Je, Watanzania tumekubali na kuridhia Deusdedith Soka kupotezwa mazima?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Leo tunakwenda almost mwezi wa saba, kijana Deusdedith Soka ma wenzie wamepotezwa. Umma ulipiga kelele mwanzoni, leo umekaa kimya.

Chama chake nacho kimejikalia kimya, hakihangaiki tena na kijana wao, kada wao. Hakuna wa kumsemea!

Kijana jasiri, mzalendo na mpenda nchi yake, nuru yake imezimwa hivihivi. Je walionyakua nuru hii wanajionaje, wanajisikiaje?. Je ni madaraka tu na kiburi chake?

Hawa madhalimu waliomtenda huyu kijana na wenzie je wataishi milele?. Udhalimu wao utawapa afya zaidi?.Utawapa furaha zaidi?.

Soka alinyakuliwa kama mwewe anyakuavyo vifaranga, na wengine wengi wamenyakuliwa. Inauma, inasikitisha, lakini hao madhalimu watajibu mbele ya Muumba mbingu na nchi!

Soma kuhusu maagizo ya Mahakama kwa Serikali: Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea
 
Yule afande aliempigia simu siku ya mwisho amepandishwa cheo sasa yuko Dodoma.
 
Leo tunakwenda almost mwezi wa saba, kijana Deusdedith Soka ma wenzie wamepotezwa. Umma ulipiga kelele mwanzoni, leo umekaa kimya.

Chama chake nacho kimejikalia kimya, hakihangaiki tena na kijana wao, kada wao. Hakuna wa kumsemea!

Kijana jasiri, mzalendo na mpenda nchi yake, nuru yake imezimwa hivihivi. Je walionyakua nuru hii wanajionaje, wanajisikiaje?. Je ni madaraka tu na kiburi chake?

Hawa madhalimu waliomtenda huyu kijana na wenzie je wataishi milele?. Udhalimu wao utawapa afya zaidi?.Utawapa furaha zaidi?.

Soka alinyakuliwa kama mwewe anyakuavyo vifaranga, na wengine wengi wamenyakuliwa. Inauma, inasikitisha, lakini hao madhalimu watajibu mbele ya Muumba mbingu na nchi!
Bosi wake Lissu yupo bize na kueneza utopia propaganda eti No Reform, No Election! Ahahahahaha!!
 
Naam, mpaka siku mbu atakapotua kwenye "PUMBU " until mosquito 🦟 lands on testes!! Namaanisha siku akipotea "ABDUL" ndo ubaya wa hili jambo utaonekana, na utakoma 🤔🤔🤔🤔
 
Amos Makalla kama ana utu azungumzie kuhusu suala la huyo bwana mdogo sio yale maigizo aliyofanya na yule mwanamke wa BAWACHA.
 
Chama chake nacho kimejikalia kimya, hakihangaiki tena na kijana wao, kada wao. Hakuna wa kumsemea!
Acha fix, Lissu na Heche na viongozi wengine naongea kila siku kuhusu mauaji, kutekwa kwa wana CDM wakati wa chaguzi na wengine kama kina soka waliopotea mikononi mwa wana dola.

Walio kimya kuhusu kupotea huko ni CCM, we ulishawahi kumsikia kiongozi wa CCM yeyote akilaani mauaji yoyote ama kupotea kwa watu tangu enzi za Ben 8 na Azory??
 
Back
Top Bottom