Mkuu. Labda mkeo hajui kupika.Wa DSM wanakiwaga wajanja sana mikoani... ukiibuka kwao wamechoka sana. huwa nashangaa eti familia ya watoto 6, mke na Mme wana kula mchele kilo moja... wao wanaujazo gani Wa matumbo?
watoto wangu watatu Range, Median na Mode wanaikamua kilo na hawabakizi hata punje.
DSM mnakwama wapi?...
Dar kweli mchele kilo moja watu sita Ila ukumbuke mchele huo una Nazi mbili, Kuna kilo ya nyama roast, Kuna maharage, Kuna mboga za majani, Kuna parachichi moja moja na ndizi mbili. Pembeni Kuna glasi ya maziwa.
Halafu Dar hata kutembea Ni ndani ya Basi. Kitandani tunapiga kimoja. Sasa unataka tufakamie miugali sisi tumekua wadukuma?