Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?


- Mkuu Masatu heshima mbele, toka jana nimekuwa nikizuiwa kuingia kutoa mawazo yangu kama yako kwa sababu sikubali mawazo ya mkubwa mmoja, wewe mkubwa I hope unazo nguvu kweli,

- Maana kama ni hizo nguvu uwe nazo kila kona sio JF tu! kwa sababu na wengine tunazo sehemu zingine ambazo huna, sasa it is only a matter of time!, hii ni mara ya pili unacheza huu mchezo, wewe umeanza kuna siku na mimi nitamalizia, ili nione kama kweli unazo hizo nguvu kila kona! That is a promise!

Respect.

Field Marshall Es!
 

Zitto alitangaza kugombea na kisha akachomoa (sioni connection yoyote ya kukemea maovu ya Chadema). Kabla ya hapo, Zitto alifanya yafuatayo-

1. Alijiunga na kamati ya madeni ya Kikwete (akipingana na wenzake)
2. Aliungana na mafisadi kwenye issue ya Dowans
3. Hakujulikana msimamo wake kwenye bajeti ya serikali iliyopita.

Kukosa msimamo kwenye mambo muhimu ndiko kumemtoa Zitto kwenye hiyo sifa unayojaribu kumpa kuwa yeye ni mpiganaji kwenye vita muhimu ya kumletea mtanzania maendeleo (haya ni maoni yangu).

Hayo mengine ya uchaga na chadema nadhani unarudi kule kule kwenye ukabila na chuki zisizofaa ndani ya nchi na hivyo kukufanya wewe kuwa mtu mwenye chuki mbaya sana za kikabila na unayefaa kuogopwa kama ukoma.
 

Huyu anayezuia watu kuchangia ashindwe na alegee.
 
Huyu anayezuia watu kuchangia ashindwe na alegee.

- You might be a smart man!, ila kwenye maisha huwa kuna kuzidiana ujanja na dunia ni ndogo sana sio kubwa sana.

- Sisi tunakuja kujadili taifa hapa kumbe kuna ambao wana agenda zao za kutumwa na wanasiasa mafisadi humu, atleast sasa I am glad kwamba nimeelewa maana kweli among all the people it was the right thing sana kunifanyia mimi, wazee wa sauti ya umeme, sasa ni zamu yangu kujibu, and I will.

Respect and Out!

FMEs!
 
- You might be a smart man!, ila kwenye maisha huwa kuna kuzidiana ujanja na dunia ni ndogo sana sio kubwa sana.


Vitisho tena?!

Respect and Out!

FMEs!

Na hao wenye agena zao ni kina nani? Wataje tu ili wajulikane na hoja zitajibiwa kwa hoja.
 
[/SIZE]

Vitisho tena?!



Na hao wenye agena zao ni kina nani? Wataje tu ili wajulikane na hoja zitajibiwa kwa hoja.


- Ninaamini message imefika sina sababu ya kuongeza zaidi, have a nice day mkuu! Bwa! ha! ha! ha! ha!

Respect.

FMEs!
 
- Demokrasia ni kazi sana imeshinda hata wenye akili sana, kuliko zako mkuu, Bwa! ha! ha!.

Later!

FMEs!

Demokrasia imewashinda hata wale wanaojiita kuwa mababa wa demokrasia duniani (wamarekani) ije kuwa mimi.

Bwa ha ha ha ha ..... Later
 
Nishawahi kusema kuwa Zitto sasa alikuwa amejaa kiburi sana na pengine kujiona kuwa ni yeye ndio Pekee katika CHADEMA. Kuna watu wengi sana katika CHADEMA kuwa lakini sio Active katika Politics za Tanzania. Lakini Zitto alikuwa ana jaribu hata timing yake ilikuwa Mbovu sana. Nilikasilika sana kuona anasema na kumwaga mambo haya hapa JF. Zitto sasa alishapoteza Dira yake Siku nyingi sana
 
 


Hii imekaa kama ya CCM jinsi baadhi ya wazee wanavyopinga watu kuchukua fomu kugombea Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2010.
Je hao wanahisi Kikwete hawezi kusimama na mgombea mwingine ndani ya CCM na akapita?
Ni rekodi ya uongozi inamsuta au???


All in all, Zitto alichemka sana alipounga mkono ule mpango wa Serikali/Ngeleja wa kununua mtambo wa Richmond/Dowans huku akijua hiyo inakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Zitto alijua kabisa kuwa suala hilo si la Kamati yake ya Hesabu za Mashirika ya Umma, bali ni la Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti Shelukindo, ambaye kwa ujasiri aliingilia kati na hivyo kuokoa pesa za walipa kodi yaliyotakiwa kuchotwa kwenye 'dili' hiyo.

Hii iliongezewa nguvu na ufafanuzi wa kanuni uliotolewa na Spika Sitta.

Ukichunguza media coverage, hivi sasa ni vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM, Serikali na viongozi wa CCM ndio vinamshabikia. Hii imekaaje?


Ila hilo la Dowans analo tu...

 
Duh...kumbe Zitto ndani ya Chadema yupo na Mama yake pia.

Ha ha ha ha,

Labda mama yake Zitto naye ni mchaga maana sasa hivi wachaga wamejaa kila sehemu hapo Tanzania hadi inakuwa kazi kuwatambua.
 
Zitto alitangaza kugombea na kisha akachomoa (sioni connection yoyote ya kukemea maovu ya Chadema).

Zitto alishauriwa na "wazee wa chadema" hasigombee. Ni dhahiri hakujitoa kwa matakwa yake. Huu ni ukiukaji wa democracy ndani ya chadema. Katika hotuba zake mara nyingi amekuwa akiguswa na kufukuzana kulikoshamiri ndani ya chadema na ufujaji wa fedha za Chadema.

Kabla ya hapo, Zitto alifanya yafuatayo-

1. Alijiunga na kamati ya madeni ya Kikwete (akipingana na wenzake)
2. Aliungana na mafisadi kwenye issue ya Dowans
3. Hakujulikana msimamo wake kwenye bajeti ya serikali iliyopita.

---Nini kazi ya upinzani kama si kushirikiana na chama tawala kuleta maendeleo? Zitto anakosa gani kujiunga na kamati ya JK?

---Kwani upinzani ni kupinga kila kitu? Huo msimamo wa bajeti, ni wabunge wangapi msimamo wao unajulikana hata ndani ya ccm?

Chadema kweli hamnazo; yani you are so concerned na kuropoka kwa Zitto hata kama yote aliyoyasema ni ukweli 100%. Lakini kuweni makini, mana ni vigumu sana kuuficha ukweli.
 
 

Kama yeye mwenyewe amesema kuwa anakubaliana na ushauri wa wazee na kujitoa basi jamii itamchukulia Zitto na maneno yake. Hayo mengine ni ya kwako mwenyewe.



Ni kweli sio kazi ya upinzani kupinga kila kitu au kutoshirikiana na chama tawala kwenye maendeleo ya nchi.

Lakini kumbuka kuwa, kamati ya madini ni kitu tofauti. Kabla ya hii kamati ya Zitto, kulikuwa na kamati na tume kibao zimeundwa kuchunguza na kutoa ushauri kuhusu masuala ya madini. Kabla hayo mapendekezo ya kamati na tume zilizopita hayajafanyiwa kazi, kamati nyingine ikiundwa ni upotevu na uharibifu wa muda na pesa za watanzania.

Zitto alilijua hili, aliambiwa na wenzake kuhusu hili lakini bado tu alijiunga na Kikwete kuwapotezea muda na pesa watanzania. Je ile kamati ya Zitto imeleta nini tofauti na kile kilicholetwa kabla?

Je issue ya Buzwagi ambayo ndiyo ilianzisha yote haya ilishughulikiwa? Kuna wakati chama kilicho madarakani.

BTW ... kuita watu kuwa hamnazo hakujengi hoja yako zaidi ya kukuonesha vile ulivyo. Mtu mwenye chuki za ajabu (ohh nimekumbuka, kuwa ulipondea wachaga somewhere hapo juu) za kikabila.
 
 

Mkuu kuhusu Zitto kuingia kamati ya madini kuna kasoro moja kubwa sana. Zitto anawakilisha sera za Chadema ambazo zinahitaji nci yetu kuwa na hisa katika amshirika ya madini. Sasa ikiwa serikali yetu haina hisa ndani ya mashirika hayo, hakuna sera wala kifungu cha mtazamo wa chama chake (Chadema) umekubalika na serikali kuu kutumiwa ili kuboresha sekta ya madini. Zitto hakutakiwa kufanya kazi huko kwa sababu ni Kinyume cha katiba ya chama chake.
Siku zote wabunge wanashirikiana na serikali kuu ikiwa tu serikali kuu itakubali kubadilisha baadhi na sera zake na kufuata mkondo wa kati kaisi kwamba hata Wapinzani wanakuwa na mchango wa sera zao.. Lakini sii mtu kuingia kamati ambayo malengo yake ni kinyume kabisa chga mtazamo wa chama chako..
Anyway haya yalikwisha pita.. Zitto alichemsha, akachemsha na anaendelea kuchemsha kutokana na tatizo kubwa na siasa nchini. Yaani vyama vyote vya siasa havina mrengo, Zitto ni Conservative na anahusudu mrengo huo wakati Bongo kila mtu ana dini yake lakini unaambiwa nchi haina dini..hivyo hivyo principal hiyo ipo ktk Mrengo..
Hivyo itakuwa shida sana kwa wananchi kumwelewa Zitto na msimamo wake..Hii haina maana hafanyi makosa.
 
Last edited:

Omar,

Nilikuuliza jana kama unamsemea Zitto au unasema kwa niaba yako. Zitto alidai kuwa anaandamwa na wamachame (na wachaga?) lakini baadaye akaonekana kuback down.

Naona wewe leo umekuja full ... kudai kuwa Zitto anaandamwa na watu wa dini na kabila tofauti na Zitto.

Unaamini kuwa wanaompinga Zitto hapa na kwingine wanafanya kwa vile wao sio kabila au dini moja na Zitto! are you serious?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…