Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Embu naomba nikujibu mm na nitakujibu kwa kuuliza maswali,

Je unafahamu kama kigoma IPo karibu na Kongo?
kiukweli nilikuwa sifahamu mpaka nilipo enda kujiridhisha kwa kuangalia ramani. lakini mbona Kagera wapo karibu na Rwanda lakini kagera wana ka unafuu...awasumbuliwi sana kwenye maswala ya uraia.​
 
View attachment 2881093

Ukishazaliwa Kigoma au ukiwa na asili ya Kigoma jambo la kwanza unalotakiwa kuwa nalo (kichwani) kabla ya yote unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa maswala ya elimu ya uraia na utaifa. Kwasababu hiyo ndio fitina ya kwanza utakutana nayo pindi tu ukihitaji kujitanua kihimaya. Uraia ndio fimbo ya kwanza utayocharazwa nayo.

Mambo muhimu ni kuhakikisha kwamba makaburi ya wazee wako yanahifadhika kwa pande zote (ubabani na umamani). Hakikisha kwamba nyumba za wazee wako zinahifadhika haziuzwi wala kuvunjwa. Hakikisha kwamba ardhi yenu mnaitunza vyema, kumbukumbu za picha na mabaki ya historia muyahifadhi ipasavyo.

Watoto zenu anzeni kuwafundisha mapema namna ya kukabiliana na kasumba hii ya uraia inayotumiwa kama silaha kuwadhoofisha watu wa Kigoma.

Kwanini tunashauri mambo haya? Ni kwasababu nchi yetu pendwa bado haina njia sahihi ya kufanya verification ya uraia hususan kwa watu walio mipakani. Usumbufu umekithiri mno, na sasa imekua kasumba endelevu.

Sio ajabu tena muhamiaji haramu kuingia nchini, kupata haki zote kinyemela ikiwemo kuajiriwa na kuteuliwa katika nafasi za maamuzi.

Hawa watu wanapataje nguvu hiyo?
...........
Hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mifumo mizuri kwa watu wa mipakani, hususan huku kwetu Kigoma na watu wenye asili ya Kigoma.

Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopewa uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huu kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kama tunawapa watu uraia kwanini hakuna mifumo mizuri ya utambuzi kwa watu hawa? Kwanini bado wenyeji wenye asili ya Kigoma wanapitia madhila na kasumba ya uraia hadi sasa?

Kasumba hii imepelekea hofu kwa watu wa Kigoma, leo mtu wa Kigoma hawezi kuthubutu kusema kwamba ana ndugu Congo au Burundi.

Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi wamesoma hadi shule za Kenya, wana ndugu zao Kenya na Tanzania na wala hawapati usumbufu au ukakasi wowote.

Ukienda Mtwara, Wamakonde na Wayao wapo pande zote mbili za Msumbiji na Tanzania, wala hakuna shida.

Ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na Wazambia na Wamalawi, wameoleana mno, wafanyabiashara wengi wa Lusaka ni Wakinga na Wanyakyusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule Zambia.

Leo hapa mwanakigoma apite mpakani aseme naenda kusalimu ndugu zangu Burundi au naenda kwa ndugu zangu Congo. Basi na yeye atajumuishwa kuwa ni Mrundi au Mkongo.

Ukienda Moshi kwa Wachagga, na Wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili Tanzania na Kenya, nchi ya Kenya kuna eneo na kabila la Wameru.

Ni kawaida sana kumkuta mtu wa Tanga au Zanzibar ana ukoo wa mashangazi na wajomba huko Mombasa Kenya.

Mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote kwasababu watu wanaoleana, wanafanya biashara pamoja, wanazaliana na wengine wanahamia kabisa. Lakini huku kwetu Kigoma mambo yanakua ni tofauti. Dhiki na manyanyaso ya uraia yanazidi.

Je! serikali inasubiri nini kutatua fumbo hili la muda mrefu kwa wakazi wa asili ya Kigoma?

Ukijitambulisha wewe ni mtu wa Kigoma chakwanza kabisa mtu anakufikiria kunako uraia. Kanakwamba watu wa Kigoma ni raia daraja la pili. (Inaumiza sana kihisia na kiakili pindi unapowekewa mashaka).

Kigoma Region Tanzania
1. Ujifunze Kiswahili fasaha.
2. Namba 4 uitamke kama NNE na siyo INNE.
 
Ni kwasababu ya historia ya nchi zilizopakana na mikoa hiyo zote zilikuwa na machafuko hivyo mikoa hiyo ilipokea wakimbizi wengi na wengine waliingia kama wahamiaji Haram na kijichanganya mitaani
shida hapo ni uhamiaji haramu😭😭😭 nawaonea huruma sana ni kama wamepoteza urai😭😭😭😭
 
Sasa hivi Vipi ni Muha! Kuna Wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Kigoma! Wao wanasemaje na wanalionaje hili?

Au na wao wanatiliwa mashaka juu ya Uraia wao?
 
Shida ni muonekano kaka, hao wanafanana huwezi watofautisha kwa macho ila wengine sura zao na pua zao ndefu ndo zinawanyima fursa na kupelekea kubaguliwa
Wamasai wa Tz na Kenya wanatofauti gani? umewahi kuona masai anahojiwa uraia wake au mwarabu yoyote? nadhani kuna shida zaidi
 
Ati wamepewa uraia watu zaidi ya 200,000? Huo ni uraia hewa ndugu yangu kutengwa kupo pale pale miaka ya 70's watusi waliokuwepo kagera hasa kambi ya kimuli walipewa uraia na nyerere basi wakaishi mpaka wakazeeka na kufia hapo kagera sasa mwaka 2006 vizazi vyao vilivyobaki vikasombwa na kupelekwa Rwanda kwamba ni wahamiaji haramu wanarudishwa kwao, wengi wao hajui hata lugha ya kinyarwanda hawana ndugu huko ila ikabidi wapekwe tu bila kujali lolote. Utajiri wa kwanza ni watu sasa inakuwaje nchi inakataa watu? Tutapataje maendeleo bila watu? Na hii kasumba ya ukitaka kumdhoofisha mtu unamuita mkimbizi itaisha lini? Hayo tumeyaona na yanazidi kuongezeka ilikuwaga kigoma na kagera sasa hata geita na shinyanga ukizaliwa huko unaonekana ni raia wa mashaka, mwisho wa haya mambo lini? Yanafaida kwa nani?
Wewe kama ni mkimbizi rudi kwenu tu na hasa ukiwa ni Mnyarwanda na Mrundi ndiyo kabisaaa
 
Tatizo ni hulka za origin yenu hata kutaja hayo makabila naogopa. RIP Mtikila, C.
Wamejazana Mno Mishamo Huko, Nambuka Jiwe Aliwakataa Kuwapa Uraia Akawaambia Wazi Mnamiliki Mpaka Silaha Tutawanyoosha Hakuna Uraia
20240120_155935.jpg
20240120_121116.jpg
 
Hata wewe ni Mushuti tu ndiyo maana unajikombakomba kwa ccm
Uliiona spichi ya Chongolo alivyosema kwamba Mbowe babu zake ni watu wa Nyeri?

Heche ni raia wa Kenya, Isibania huko
 
Kigoma ni kwa sababu ya asili ya wahutu. Ni watu makatili sana. Ujambazi mkubwa Kagera na Kigoma ni wao.
Watusi nao wana ujinga wao ila sio makatili. Hii ndio sababu kuu
 
Mbona wahaya, wachaga, wanyakyusa,wameru, wajita n.k huwa hawasumbuliwi isipokuwa watu wa Kigoma pekee? kuna tatizo mahali
Hili halikubaliki,waulizwe waliowapa hizo nyadhifa za kwenye mamlaka ya maamzi ili wabebeshwe wao zigo na wawataje kwa majina kabisa hao raia wa kigeni.

Vinginevyo hizo ni siasa za majukwaani na siyo utaalamu.
 
Mchanganyiko wa watu wa mipakani, kabila moja kuwa nchi mbili tofauti pia ni faida kwa intelijensia, mawakala wana-move in and out unnoticed.

Na pia kama kabila halivuki mipaka ya nchi, adui akiingia ni rahisi kumjua kwa kuwa atashindwa kujichanganya.

Na pia kama kabila ni crossborder, ni rahisi kwa nchi kupandikiza watu wao kwa nchi jirani.

Wakati wa bifu la JK na Kagame, Kagame alikuwa na watu wake wengi wako Tanzania wanajifanya wafugaji.

Na Tanzania ina watu wake Rwanda mipakani kote, wakifuatilia kama kuna movement zozote za kijeshi mipakani watoe taarifa nyumbani.

The immediate former RC wa Kagera Major General Gaguti, the genious millitary personel, amefanya patrol sana katika border za mkoa wa Kagera, tena kwa miaka mingi kabla ya kuwa RC, anajua mpaka mazalia ya panya na senene maeneo ya mipakani mkoa wa Kagera.
 
Ndugu watu wameishi vizazi na vizazi hawajafanya baya lolote leo unawafananisha na hamasi? Hii chuki imepitiliza sasa
Sija wafanananisha na hamas, halafu ngoja nikwambie kitu hamas unao waona wewe ni magaidi Kuna watu wanaeaona ni wakombozi wao the same hao unaowaona ni wema kwa kua wameishi miaka na miaka Kuna watu wanawaona sio watanzania na bado wanauzalendo na taifa lao la asili hivyo ni Bora wakakae huko huko kwenye taifa lao la asili

No hate ✌️
 
Back
Top Bottom