Je, Watanzania tumekubali na kuridhia Deusdedith Soka kupotezwa mazima?

Je, Watanzania tumekubali na kuridhia Deusdedith Soka kupotezwa mazima?

Kumbe unaelewa lakini unawatia hofu wanaotaka kuandamana kupinga hayo mambo
Mkuu mbona slow learner sana? Nawasisitiza wasitoke tu na barakoa na maji kama wanavyoambiwa ,wajikoki na zana za kujilinda na maadui ,kutoka mikono mitupui kama MO29 walivyofanya ni hatari zaidi kwao ,hauwezi kwenda kupambana na magaidi wa abdul ukiwa na chupa ya maji wakati wao wana VYUMA.
 
Leo tunakwenda almost mwezi wa saba, kijana Deusdedith Soka ma wenzie wamepotezwa. Umma ulipiga kelele mwanzoni, leo umekaa kimya.

Chama chake nacho kimejikalia kimya, hakihangaiki tena na kijana wao, kada wao. Hakuna wa kumsemea!

Kijana jasiri, mzalendo na mpenda nchi yake, nuru yake imezimwa hivihivi. Je walionyakua nuru hii wanajionaje, wanajisikiaje?. Je ni madaraka tu na kiburi chake?

Hawa madhalimu waliomtenda huyu kijana na wenzie je wataishi milele?. Udhalimu wao utawapa afya zaidi?.Utawapa furaha zaidi?.

Soka alinyakuliwa kama mwewe anyakuavyo vifaranga, na wengine wengi wamenyakuliwa. Inauma, inasikitisha, lakini hao madhalimu watajibu mbele ya Muumba mbingu na nchi!

Soma kuhusu maagizo ya Mahakama kwa Serikali: Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea
🥶
 
Back
Top Bottom