Je, wazungu sio wakazi asilia wa hii dunia?

Badala ya kuzungumzia kuhusu mzungu nadhani ni bora tuzungumzie ipi haswa ni asili yetu watu weusi?,
kila kitu kinaelezwa ndani ya biblia, baada ya gharika ya nuhu ambaye alikuwa na wanaye watatu, ham, shem na sijui yafethi hivi, ikatokea mmojawapo akalaaniwa na baba yao(mzee nuhu) ndio kuanzia hapo huyo mwana aliyemlaani akawa anaitwa 'kushi' maana yake ni black, na huyo ndiye baba wa blacks wote
hamu alimkosea Baba yake Nuhu. hamu alizaa Kushi ambae Ni Nubi,Misri,puti na kanaani. Nuhu alimlaani kanaani hakumlaani kushi au hamu.Kushi ipo Kati ya Ethiopia na Sudan kama sijajosea
 
I Someni Quran ndio utajua Mungu ni yupi na nani wa kuabudiwa, na mitume ni ipi na yupi wa kuabudiwa, utajua binadamu alianza vipi na aliumbwa vipi na aliletwa duniani kwa mujibu Upi, na sisi pia tulibadilika katika mataifa tofauti Kivipi, yote hayo yapo katika Quran.

Quran inaeleza past, present and future
Apana labda kule kwenye prymid za giza
 
View attachment 535737kuna vitu vingi vya kushangaza mno, ambavyo kutokana na kutwezwa na mahangaiko ya dunia tunakosa muda wa kuvitafakari
1. Dunia ya Mungu ilikuwa mashariki ya kati?
Hapa ndio kama Mungu alipatambua kama uumbaji wake! Si kwamba hakukuwa na maisha mengine la hasha yalikuwepo! Soma habari za Lilith au Kaini kwenda kuoa 'huko kwingine' baada ya kumuua ndugu yake!

2.Dini zote zinazoamini katika uwepo wa Mungu asili yake ni mashariki ya kati, hata katika misahafu tunachosoma kwa sehemu kubwa sana ni habari za mashariki ya kati..
Habari na matukio makuu ya dunia yote ni hapo
- Bustani ya Eden
- Mnara wa Babel
-Gharika ya Nuhu
-Sodoma na Gomorah etc etc
Kuna mahali kwenye kitabu cha Mithali tunaaswa kutafuta elimu hata mpaka China! Kwa hiyo hii ilikuwepo pia

3. Historia ya mzungu haiandikwi popote (I may be corrected) ama inaandikwa kwa uchache! Africa ilijulikana kwa Mungu(aliitambua pia) soma habari za mafarao na mfalme Suleiman na Cheopatra na asili zao!

4. Mzungu ni mvamizi wa dunia( possibly Alien ama mkuzimu) cha kushangaza mno ndio tunamchukulia kama uzao wa Mungu kutokana na yote aliyoyafanya ya kushangaza hapa duniani hasa kwenye tech
Kwa kutumia ufahamu wake na uwezo wake mkuu mzungu amejitahidi kuidanganya na kuiaminisha dunia kuwa yeye ndio kiumbe bora zaidi duniani( haya matangopori wamelishwa wengi na kuvimbiwa)
Kwa kutumia ushawishi wake huo ameweza kuigeuza historia ya dunia na kuweka mapicha yake kutuaminishaView attachment 535749 Mambo yote mabaya yana mkono wa mzungu...mipango ya muda mrefu na ya siri sana ya kutaka kuangamiza uzao wa dunia je ni hofu kuwa wenye dunia yao kuna siku watakuja kuamka na kufunuliwa ukweli?
Hofu ni ya nini mpaka alete utambulisho wa microchips mwilini?
Hofu ya nini mpaka aanzishe projects nyingi za kuleta na kueneza imani zinazopingana na Mungu?
Hofu ni ya nini mpaka yale mambo ambayo ni chukizo mbele za Mungu yeye ayashadadie kwa kiwango cha juu mno?
Hofu ni ya nini mpaka aendelee kuichonganisha na kuipiganisha mashariki ya kati kila uchao?
Utajiri wa dunia (mafuta na madini) kwa sehemu kubwa vinapatikana hapo mashariki ya kati na Africa! Huko kwingine Mungu hakukubariki! Huko ndiko alikotokea Lilith! Huko ndiko asili ya Kaini alikimbilia! Huko ndiko kulikolaaniwa na Mungu ndio maana hawakubarikiwa chochote cha asili (wengi hawatanielewa)
Huko ndiko walikotikea wale wanefili majitu makubwa
Kila kitu kina pande mbili hasi na chanya! Mzungu anajua upande wa hasi ni upi ndio maana haachi kuhangaika na kule kulikobarikiwa

WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA! MUNGU HAJAWAHI KUSHINDWA

Mzungu ni nani na katokea wapi? je kipindi ambacho yesu anazaliwa huko mashariki ya kati wale akina kaisari amabao walikua ni watawala wa ufalme wa kirumi walikua watu gani kama sio wazungu? swala la kuwapondea ni wivu wetu tu sisi watu weusi na hali ya kukosa ubunifu na akili za kukabiliana nao..... ikumbukwe kua hata hizo dini mnazojifichia akazileta huyohuyo mzungu na ndio aliowafundisha ustaarabu pamoja na kuuleta ukoloni na badae kusaidia harakati za mapambano dhidi ya biashara ya utumwa na baadae ukoloni...

kama kweli mtoa mada unadai sisi ni watu wa mungu iweje hao tunaowasema vibaya wapendelewe kua na maendeleo pamoja na utajiri uliotukuka?
hayo ni maneno tu ya mfa maji....walishatutangulia kutokana na matumizi yao sahihi ya akili zao.....
na huyu Mungu mnaemuongelea pengine sio mungu mkuu na ndio maana wao wazungu kama wana mungu wao amekua anawasaidia sana na mambo yao yanakwenda vizuri.
 
Bw. Mshana Jr asante kwa mada tajwa, naomba kupingana nawe.

Maelezo yako si tu kwamba hayana ushahidi wala mashiko (kisayansi au kihistoria) lakini pia ni potofu.

Naanza kuona madhara ya mythology na spirit-ism. Katika hali ya kawaida na kwa hadhi yako hapa JF, dhana yako ya Wazungu ni wavamizi "aliens" imejengwa kwenye imani ya mambo ya hadithi za kimizimu lakini ktk akili ya kawaida na uhalisia ni hoja mfu kabisa.

Historia inaonyesha na kuthibitisha kuwa binadam wa kale (Adam-Nuhu) waliishi kwenye dunia ya wakati huo. Historia inaonyesha baada ya Gharika ya Nuhu, jinsi jamii, watu na mataifa ya ulimwengu (uliofuata baada ya Gharika) walivyoishi na kutawanyika. Historia imejaa ushahidi na taarifa za makabila, lugha na tamaduni za mataifa ya ulimwengu wakiwemo Wazungu. Sayansi pia inaonyesha Mzungu ni binadamu kama Mwafrika, Mu-Asia, Mlatino yeyote kwa 100%. Suala la rangi yao (ukizingatia wana tofautiana hata wao kwa wao) halina mashiko kwa vigezo vyako hapo juu.

Kwa vile Mzungu ni binadam (wa kawaida) ndio maana anahusika na madhara na uharibufu katika dunia hii na sio ktk sayari nyingine. Unataka kuniambia matatizo tuliyo nayo leo ni Tanzania ni mkono wa Mzungu tu? Ni upi mchango wa jamii nyingine kama Waafrika, Waasia nk kwenye matatizo yetu?

Hebu nikuulize yafuatayo:-

1) Mzungu amemzidi nini (kimaumbile, kiumuundo) Mwafrika au Mlatino au Mu-Asia?

2) Hao Wazungu "aliens", wana mfumo gani hasa wa maisha?

3) Je wanazaa, wanaugua na kufa?
 
Sijui una maana gani kuweka pamoja mchango wangu na wa BL.

Lakini nisisitize tu, you're planting a bad & evil seed which once brought to harvest.....breath... the havoc will be unimaginable.

Unaweza kuona jinsi kuna watu wamemeza kichwa kichwa maneno yako bila hata kujiuliza. Wengi wao ni kwa kusukumwa na hisia (hatred, prejudice) na ignorance. Lakini wewe unayewa expose kwa kuwalisha "sumu" you will not remain innocent.
 
Mkuu wala usihofu nadhani bwana mshana anaeleza matokeo ya fikra zake sasa ni wajibu wetu kumuuliza na kuutafuta ukweli ambae utapatikana kwa kupitia maswali na majibu ila ninachokiona hapa mtoa hana majibu ya maswali mengi ambayo yanatokana mada yake.
 
Am sorry kwa hilo lakini nilitaka kujibu kwa pamoja ila reply yangu haikuonekana
Nimeweka hii mada kama hoja jadilika na ili iweze kuleta ushawishi ni lazima niwe na upande (mtazamo wangu unaweza kuwa na pingamizi nyingi) lakini mwisho wa siku ni kujifunza na kupanua ufahamu

Sipendi kuwa rigid kwenye mjadala labda tu iwe ni kwa jambo linalonihusu direct lakini si kama kwenye dhana kama hizi ambazo ndani yake kuna mengi yakudadavua
 
Mmh usitoe hukumu kwa haraka kiasi hicho mjadala bado uko hai usihofu
 
Hivi, huwa wanapata Mrejesho gani...!! pale wanapo jaribu kupima au kuchukua vipimo vya DNA (vinasaba) kwa viumbe wa kale (hii inaweza kuwa ni Siri) ili kujua chimbuko na asili MZUNGU alipotokea..!

Kwa sababu, kama anavyo sema Mshana Jr, hakuna vitabu vya Dini, wala vile vya Wanazuoni wa kale, vinavyo mzungumzia Mzungu na Asili ya kule alipotokea..

Yapo mengi (Mzungu) anayojaribu kwa juhudi kubwa, kuyafunika ama kuyapoteza, kwa nia ya KUFICHA alipo tokea.
 
Am sorry kwa hilo lakini nilitaka kujibu kwa pamoja ila reply yangu haikuonekana
Nimeweka hii mada kama hoja jadilika na ili iweze kuleta ushawishi ni lazima niwe na upande (mtazamo wangu unaweza kuwa na pingamizi nyingi) lakini mwisho wa siku ni kujifunza na kupanua ufahamu
Sipendi kuwa rigid kwenye mjadala labda tu iwe ni kwa jambo linalonihusu direct lakini si kama kwenye dhana kama hizi ambazo ndani yake kuna mengi yakudadavua

Asante Mshana Jr, sasa kama ulikusudia kuleta mjadala fikirishi (yaani wewe usiwe mjibuji) basi nafikiri ungeuleta kivingine kidogo.

Samahani kwa kusema hivi, lakini ukitazama wachangiaji wa mwanzo kwa sehemu kubwa walichukua kama facts na kumeza tu.
 
Hivi, huwa wanapata Mrejesho gani...!! pale wanapo jaribu kupima au kuchukua vipimo vya DNA (vinasaba) kwa viumbe wa kale (hii inaweza kuwa ni Siri) ili kujua chimbuko na asili MZUNGU alipotokea..!

Kwa sababu, kama anavyo sema Mshana Jr, hakuna vitabu vya Dini, wala vile vya Wanazuoni wa kale, vinavyo mzungumzia Mzungu na Asili ya kule alipotokea..

Yapo mengi (Mzungu) anayojaribu kwa juhudi kubwa, kuyafunika ama kuyapoteza, kwa nia ya KUFICHA alipo tokea.

Kabla ya kukujibu naomba kukuuliza, je wewe mpaka sasa umesoma au kupekua vitabu gani mpaka ukapata majibu uliyoondika hapa?

Nauliza kwa nia nzuri ya wazi hivyo uwe huru kueleza
 
Kihistoria advanced species walikuja na advanced tech, kipindi hicho baadhi ya maeneo yalikua yameungana, hata bahari.

Hivyo nyakati zingine watu wa kale walikua wanatembea kati ya bara na bara.

Mwalimu akaulizwa vipi kuhusu rangi? Kama wote asili ni ile na mtawanyiko ulikuja baadaye mbona wengine wakawa weupe, weusi n.k?
Akajibu stronger species survived, na strength ya kiumbe husika huonekana kwa jinsi gani atakavyoadapt mazingira yake, hivyo yale mabadiliko yaliyotokea ni namna ya kiumbe kuadapt mazingira yake kukisaidia katika survival.

Mabadiliko hayo yanajumuisha rangi.

Kuhusu dini, hata Histori inaikana dini inaihesabu kama kipumbazio kilichotumika kupumbaza watu.
Naona mambo ya NATURAL SELECTION
 
Back
Top Bottom