Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
1. Dunia ya Mungu ilikuwa mashariki ya kati?
Hapa ndio kama Mungu alipatambua kama uumbaji wake! Si kwamba hakukuwa na maisha mengine la hasha yalikuwepo! Soma habari za Lilith au Kaini kwenda kuoa 'huko kwingine' baada ya kumuua ndugu yake!
2.Dini zote zinazoamini katika uwepo wa Mungu asili yake ni mashariki ya kati, hata katika misahafu tunachosoma kwa sehemu kubwa sana ni habari za mashariki ya kati..
Habari na matukio makuu ya dunia yote ni hapo
- Bustani ya Eden
- Mnara wa Babel
-Gharika ya Nuhu
-Sodoma na Gomorah etc etc
Kuna mahali kwenye kitabu cha Mithali tunaaswa kutafuta elimu hata mpaka China! Kwa hiyo hii ilikuwepo pia
3. Historia ya mzungu haiandikwi popote (I may be corrected) ama inaandikwa kwa uchache! Africa ilijulikana kwa Mungu(aliitambua pia) soma habari za mafarao na mfalme Suleiman na Cheopatra na asili zao!
4. Mzungu ni mvamizi wa dunia( possibly Alien ama mkuzimu) cha kushangaza mno ndio tunamchukulia kama uzao wa Mungu kutokana na yote aliyoyafanya ya kushangaza hapa duniani hasa kwenye tech
Kwa kutumia ufahamu wake na uwezo wake mkuu mzungu amejitahidi kuidanganya na kuiaminisha dunia kuwa yeye ndio kiumbe bora zaidi duniani( haya matangopori wamelishwa wengi na kuvimbiwa)
Kwa kutumia ushawishi wake huo ameweza kuigeuza historia ya dunia na kuweka mapicha yake kutuaminisha
Mambo yote mabaya yana mkono wa mzungu...mipango ya muda mrefu na ya siri sana ya kutaka kuangamiza uzao wa dunia je ni hofu kuwa wenye dunia yao kuna siku watakuja kuamka na kufunuliwa ukweli?
Hofu ni ya nini mpaka alete utambulisho wa microchips mwilini?
Hofu ya nini mpaka aanzishe projects nyingi za kuleta na kueneza imani zinazopingana na Mungu?
Hofu ni ya nini mpaka yale mambo ambayo ni chukizo mbele za Mungu yeye ayashadadie kwa kiwango cha juu mno?
Hofu ni ya nini mpaka aendelee kuichonganisha na kuipiganisha mashariki ya kati kila uchao?
Utajiri wa dunia (mafuta na madini) kwa sehemu kubwa vinapatikana hapo mashariki ya kati na Africa! Huko kwingine Mungu hakukubariki! Huko ndiko alikotokea Lilith! Huko ndiko asili ya Kaini alikimbilia! Huko ndiko kulikolaaniwa na Mungu ndio maana hawakubarikiwa chochote cha asili (wengi hawatanielewa)
Huko ndiko walikotikea wale wanefili majitu makubwa
Kila kitu kina pande mbili hasi na chanya! Mzungu anajua upande wa hasi ni upi ndio maana haachi kuhangaika na kule kulikobarikiwa
WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA! MUNGU HAJAWAHI KUSHINDWA