zetu.
Mimi hapa bnafsi nimejifunza lugha nyingi sana zikiwemo kadhaa za kwenu. Halafu hamna cha utumwa kwa mtu kujivunia uwezo wa kuongea Kingereza, hiyo ni lugha ya dunia na imeunganisha mataifa mengi sana na inatumika sana kitaalam, hivyo kujifunza hadi unaweza kuiogea, ni jambo la kujivunia na siwezi kujutia hata siku moja. Kingereza kimenisaidia sana kwenye taaluma yangu pale ambapo Kiswahili kilishindwa pakubwa, hivyo nina sababu nyingi za kukipenda na kujivunia pale ninakitumia bila matatizo.
Ttatizo lenu mna dhana ya sizitaki mbichi.....