Je, Watanzania tumeridhika kabisa na Dharau, Kejeli na Matusi anayotufanyia sasa Tapeli wa Kiimani 'Kiboko ya Wachawi' akitokea huko Kwao Congo DR?

Aisee... hii safari ndiyo kwanza inaanza.
Gari ni moja, wanaobalika ni madereva tu...
Sijui tutaendeshwa hadi lini...?
Inabidi JESUS arudi haraka aje aone waumini tulivyogeuzwa mazuzu.
 
Mi Kuna mdogo wangu aliniazima gari lake pale kwenye dash board kuna mafuta ya mwamposa, roho ikawa inaniambia yatupe nje, akiuliza utamwambia ulepeleka carwash madogo wameyapoteza labda
Mwisho wa siku nikayaacha tu.
Ni roho ya ibilisi hiyo, ikiona mafuta ya upako inateseka.
 
Ni roho ya ibilisi hiyo, ikiona mafuta ya upako inateseka.
Hakuna kitu kama hicho hivi mafuta ya upako ndio nini? Nyie ndio mnaibiwa yaan mafuta ya upako uyanunue uweke kwenye gari, nyumbani, ofisini, chumbani kwamba ndio utakuwa safe😀😀😀
 
Kuna vitu umeandika lakini huvielewi vizuri nitakujuza vichache tu.

Museven ndio Kibwetere halisi, achana na propaganda. Fuatilia Joseph Kony anatokea wapi na ana uhusiano gani na Kibwetere marehemu.

Pili tukio la Moshi ni hujuma za wazi dhidi ya huduma ya Mwamposa usidhani vyombo vya dola havipo au havipati taarifa, Mwamposa ni tishio kwa makanisa makongwe.

Halafu pia uelewe dini ndio siasa kongwe kabisa duniani, wanasiasa wa leo hawana watu, bali watu wa dini ndio wana watu, kiongozi wa serikali hawezi kucheza na kiongozi wa dini mwenye watu, labda kiongozi huyo awe na ajenda ya kupinduwa serikali hapo ndio partneship yao inaweza kuvunjika.

Unaona kuna ile kamati ya amani ya viongozi wa dini kina sheikh Alhad Musa na wenzake, kile ni chombo tu cha kuwapumbaza Watanzania na hao viongozi wa dini wanalipwa marupurupu yao na serikali.

Kwahiyo viongozi wa dini na serikali ni damdam kasoro wachache ambao wamesimama wahesabiwe wameikataa hii batwili hapo kuna Sheikh Ponda, Askofu Bagoza na Askofu Emaus Mwamakula hao ni mfano kwa uchache wamekataa kutumia majoho yao kuwa machawa wa serikali.
 
Hakuna kitu kama hicho hivi mafuta ya upako ndio nini? Nyie ndio mnaibiwa yaan mafuta ya upako uyanunue uweke kwenye gari, nyumbani, ofisini, chumbani kwamba ndio utakuwa safe😀😀😀
Nina uhakika nakuzidi ufahamu wa mambo mengi ya dunia hii utakuja kuyajuwa baadaye sana.

Mimi nimeukataa utapeli wa ccm unaamini naweza kutapeliwa na watu wa dini?

Kwa taarifa yako mimi ni muumini wa kanisa la Roman katoliki mpaka leo, ila namuelewa vizuri Mwamposa, Yesu yupo pale.

Halafu wengi hamjui chochote zaidi ya kufuata mkumbo wa chuki.

Mwamposa hana kanisa, wala Mwamposa haubiri dini, bali Mwamposa ana huduma (ministry) na siyo Kanisa ( church)

Hizo rituals za mafuta na maji ya upako unaweza kufanya hata ukiwa nyumbani kwako ukanunuwa chupa ya maji na ukajiconnect na madhabau yake kwenye tv, ukishangaa hili washangae wanaoswali kuelekea kibra.
 
Dogo anapiga kazi sana yule namkubali anajitambua kiuchumi wacha awanyolose.
 
Si ametimuliwa Bongo huyu jamaa!? Acha aongee unafikir ni vzr kunyang'anywa tonge mdomoni!? Hana nguvu yyte ya MUNGU ni mlaghai tu hvo apuuzwe yeye na waumini wake.
 
Huyo nae ni tapeli kama matapeli wengine over
 
Sisi hatunaga utaifa,tuna uccm na uchadema na ufisadi unaolindwa na Dola Kwa kivuli Cha katiba mbovu!

Utaifa ulishakufa siku nyingi sana!!

Umebaki hayo!
 
Huyo nae ni tapeli kama matapeli wengine over
Na ndiyo maana Kamtapeli hadi Akili zake na sasa kabakia tu kuwa Juha (Fool) hapa Jamvini hadi kusema kuwa miaka ya 70 aliyokuweko Yeye Tanzania na Mkoani Dar es Salaam kulikuwa hakuna Hospitali ya Agha Khan na kwamba zilizokuwepo ni yake ya Walala Hoi aliyozaliwa ya Ocean Road na Muhimbili. Nilishalidharau hilo Jamaa Kitambo tu na nashangaa sijui kwanini huwa linapenda pia Kushobokea Mada zangu wakati Kutwa linasema halinipendi.
 
Mbona uliambiwa uhamie uhamishoni Burundi kutoka kwenye nchi yako hukuona dharau
 
Sasa ni rasmi Watanzania wachache waliokuwa Wakimuamini wametuponza mno Watanzania wote kwa anayotufanyia.
Na anajua kweli kutu nanga na kutukejeli maana kaja kuchuma huku anawekeza kwao huku alikuwa shambani kujivunia ma pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…