Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Mimi ni nimetanguliwa na Dada zangu wawili,je Mimi ni mzaliwa wa Kwanza?
 
Ni kweli kabisa. Mimi ni mzaliwa wa kwanza. Hivyo nina ushuhuda wa kuthibitisha ukweli wa yote uliyaandika. Shetani baada ya kupambana sana kutaka kuniua kiroho alianzisha kampeni ya kutaka kuniua kimwili. Nayo ikabuma. Sasa hivi naona amekomaa kuniletea mawakala wake wanitege na kuniangusha kwenye zinaa. Mi namchora tu,anadhani mi zuuuuuzu!.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Aisee, somo linahusu kabisa halafu naliona leo!!!!???? Msomaji wa forum hii mara kwa mara, topic ina zaidi ya miaka miwili mimi siioni wakati mimi ni mzaliwa wa kwanza ambaye andiko zima linagusa. Ama kweli shetani yuko kazini! Kilangila.
 
Kweli!!!
 
Nina kaka yangu wa kwanza aisee kila siku ni majanga juzi kapoteza kipande cha mdomo alitoka kula vyombo
 
Duuu Huu Ukweli Kabisa Yaani Kwa Jinsi navyopambana na Maisha vikwazo daily but tutashinda na Zaidi ya kushinda
 
Duuu Huu Ukweli Kabisa Yaani Kwa Jinsi navyopambana na Maisha vikwazo daily but tutashinda na Zaidi ya kushinda
Pole sana mkuu usichoke wala uisikate tamaa. Aliyekuumba anakuona juhudi zako, one day jua litachomoza maishani mwako. Hata kamasio kwako basi kwa juhudi zako Wanaokufuata wataishi matunda ya juhudi zako. Kikubwa usisahau kusudi lako as mwana wa kwanza
 
Mimi ni nimetanguliwa na Dada zangu wawili,je Mimi ni mzaliwa wa Kwanza?
Obviously mzaliwa wa kwanza huwa Mwanaume hata kama katanguliwa na wakike unless kusiwe na mtoto wa kiume
client3
 
Mtoto wa kwanza huchukuliwa tahadhari zote kutoka kwa wazazi kwasababu mawindo ya shetani huwa ni kumuwinda mtoto wa kwanza na kumvuruga. (Chunguzeni watoto wa kwanza ambao hawako vizuri kiakili na kimaisha huenda walivurugwa na kuangukia sehemu mbaya na wakawa hivyo walivyo sasa)

Wazaliwa wa kwanza huwa wanafunzwa, wanasukumwa kufanya maonyesho. Hivyo matarajio ni makubwa kwa wazaliwa wa kwanza, haswa wavulana wazaliwa wa kwanza, kwa hivyo misukosuko ya shinikizo ni kitu ambacho wanajua kabisa tangu utotoni mwao.

Wanaume wazaliwa wa kwanza huwa wana nafasi ndogo ya kufeli kuliko wazaliwa wakwanza wasichana, au wale walio katika nafasi nyingine za kuzaliwa. Wavulana wazaliwa wa kwanza wanaogopa sana kushindwa hivyo mara nyingi huepuka maeneo ambayo hawawezi kufanya vyema.

Wazaliwa wa kwanza wanaweza kutoroka nyumbani ikiwa mazingira hayako vizuri, wanapoelekea huamini wanakwenda kufanya kazi nzuri zaidi kwasababu wanaogopa sana kuharibu mazingira.

Wazazi huwa wagumu zaidi na wakali kwa wazaliwa wao wa kwanza katika suala la nidhamu, na hulegea kadri wanavyosonga mbele zaidi katika familia. Wazaliwa wa kwanza kwa kawaida hawaitikii vizuri kwa kuwasili kwa mzaliwa wa pili.

Kwa mzaliwa wa kwanza, kuwasili kwa mtoto mwingine kunamaanisha jambo moja tu "Mfalme apoteza taji yake." Mtoto mzaliwa wa kwanza hufanya kila awezalo ili kushika nafasi ya kwanza iliyopendelewa. Ataonyesha mapungufu ya mzaliwa wa pili kwa wazazi wake.
 
Unaongoza kwa Ban jf
Tatizo linainzia kwenye kufuta comments. Wao hawataki nifute comment. Kuna muda unaweza weka comment za Kiwack baadae ndio unakuja kugundua kwamba ulicoment upuuzi. Sasa nikifuta tu nakula tofali
 
Nalimngoja bwana kwa zaburi, akaniiambia, akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibufu...akaisimamisha miguu yangu na akaziimarisha dua zangu
 
Pia ktk changamoto za mtoto wa kwanza ni pamoja na kukosea
Ndio maana wazazi huwa wakali kwa wazaliwa wa kwanza maana akikosea wanaomfuata wote pia hukosea au kutoka nje ya mstari
Shime vijana waliomo humu waelewe mtoto wa kwanza ni kioo cha wengine wote watakaofuata na ndio maana kila uchao viongozi wa dini utasikia tuwaombee uzao wa kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…