GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kwa hizi Mvua Kubwa na nyingi zinazonyesha sasa Nchini Tanzania nimetaarifiwa kuwa tayari zimeshaanza Kujaza Mito yetu Mikubwa kiasi kwamba muda si mrefu inaweza ikaanza Kufurika na kujuta hata kwanini kwa Uwongo, Roho Mbaya na Propaganda zetu tuliamua Kumtupia lawama Mchina Mkulima wa Ruvu kuwa ndiyo pekee anazuia Maji kutopatikana Mkoani Dar es Salaam na Kukatikakatika hovyo kwa Umeme wa Tanesco.
Je, huu siyo wakati mzuri wa Kumruhusu Yule Mchina Mkulima aendelee kuyatumia kwa Kumwagilia Mazao yake kwani tayari Mkoa wa Dar es Salaam Maji yanatoka mengi, Visingizio vya Kutokuoga vimeshapungua sasa na Umeme haukatiki tena na tishio la kuwepo kwa Mgao haupo?
Tanzania ndiyo Nchi pekee duniani ambayo ina Watendaji na Viongozi wa 'ajabu ajabu' mpaka kwa Maamuzi yao ila ndiyo hao hao kila Siku wanapata Doctorates ( PhD's ) ambao furaha yao Kubwa ni kuona Wanaandikwa au Wanatajwa kwa Neno la 'Dakta' fulani.
Tafadhali hebu mruhusuni haraka huyo Mwekezaji ( Mkulima Mchina ) mliyemzuia asiendelee Kuyachepusha Maji ya Mto Ruvu kwa Kumwagilia Mashamba yake aendelee Kuyachepusha ili Mazao yake yakue haraka na yawe kwa Wingi kisha yake Kuuzwa Mkoani Dar es Salaam ambapo hivi sasa Bei ya Mboga za Majani, Pilipili ( ambazo GENTAMYCINE napenda mno Kula ) pamoja na Matunda zimepanda maradufu.