Je, wazazi wetu walituletea urithi wa umaskini, au walitupa msingi ambao hatujajua kuutumia?

Je, wazazi wetu walituletea urithi wa umaskini, au walitupa msingi ambao hatujajua kuutumia?

Bikra unayo

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2026
Posts
638
Reaction score
2,312
Wengi wetu tulilelewa na wazazi waliofanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha tunapata chakula, elimu na mahitaji muhimu.

Baadhi yao walijenga nyumba, mashamba au biashara. Wengine hawakufanikiwa kupata mali nyingi kwa sababu ya kipato kidogo, majukumu makubwa au changamoto za maisha.

Tunapokuwa watu wazima, tunaanza kutambua kwamba elimu na malezi mazuri ni zawadi kubwa, lakini wakati mwingine haviji na msingi wa kutosha wa kifedha.

Hapo ndipo swali linapokuja:

== Je tunapaswa kuwajibika kwa maisha tuliyokuta au kujenga mazingira tofauti kwa watoto wetu?


==Je, wazazi wanapaswa kuhakikisha watoto wao wanarithi mali, au kuwapa elimu na uwezo wa kujitegemea kunatosha?


==Kama umeanza maisha bila urithi wa mali, unaweza kupunguza vipi pengo hilo kwa kizazi chako?


==Ni maarifa gani ya fedha ambayo ungependa kufundishwa na wazazi wako lakini hukuyapata toka kwako ?

==Je, ni bora kutumia fedha zote kuhakikisha watoto wanapata maisha yenye kipato cha uhakika kupitia elimu na baadae ajira, au ni bora kubakiza mali ambayo watairithi?


==Unaona jukumu lako kuu ni kuboresha maisha yako, kuwasaidia wazazi wako, au kuandaa msingi kwa watoto wako?

==Unawezaje kusawazisha yote hayo ukiwa kama mzazi, mtoto kwa wazazi wako wazee na mbeba maono wa maisha yako binafsi?

Tushirikishane mafunzo ambayo familia zetu zimetupa kuhusu pesa, na yale tunayopaswa kubadilisha ili kizazi kijacho kiwe na nafasi nzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom