Kubaini na kukubali udhaifu ndio hatua ya kwanza ya kutatua changamoto yoyote duniani wazungu wanaita ownership of the problem. Kuna matukio kama hayo yalishatokea na yanaendelea kutokea, hivi sasa wakati natoa comment hii Kuna watu wanapigwa lakini hatujifunzi, kwa nini. ?
Kwa hiyo Ili tutatue hili tatizo kwanza bado sisi Watanzania LAZIMA TUKUBALI wengi wetu ni WAJINGA
Angalia yaliyowahusu au yanaowahusu watu hawa
Babu wa Loliondo
Mchungaji Mwingira
Mzee wa Upako
Mchungaji Kakobe
Mtume/Nabii Mwamposya
Sharifu Majini
Kibwetele
Mr. Kuku, Zanzibar
DECI Mabibo
Gwajima
Na wengine
Hao mtaji wao mkubwa ni ujinga wetu. Hawana jinsi wanaweza ku survive ikiwa sisi tutakuwa werevu
Baada ya kukubali sisi ni WAJINGA, then tunafanya nini kutoka ktk ujinga huu ?
Serikali
Inaonekana haina shida na hawa watu na ndio maana wanaendelea ku survive. Kumbuka tukio la Moshi (Mwamposya)baada ya watu kadhaa kufa tulitarajia serikali ingechukua hatua lakini hicho hakikutokea na bado Mshua anatamba kwenye Majukwaa. Tunajiuliza
Kuna udhaifu ktk kusajili haya Makanisa/ Taasisi ?
Kuna rushwa ?
Kuna maslahi ya kisiasa wakuu wetu wanayapata kushindwa kuwachukulia hatua ?
Kuna udhaifu wa Kisheria ambao wanautumia kama uchochoro kiasi inakuwa ngumu kuwawajibisha ?
Ukiangalia tukio la Moshi baada ya kutokea tu. Waziri wa Home Affairs+ RPC wa Kilimanjaro, walikuwa wako tayari kuchukua hatua. lakini walivyomsoma boss wao JPM alionekana Hana shida na Mshua, hivyo jamaa (RPC + Waziri) wakapotezea hii issue
Yale makumi ya watu waliokufa kwenye lile tukio ikaonekana kama kifo cha panya tu
Na hii love affair haikuwa tu kwa Mshua wa Kawe bali ilikuwa kwa Gwajiboy + Mzee wa Upako
Jamii
Bado jamii yetu Iko nyuma ktk masuala ya kuwasiliana/kufunguka juu ya changamoto tunazokutana nazo
Kwa mfano hata humu JF kungekuwa na platform ya watu walioumizwa na matapeli wa aina hii
Motivational speakers kama Nanauka tulitarajia aje na vitu vya kutahadharisha wananchi wa kawaida na mada kwa mfano "UTAJUAJE KANISA/MCHUNGAJI NI MPIGAJI"
Katika suala hili nampa big up Mchungaji Hananja
Media
Kwanza nilipopata tu taarifa za huyo jamaa Kiboko ya Wachawi nikajiuliza media ambayo ilikuwa Ina host vipindi vyake hawa kuwa wanatathmini maudhui yake. ?
Kwa muda gani amekuwa akiendesha vipindi ?
Hapa sasa ndio naamini kwa kiasi kikubwa sana Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalichochewa na media especially Radio
Education System
Kwenye mfumo wetu wa elimu za dini yaani EDK(Elimu ya Dini ya Kiislamu) + Divinity zitiwe mada maalum jinsi ya kung'amua Matapeli waliojificha kwenye kichaka cha dini
Lakini pia inaweza ikawekwa hata kwenye Civics/General Studies
Wakatabahu