Je, Yanayotokea Iran ni Utimilifu wa Unabii wa Yeremia Sura ya 49?

Je, Yanayotokea Iran ni Utimilifu wa Unabii wa Yeremia Sura ya 49?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Mijadala imekuwa mingi juu ya unabii ndani ya biblia uliotolewa na nabii Yeremia, Yeremia 49 kuhusu nchi ya Elamu, ambayo ni Iran ya leo. Nabii Katika kufafanua zaidi juu ya unabii huo, Pirooz Abir, muiran mwenye asili ya Kiyahudi, ambaye anamwamini Yesu kuwa ndiye Masiha, anachambua mambo mengi kwa mtizamo wa kiimani na uhalisia:

Pirooz Abiri anasema:
Elam imetajwa mara nyingi kwenye Biblia, ikiwa ni pamoja na unabii wa nini kitatokea kwa nchi ya Elam, inayojulikana leo kama nchi ya Iran. Anasema, Kichwa changu kinazunguka nikifikiria yanatakayoipata Iran kutokana na unabii.

Pirooz alizaliwa na kukulia Iran kwenye familia ya Kiyahudi, lakini baadaye alibadili imani na kuwa mkristo baada ya kuhamia Marekani. Pirooz ameamua kuwashirikisha watu wengine juu ya unabii wa Yeremia kuhusiana na Iran.

Unabii Wenyewe:
Neno likamjia nabii Yeremia kuhusu nchi ya Elam, wakati wa kipindi cha mwanzo cha mfalme wa Yudea, mfalme Zedekia, likisema: Hivi ndivyo asemavyo BWANA, nitaivunja Elam, na ukubwa na nguvu zake, na kuwapelekea WaElam dhoruba nne kutoka robo zote 4 za mbingu, nazo zitawatawanya Waelam Dunia nzima, hata kusiwepo nchi ambayo haitakuwa na Muelam.

Nitamtia woga Elam mbele ya maadui zake, nitawapalekea machafuko, nitawapelekea hasira yangu, asema Bwana. Nitampelekea upanga, hadi niwamalize, nitasimika utawala wangu, na kumwangamiza mfalme wake na viongozi wake, asema BWANA. Lakini kwa siku za mbeleni, nitaiinua tena nchi ya Elamu (Yeremia 49:34-39).

Pirooz anasema kuwa unabii huu unazidi kutimia, anasema angalia wairan walivyokimbilia mataifa mbalimbali, yeye akiwa mmojawao. Pirooz anasema kuwa hili suala la wairan kutawanywa Dunia nzima limekuwa likitokea na kuendelea kwa kasi zaidi tangu mwaka 1979, japo sasa limefika kileleni.

Kuhusu Mungu kusimika utawala wake kwenye nchi ya Elam, Pirooz anasema anakumbuka pale mchungaji mmoja alipofukuzwa toka Iran, akakimbilia Marekani, alipoulizwa ni waislam wangapi walikuwa wamebadilika na kuwa Wakristo, akasema kuwa yeye hana uhakika, yaweza kuwa ni milioni 1, lakini afisa wa Serikali ya Iran akasema kuwa siyo milioni 1, waislam kati ya milioni 6 mpaka 8 wamebadilika na Wakristo. Anasema kuwa hiyo ilikuwa ni miaka mingi iliyopita, nani anajua wapo wangapi kwa sasa?
Pirooz asema kuwa kwa uhakika, kama ilivyotangazwa na Iran International outlet, mpaka mwaka 2023, misikiti 75,000 imefungwa, kwenye maandamano ya karibuni misikiti mingi ilichomwa moto.

Kutokana na utafiti wa shirika la Iran linalojishughulisha na uchunguzi, linasema kuwa kuna mamilioni ya wakristo nchini Iran.
Pirooz alipoulizwa hao wakristo wa huko Iran wanafanyaje nyakati ngumu kama hizi za vita, alisrma kuwa Wakristo wa Iran ni watu wenye imani kubwa kwa masiha Yesu Kristo, kiasi kwamba wapo tayari kufa lakini wafe mikononi mwa Kristo. Anasema kuwa wakristo wa Iran, siyo tu wanamfuata Yesu bali wamejikabidhi kwa Yesu.

Kuhusu Mungu kuwa kinyume na watawala wa Iran, na kwamba atawashusha na kuuangamiza utawala wa Iran, mfalme wao na viongozi wao, anasema walianza kuyaona hayo yakitokea tangu ile mwakajana pale ambapo Israel na Marekani walipopiga vibaya vinu vya nyukilia. Anasema kuwa kinachotakiwa sasa, siyo kuiomba Israel au Marekani walete amani, bali inatakiwa kumwomba Mungu.

Note: Ujumbe muhimu ni kuwa kufuatana na unabii huu wa Yeremia, Iran itapigwa, utawala utaondoshwa, Wairan wengi wataikimbia Iran, kisha Mungu atasimika utawala wake, na baadaye Iran itainuka, na kuwa taifa lenye baraka kwa sababu litakuwa chini ya utawala wa Mungu.

Tusije kushangaa Iran ikawa ndiyo mlango wa kuibuka na kurudi kwa ukristo wenye nguvu Mashariki ya kati, kama ilivyokuwa pale ulipoanza. Ongezeko la kasi la wakristo nchini Iran katikati ya vitisho kwa wote wanaobadili dini, haiwezi kuwa ni nguvu ya awaida. Bila shaka kuna nguvu ya Mungu. Wakristo wa Iran hawana tofauti na wale wa enzi za mitume, waliosimama imara katikati ya mateso na vitisho vya kila namna.
 
Kwanza: Elamu si Iran ya leo kwa maana ya kisiasa.
Elam ilikuwa ustaarabu wa kale uliokuwepo kusini magharibi mwa Iran ya sasa (eneo la Khuzestan). Ilikuwa ni taifa la kale lililokuwepo maelfu ya miaka kabla ya taifa la kisasa la Iran. Hivyo, kulinganisha moja kwa moja Elamu na Iran ya leo ni kurahisisha historia kupita kiasi.

Pili: Unabii huo ulitolewa katika mazingira ya wakati wake.
Katika Book of Jeremiah hasa Jeremiah 49, unabii ulihusu mataifa yaliyokuwa jirani na Yuda katika karne ya 6 KK. Nabii alikuwa akizungumza kuhusu matukio ya kisiasa ya kipindi hicho, si kuhusu siasa za karne ya 21.

Tatu: Historia inaonyesha kuwa unabii huo tayari ulitimizwa zamani.
Nguvu ya Elamu ilivunjwa na himaya zilizokuja baadaye kama ile ya Babylon na baadaye milki ya Persian Empire. Baada ya hapo Elamu ilipoteza uhuru wake wa kisiasa na kuunganishwa ndani ya himaya kubwa. Wanahistoria wengi wanaona matukio hayo kama utimilifu wa kile kilichoandikwa na Yeremia.

Nne: Kutawanyika kwa Wairan duniani si ushahidi wa unabii.
Kila taifa lina diaspora duniani. Wachina, Wahindi, Waarabu na hata Waafrika wako kila bara. Hivyo uwepo wa Wairan katika nchi mbalimbali hauwezi kuwa ushahidi maalum wa utimilifu wa unabii.

Tano: Takwimu zilizotajwa hazina vyanzo huru vinavyothibitisha.
Madai ya kufungwa kwa misikiti 75,000 au mamilioni ya Waislam kubadili dini yanahitaji uthibitisho kutoka tafiti huru za kimataifa. Bila ushahidi wa kuaminika, yanabaki kuwa madai tu.

Sita: Tatizo la mantiki (confirmation bias).
Watu wengi huchukua tukio lolote la sasa na kulifananisha na maandiko ya kale ili kuthibitisha imani zao. Lakini hawachunguzi kama maandiko hayo yalikuwa yakizungumzia mazingira ya wakati wake.

HIVYO, Unabii wa Yeremia kuhusu Elamu unaeleweka vizuri zaidi katika muktadha wa historia ya Mashariki ya Kati ya karne ya 6 KK. Kuuunganisha moja kwa moja na matukio ya leo ya Iran ni tafsiri ya kiimani, si hitimisho la kihistoria au kielimu.
 
Mengine uliyoyaandika, nadhani hujafuatilia kwa umakini:
Elamu hapao kale ilikuwa ni utawala unaojitegemea, lakini kwa sasa eneo lililokuwa likiitwa Elam hapo kale ni sehemu ya majimbo ya Iran, mojawapo ni hilo jimbo ulilolitaja, jimbo la Khuzistan. Hilo ni miongoni mwa majimbo 31 ya nchi ya Iran.
Kuhusu idadi ya misikiti iliyofungwa Iran, unaposema kuwa inatakiwa kutolewa na taasisi zinaxojitegemea, unataka taasisi gani, wakati kuna taarifa nyingi za taasisi mbalimbali zimekwishawahi kutoa hizo takwimu? Hata Ayatollah, bila ya kusema kuwa misikiti hiyo imefungwa kwa sababu ya watu kubadili dini, kwenye taarifa rasmi aliwahi kulaumu na kuwaasa wauslam kusimama katika dini yao, na kusema kuwa kulikuwa na misikiti 50,000 iliyokuwa imefungwa kutokana na kukosa waumini.

Kuhusu ongezeko kubwa la wakristo nchini Iran, ni taarifa ya kutoka source mbalimbali zinaeleza kuwa Iran ndiyo nchi inayoongoza kwa ongezeko kubwa la converts wa uislam kwenda ukristo, japo wanatofautiana katika idadi.

Key Countries and Regions Leading in islam to christianity Conversions:
  • Sudan & Africa: Sudan has experienced a massive shift with millions converting. Nigeria, Kenya, and Ghana also report significant numbers of Muslims turning to Christianity.
  • Middle East & Central Asia: Iran, despite strict laws, has seen over 1 million conversions. Other notable countries include Afghanistan, Iraq, Turkey, and Saudi Arabia.
  • Asia: Indonesia is experiencing rapid, though sometimes underground, Christian growth.
  • Europe: France, Germany, Austria, Belgium, and Sweden have reported a rise in conversions, particularly among muslim refugees

Why are so many Iranian Muslims converting to Christianity?
Muslims convert to Christianity for various reasons, often citing personal spiritual experiences like dreams or visions of Jesus, a desire for a more personal relationship with God emphasizing grace and unconditional love.
 
Unachofanya hapa ni anachronism, kuchukua maandiko ya kale na kuyapachika kwenye siasa za leo.

Elam ilikuwa ustaarabu wa kale uliokuwepo maelfu ya miaka kabla ya taifa la kisasa la Iran. Unabii wa Book of Jeremiah sura ya Jeremiah 49 uliandikwa katika muktadha wa migogoro ya karne ya 6 KK kati ya Yuda na mataifa jirani.

Kihistoria, nguvu ya Elam ilivunjwa na himaya kama Babylon na baadaye ikaingizwa katika milki ya Persian Empire. Hapo ndipo wanahistoria wengi wanaona utimilifu wa unabii huo.

Kuhusisha diaspora ya Wairan au migogoro ya leo ya Iran na unabii huo ni tafisiri ya kiimani, si hitimisho la kihistoria.

Kwa kifupi: Historia inaelezea maandiko hayo tayari, si lazima kuyatafsiri upya kila tukio la kisiasa la leo.
 
Back
Top Bottom