Tongue blister
JF-Expert Member
- Jun 19, 2009
- 362
- 11
Hii ni habari ya kweli kabisa,Rafiki yangu wa damu walitengana au tuseme waliachana na mkewe miaka mingi iliyopita.
Mkewe huyo akaolewa na kuzaa watoto kadhaa. Sasa rafiki yangu huyu kaniambia nimtafutie mchumba nikamsimulia kuhusu shemeji yangu mmoja yuko upcountry nikampa namba ya simu wakaweza kuwasiliana.
Cha kushangaza ni kuwa rafiki yangu huyu amefikia hatua ya kufanya maamuzi ya kumuoa yule shemeji yangu, hawajakutana hawajuani hata picha yake kila mmoja hamjui mwenzake zaidi ya mawasiliano kwenye simu tuu!!!
Ni mwezi wa tatu sasa unaenda wako kwenye mapenzi moto moto, ila kutokana na wingi wa kazi kila mmoja hapati mwanya wa kwenda kuonana na hasa hasa umbali uliopo kati yao.
Naomba kusikia kutoka kwenu wadau.
Kiroroma jibu unalo kwanini unatusumbua watu mkuu ? wk end ishaanza kaka, tunataka kuanza kuchapa maji !!!
Point ni kwamba anaamini maelezo yako..!! Ulisha msimulia kuhusu shemejio..!! Labda uulize kwamba kwanini Rafiki yako ameamua kukuamini wewe katika jambo la kumtafutia mchumba !! Na si kwanini kaamini mwanamke uliyo mtafutia! Kwaheri na wk njema !!!!