Je, watumia Zoom? Chukua tahadhari namna ya kujilinda na mambo kama ya kurekodi na kupeana picha na pia hatua za kiusalama security settings control .

Je, watumia Zoom? Chukua tahadhari namna ya kujilinda na mambo kama ya kurekodi na kupeana picha na pia hatua za kiusalama security settings control .

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Taarifa za uhakika kabisa za kijasusi zilizopo ni kwamba jeshi la polisi chini ya kamanda Mafwele wapo kazini kuwatafuta, kuwabaini na kuwatambua wale wote walohusika na kuandaa mikutano ya kupanga maandamano ambayo kwa namna fulani yamefanikiwa kufikisha ujumbe.

Ujumbe wa maandamano hayo ulikuwa ni kusimamishwa uchaguzi, mabadiliko ya katiba, kuwaachia wale wote ambao wametekwa.

Sasa taarifa zilizopo za kijasusi zadai kuwa mara tu baada ya kuapishwa Samia Suluhu Hassan kuwa raisi wa awamu ya sita, polisi khasa wale wa ile "task force" ( na wengineo) wataingia kazini kuanza rasmi kimyakimya kuwatafuta kuwatambua na kuwakamata vijana wote waloshiriki kuandaa, kupanga na hatimae kufanikisha kuwepo kwa maandamano kwa kutumia Application ya Zoom.

Moja ya mbinu ambayo taskforce wametumia ni kuchukua "screenshots" za watu wote walohusika na mipango hiyo ambazo baadae watazitumia kuwasaka na kuwatambua kimyakimya na kisha kuwapoteza. Application ya Zoom ya kawaida haina uwezo wa kuzuia mtu asichukue screenshots na pia kutokana na uelewa mdogo wa waandaji wa mijadala (discussions) kwenye app hiyo walipitiwa juu ya kuchukua hatua za tahadhari kuzuia baadhi ya washiriki ambao ni mapandikizi wasiweze kuchukua hizo picha kwa kutumia simu zao za mkononi.

Taarifa hizo za kijasusi zimeendeea kudai kuwa baadhi ya washiriki wa mijadala hiyo ni watoa taarifa yaani "informers" ambao wameshiriki kindakindaki kwenye kila hatua ya maandamano hayo na kuanzia kesho hawatoonekana tena.

Sasa ni vipi mtumiaji wa Zoom aweza kuhakikisha usalama wake akiwa mtandaoni?

Njia pekee nzuri na salama kabisa ni kutumia vidhibiti vya kugawana picha kurekodi yaani "screen sharing and recording controls". Pia njia ingine ni kurekebisha vidhibiti vya usalama yaani "meeting security settings."

Njia zingine za msingi ambazo mtayarishaji au Host aweza kuzitumia ni kama ifuatavyo:

1. Kudhibiti kurekodi mazungumzo yaani ni weye Host pekee ndiye mwenye uwezo wa kurekodi.
2. Kuhakikisha hutoa ruhusa kwa washiriki kufanya recordings.
3. Ingawa njia hiii yazuia kurekodi mazungumzo lakini haiwezi kuzuia washiriki kuchukua picha au screenshots.
4. Zuia washiriki wasiweze kuchukua maingizo ya maneno yako (content) au pia hata kuyachakachua yaani yakiwa Disable Annotation Option.

5. Njia hii ni muhimu sana yaani "very important" kwamba Zoom yako iwe ni ile ya kulipia khasa lifikapo suala la kutumia barua pepe. Hapo utawezesha kitu chaitwa "Watermark" ambacho kitatokea juu ya barua pepe ya mshiriki ambae mtu mwenye nia ovu atataka kuchukua taarufa za anuani ya barua hiyo pepe na pia Awatermark hiyo itasaidia kubaini mshiriki aliechukua picha au screenshot.

Hata hivyo Zoom haiwezi kuzuia vifaa vya nje kama simu za mkononi na vifaa vya kutunzia naraka au documents kama USB, CDs na vingine.

Hivyo kwa kuhitimisha hii mada njia nzuri na kutumia kwa ujumla ili kujiepusha na madhila ya kikosi kazi cha kamanda Mafwele, chukua hatua hizi za ziada.

1. Gawa au share mambo ambayo yana umuhimu na vitu vingine vyote ambazo havina umuhimu viweke mbali na screen. Vitu hivi vyaweza kutambulisha mahali ulipo.

2. Tumia vyumba maalum vya kusubiria na pia nywila kwa kila mshiriki apigae hodi kutaka kuingia kwenye mjadala.

3. Wakumbushe washiriki kutochukua screenshots endapo mijadala ni ya siri.

4. Ukitaka kugawana documents ambazo ni nyeti basi tumia njia ya barua pepe (emails) au hata kuweka kwenye "cloud storage" badala ya kuonyesha kwenye Zoom.

Pamoja na hii ya Zoom bado TCRA wapo makini na kila kitembeacho katika mitandao ya kijamii khasa WhatsApp, Tik-Tok na Facebook.

Nimechukua wakati huu kuandika haya nikitarajia vijana Tech Savvy wa GenZ watasoma na wataelewa.
 
Back
Top Bottom