Je, watu wa mikoani na vijijini wakianza vitimbwi wanavyofanyiwa wakienda kwa ndugu zao wa Dar patatosha?

Mkuu. Labda mkeo hajui kupika.
Dar kweli mchele kilo moja watu sita Ila ukumbuke mchele huo una Nazi mbili, Kuna kilo ya nyama roast, Kuna maharage, Kuna mboga za majani, Kuna parachichi moja moja na ndizi mbili. Pembeni Kuna glasi ya maziwa.
Halafu Dar hata kutembea Ni ndani ya Basi. Kitandani tunapiga kimoja. Sasa unataka tufakamie miugali sisi tumekua wadukuma?
 
UMEONGEA UKWELI WA MUNGU. DAR LIFE NI GUMU SANA.
NILIPOKUWA DAR HATA KULA KITIMOTO NUSU ILIKUWA NI ANASA KUBWA. SASA HIVI HUKU IRINGA ANGALAU NAPATA MARA MOJA KWA WIKI NUSU YA 3500.
We acha tu watu wanacomplain kwamba tuna uchoyo lakini MUNGU ndo anajua.
 
Ndio kabla hamjaenda kuzurura majumbani kwa watu mjipange!!!!!!!

Kijijini ni kijijini na mjinj ni mjini!!!!

Haiwezekani mwenyeji wako anakaa chanika huko aje kukupokea saa mbili usiku standi mpya (ya magufuli) bodaboda itakuhusu tu hamna namna
 
Ila dada yako kauzu hadi simu kazima.

Siku nyingine heri utafute 20,000 ya kulala hotelini kwa amani


Wachache sana watakaokuja kukupokea standi saa tano usiku.
 
Watu hawapendi wageni siku hizi kila mtu anataka aishi na familia yake tu
Wachache sana watakukarimu tena uwe na pesa utakaribishwa vizuri
Uwe huna kitu sasa ehehhe unaamshwa asubuhi ufagie
Kuna jamaa kaamshwa asubuhi magodoro yanatolewa nje


Hahahahahahahah
 
Vyote ivo ni visingizio tu...hamna jipya

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Acheni kwenda kuweka makao kwa watu bila sababu za msingi hata kama ni ndugu yako wa damu.

Piga simu uone kama ana nafasi mkutane msalimiane iishe ki namna hiyo. Mambo ya kwenda kulala sijui kwa dada/kaka mwezi mzima kisa tu umekuja na mkungu mmoja wa ndizi toka Katavi huko yamepitwa na wakati.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ni cheap generalization. Siyo wote wachovu na wenye roho mbaya hivyo. Nadhani hapa mleta uzi anapaswa kusema baadhi ya watu na si wote. Pia itoshe kufahamu kuwa kuna watu wanalazimisha kuja Dar es Salaam. Mwingine anataka mwanae akimaliza shule aje umtafutie kazi kana kwamba wewe ni serikali. Mwingine anataka aje asomee kwako au abangaizie kwako. Hapa kweli kuna haki?
 
Ha ha haaaa. Pole sana mkuu, option ya kufikia hotel ndio the best aisee. Bora wakulaumu lakini mwisho wa siku unakaa kwa amani huko hotelini na kufany mambo yako kwa uhuru.
 
Ila wajaluo Ni kiboko.
Kuna dogo mmoja alikuja Dar toka huko kwao usweken kanda maalum akafikia kwa ndugu zake. Asubuhi aliambiwa atengeneze chai na vitafunio vilikuwepo vingi tu dogo akaona Maisha si ndio haya. Ile anasubiriya waitwe mezani akaambiwa amsindikize mtoto kituo Cha Basi akapande school bus. Dogo alitimiza Kama alivyoambiwa Ila alivyorudi alikuta wenyeji walishakunywa chai yote na vitafunio vyote na baba alimuambia vaa chap twende mjini. Dogo akawa amepiga desh masuala ya chai. Kule town baba alimzungusha tu bila kumtafutia kazi au Nini lengo lake nyumbani wale Cha mchana ili wakifika home saa kumi wakute Cha mchana kilishaliwa. Mzee mwenyewe kule mjini alishakula wali wake. Ilipofika jioni Kama ujuavyo watu wa Dar usiku wanakula viwali ambavyo kule Tarime vinapewa mtoto Tena mgonjwa. Jamaa hivyo viwali vikawa ndio breakfast, lunch na dinner. Wakalala. Asubuhi like zoezi likarudiwa Tena, yaani yeye ampeleke dogo kituoni awahi school bus, kurudi anakuta watu walishakunywa chai long time.
Kama ilivyo kawaida watu wa mkoani wanaogopa njaa kuliko ukoma. Dogo alitangaza kurudi Tarime. Mzee akaulisa yeye. Nauli unayo? Dogo akawa Hana nauli, Basi mama wa nyumba Ile akasema isiwe tabu. Wana sehemu uani inahitaji ilimwe kuliko wampe hicho kibarua mtu mwingine, watampa dogo ili apate nauli.
Basi kila siku dogo akiamka anamuwahisha dogo stendi ya school bus, akirudi chai ilishanywewa anachukua jembe anakwenda kuhenya uani. Mchana hastuliwi Wala Nini mpaka jioni ndio ale vi wali.
Dogo alimaliza Ile kazi ya kulima ndani ya wiki ili apate nauli. Na walivyo washenzi walimpa nauli tu bila ya kula njiani.
Dogo ameapa kwamba yule sio ndugu yake Tena na mke wake wa kipare wote sio binadamu.
 
muda wa kupakua msosii watu wa mjini/dsm wanakodoa mimachoooo manake wanawaza mgeni akipakua kingii je kitakachobaki kitawatosha na wengineee ....hasa watu wa kanda ya ziwa wanapenda ubwabwaa na maharagweee sana
Umaskini uliokithiri
 
Mmh huyo mwenyeji wako ana nyumba ya vyumba viwili, na ni maskini au mkosa shingo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…