Je, watu wa mikoani na vijijini wakianza vitimbwi wanavyofanyiwa wakienda kwa ndugu zao wa Dar patatosha?

Je, watu wa mikoani na vijijini wakianza vitimbwi wanavyofanyiwa wakienda kwa ndugu zao wa Dar patatosha?

Wa DSM wanakiwaga wajanja sana mikoani... ukiibuka kwao wamechoka sana. huwa nashangaa eti familia ya watoto 6, mke na Mme wana kula mchele kilo moja... wao wanaujazo gani Wa matumbo?

watoto wangu watatu Range, Median na Mode wanaikamua kilo na hawabakizi hata punje.

DSM mnakwama wapi?...
Mkuu. Labda mkeo hajui kupika.
Dar kweli mchele kilo moja watu sita Ila ukumbuke mchele huo una Nazi mbili, Kuna kilo ya nyama roast, Kuna maharage, Kuna mboga za majani, Kuna parachichi moja moja na ndizi mbili. Pembeni Kuna glasi ya maziwa.
Halafu Dar hata kutembea Ni ndani ya Basi. Kitandani tunapiga kimoja. Sasa unataka tufakamie miugali sisi tumekua wadukuma?
 
UMEONGEA UKWELI WA MUNGU. DAR LIFE NI GUMU SANA.
NILIPOKUWA DAR HATA KULA KITIMOTO NUSU ILIKUWA NI ANASA KUBWA. SASA HIVI HUKU IRINGA ANGALAU NAPATA MARA MOJA KWA WIKI NUSU YA 3500.
We acha tu watu wanacomplain kwamba tuna uchoyo lakini MUNGU ndo anajua.
 
Ndio kabla hamjaenda kuzurura majumbani kwa watu mjipange!!!!!!!

Kijijini ni kijijini na mjinj ni mjini!!!!

Haiwezekani mwenyeji wako anakaa chanika huko aje kukupokea saa mbili usiku standi mpya (ya magufuli) bodaboda itakuhusu tu hamna namna
 
Ila dada yako kauzu hadi simu kazima.

Siku nyingine heri utafute 20,000 ya kulala hotelini kwa amani

Wachache sana watakaokuja kukupokea standi saa tano usiku.
Mimi nilifika dar.usiku saa tano kuangaza mwenyeji hayupo ubungo.kupiga sim hapatikani hee.baada ya masaa mawili ndio napigiwa na dada wa kazi umefika wapi dada kalala, chukua bodaboda ikupeleke fery uvuke kuja kigamboni saa saba na nusu hiyo usiku.nafika kigamboni sim haipatikani nikakaa hapo na walinzi baadae anapiga chukua boda tena ikulete dege.hata dege sipajui jamani huyo boda boda alikua ana pepeza pikipiki kila nikitaka kuongea midomo haiwezi sababu ya supidi, Tukawa tunatokomea tu nauliza bado anasema bado saa tisa usiku hiyo, mpaka nafika saa kumi.kufika hamna maji ya kuoga hamna chakula.nikalala nashtuka saa kumi ba mbili dada ananiambia amka tufanye usafi nikasema bado napumzika.Akasema Lazima tutoe magodoro.Nikahamia sebuleni ile usingizi unaanza naambiwa hata hapo nakuja kakae nje.Dah sitasahau nimeacha mkoani mjengo wangu wa maana kitanda nateseka wallah nilitoa chozi.Nilipata homa kali sikununua hata biashara nikarudi nyumbani baada ya siku tatu.mpaka leo nikija Dar nina ndugu lakini nafikia Hotel.Bora lawama kuliko fedheha
 
Watu hawapendi wageni siku hizi kila mtu anataka aishi na familia yake tu
Wachache sana watakukarimu tena uwe na pesa utakaribishwa vizuri
Uwe huna kitu sasa ehehhe unaamshwa asubuhi ufagie
Kuna jamaa kaamshwa asubuhi magodoro yanatolewa nje

Hahahahahahahah
 
Hali duni ya maisha inachangia, mtu ana room moja kwa siku akitumia 3000 kafuja pesa, Hana ajira ya maana huyo kuku unaesema anachinjiwa akipenda mkoa huku anaishiaga kula miguu tena mabroiler, Sometimes mkoani inatakiwa ijulikane ni sehemu ambayo tukienda tunaenda kurefresh mind, Huku Dar ni vitani, Sasa ndugu kaja kukutembelea vitani anategemea nini? Hatukatai kutembelewa ila wanatakiwa kujua huku ukisimama nchale ukiinuka nchale.
Vyote ivo ni visingizio tu...hamna jipya

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Acheni kwenda kuweka makao kwa watu bila sababu za msingi hata kama ni ndugu yako wa damu.

Piga simu uone kama ana nafasi mkutane msalimiane iishe ki namna hiyo. Mambo ya kwenda kulala sijui kwa dada/kaka mwezi mzima kisa tu umekuja na mkungu mmoja wa ndizi toka Katavi huko yamepitwa na wakati.
 
Alikuaja Dar kwa mdogo wake toka ntoke mzee mmoja wa kipare anaitwa Mshana. Mdogo wa Mshana akachinja kuku Safi kabisa. Kule upareni Kama kuku imechinjwa wakati wa kula mnaanza na ugali tonge mbili tatu ndio yule mkubwa kuliko wote anaokota nyama , usually anaokota paja ,then anafuatia mwingine kwa ukubwa hivyo hivyo mpaka mdogo kabisa anaambulia ATC.
Sasa mzee wa kipare toka bush wakati anaanza kunawishwa yeye akajua taratibu za kipare zitazingatiwa. Ile mzee amekata tonge la kwanza akakuta watoto wa mdogo wake yaani watoto wa mjini Mwananyama ndaani ndani walishachukua nyama zote nzuri na kwenye sahani kimebaki kipande Cha shingo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ila watu wa mijini na kwenye majiji kuna haja ya kujitafakari.

Mwana DSM ukienda mikoani huko au vijijini ukifika ni kawaida sana kukuta ndugu zako walikuwa wanakusubiri stendi zaidi ya saa ufike, umefika utachinjiwa kuku siku ya kwanza, utaishi hata mwezi na hakuna mtu atakupa maswali ya unaondoka lini, misosi utakula utasaza, ukiondoka utapewa hata debe la unga au maharage na hapo ukunbuke wewe ulipeleka tu mkate, unavyoondoka unasindikizwa kabisa wengine wanakubebea begi, kiufupi watu wa huko wengi ni wakarimu.

Ishu inakuja kwa watu wa Dar sasa, yani hata ndugu kaja kumpokea tu ni mtihani, mwenyeji anatoa maelekezo mgeni ampe simu bodaboda na malipo atalipa mgeni ambae hata hio hela haikuwa kwenye bajeti, akifika msosi ulioandaliwa ni ugali tembele yani ugeni wake ni kama hauthaminiki kama sio kumkomoa, baada ya salamu mwenyeji atakua bize na simu au mke wake kitu kinachoanza kukaribisha upweke kwa mgeni, mgeni akikaa siku 2 tu anaanza kuulizwa anaondoka lini, siku ya kuondoka pekee labda ndio mgeni husindikizwa maana ndio anasepa ni kama mzigo umetoka.

Sasa nauliza hivi watu wa huko mikoani nao wakiamua kwenda kwa style hizo kama zenu, je patatosha?
Hii ni cheap generalization. Siyo wote wachovu na wenye roho mbaya hivyo. Nadhani hapa mleta uzi anapaswa kusema baadhi ya watu na si wote. Pia itoshe kufahamu kuwa kuna watu wanalazimisha kuja Dar es Salaam. Mwingine anataka mwanae akimaliza shule aje umtafutie kazi kana kwamba wewe ni serikali. Mwingine anataka aje asomee kwako au abangaizie kwako. Hapa kweli kuna haki?
 
Mimi nilifika dar.usiku saa tano kuangaza mwenyeji hayupo ubungo.kupiga sim hapatikani hee.baada ya masaa mawili ndio napigiwa na dada wa kazi umefika wapi dada kalala, chukua bodaboda ikupeleke fery uvuke kuja kigamboni saa saba na nusu hiyo usiku.nafika kigamboni sim haipatikani nikakaa hapo na walinzi baadae anapiga chukua boda tena ikulete dege.hata dege sipajui jamani huyo boda boda alikua ana pepeza pikipiki kila nikitaka kuongea midomo haiwezi sababu ya supidi, Tukawa tunatokomea tu nauliza bado anasema bado saa tisa usiku hiyo, mpaka nafika saa kumi.kufika hamna maji ya kuoga hamna chakula.nikalala nashtuka saa kumi ba mbili dada ananiambia amka tufanye usafi nikasema bado napumzika.Akasema Lazima tutoe magodoro.Nikahamia sebuleni ile usingizi unaanza naambiwa hata hapo nakuja kakae nje.Dah sitasahau nimeacha mkoani mjengo wangu wa maana kitanda nateseka wallah nilitoa chozi.Nilipata homa kali sikununua hata biashara nikarudi nyumbani baada ya siku tatu.mpaka leo nikija Dar nina ndugu lakini nafikia Hotel.Bora lawama kuliko fedheha
Ha ha haaaa. Pole sana mkuu, option ya kufikia hotel ndio the best aisee. Bora wakulaumu lakini mwisho wa siku unakaa kwa amani huko hotelini na kufany mambo yako kwa uhuru.
 
Ila wajaluo Ni kiboko.
Kuna dogo mmoja alikuja Dar toka huko kwao usweken kanda maalum akafikia kwa ndugu zake. Asubuhi aliambiwa atengeneze chai na vitafunio vilikuwepo vingi tu dogo akaona Maisha si ndio haya. Ile anasubiriya waitwe mezani akaambiwa amsindikize mtoto kituo Cha Basi akapande school bus. Dogo alitimiza Kama alivyoambiwa Ila alivyorudi alikuta wenyeji walishakunywa chai yote na vitafunio vyote na baba alimuambia vaa chap twende mjini. Dogo akawa amepiga desh masuala ya chai. Kule town baba alimzungusha tu bila kumtafutia kazi au Nini lengo lake nyumbani wale Cha mchana ili wakifika home saa kumi wakute Cha mchana kilishaliwa. Mzee mwenyewe kule mjini alishakula wali wake. Ilipofika jioni Kama ujuavyo watu wa Dar usiku wanakula viwali ambavyo kule Tarime vinapewa mtoto Tena mgonjwa. Jamaa hivyo viwali vikawa ndio breakfast, lunch na dinner. Wakalala. Asubuhi like zoezi likarudiwa Tena, yaani yeye ampeleke dogo kituoni awahi school bus, kurudi anakuta watu walishakunywa chai long time.
Kama ilivyo kawaida watu wa mkoani wanaogopa njaa kuliko ukoma. Dogo alitangaza kurudi Tarime. Mzee akaulisa yeye. Nauli unayo? Dogo akawa Hana nauli, Basi mama wa nyumba Ile akasema isiwe tabu. Wana sehemu uani inahitaji ilimwe kuliko wampe hicho kibarua mtu mwingine, watampa dogo ili apate nauli.
Basi kila siku dogo akiamka anamuwahisha dogo stendi ya school bus, akirudi chai ilishanywewa anachukua jembe anakwenda kuhenya uani. Mchana hastuliwi Wala Nini mpaka jioni ndio ale vi wali.
Dogo alimaliza Ile kazi ya kulima ndani ya wiki ili apate nauli. Na walivyo washenzi walimpa nauli tu bila ya kula njiani.
Dogo ameapa kwamba yule sio ndugu yake Tena na mke wake wa kipare wote sio binadamu.
 
muda wa kupakua msosii watu wa mjini/dsm wanakodoa mimachoooo manake wanawaza mgeni akipakua kingii je kitakachobaki kitawatosha na wengineee ....hasa watu wa kanda ya ziwa wanapenda ubwabwaa na maharagweee sana
Umaskini uliokithiri
 
Mimi nilifika dar.usiku saa tano kuangaza mwenyeji hayupo ubungo.kupiga sim hapatikani hee.baada ya masaa mawili ndio napigiwa na dada wa kazi umefika wapi dada kalala, chukua bodaboda ikupeleke fery uvuke kuja kigamboni saa saba na nusu hiyo usiku.nafika kigamboni sim haipatikani nikakaa hapo na walinzi baadae anapiga chukua boda tena ikulete dege.hata dege sipajui jamani huyo boda boda alikua ana pepeza pikipiki kila nikitaka kuongea midomo haiwezi sababu ya supidi, Tukawa tunatokomea tu nauliza bado anasema bado saa tisa usiku hiyo, mpaka nafika saa kumi.kufika hamna maji ya kuoga hamna chakula.nikalala nashtuka saa kumi ba mbili dada ananiambia amka tufanye usafi nikasema bado napumzika.Akasema Lazima tutoe magodoro.Nikahamia sebuleni ile usingizi unaanza naambiwa hata hapo nakuja kakae nje.Dah sitasahau nimeacha mkoani mjengo wangu wa maana kitanda nateseka wallah nilitoa chozi.Nilipata homa kali sikununua hata biashara nikarudi nyumbani baada ya siku tatu.mpaka leo nikija Dar nina ndugu lakini nafikia Hotel.Bora lawama kuliko fedheha
Mmh huyo mwenyeji wako ana nyumba ya vyumba viwili, na ni maskini au mkosa shingo
 
Back
Top Bottom