Kiba ile nyimbo tuseme ukweli tu, amekurupuka. Jamaa uwezo anao ila anafanya mambo kimazoea akitegemea media, alitakiwa ajenge fanbase kubwa na pia ajiandae kila mara akitoa nyimbo.
Mafanikio yanalala kwenye ubunifu si mazoea, kusema kweli toka atoe nyimbo ya Aje ngoma zilizofuata anaharibu. Anapanick.
Akataze kushindwanishwa na Diamond, si wa kiwango chake. Ndiyo maana jamaa kule akiachiwa jiwe likivuma unakuta anaingizwa upepo na presha juu, mashabiki na wapambe wanamchochea.
Unajua ushindani na aliyekupita, mwishowe unaharibu kila kitu.
Aepuke kushindanishwa na atulize kichwa chake, naamini jamaa uwezo bado anao. Asipelekeshwe na mashabiki.
Kubuma kwa viewers wasimtafute mchawi, kajiloga mwenyewe